ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

Alietoa na aliepokea rushwa wote ni wahalifu, mzee nae alitakiwa awe ndani wakati uchunguzi ukiendelea, haiwezekani profesa mzim ukatoa rushwa kirahisi hivo bila kua na uhalifu wowote,

Inafikilisha hii isije ikawa anajifich kwenye kivuli cha uzee kuficha maovu
 
Polisi wengi hasa hawa wapelelezi wanaUKWASI wa kutisha sana. Shida ni maadili ya kazi yamepotea sasa askari mdogo anatumwa na mkuu wa kituo akamchukulie rushwa unadhani kuna maadili tena hapo. Vituo vingi vya polisi vimekuwa mahala pa kuchukulia hela. Mfano hapa kimara mwisho ni rushwa tupu hakuna uadilifu tena. Serikali ingelisafisha jeshi la polisi kwa ujumla wake.
 
...Nimvekwazika kidogo hapo Mkuu. Kama huyu Profesa naye alikuwa ni Msafi na hana Mazonge zonge yoyote, kwa nini alitaka kuwapa hao makalamba hela yote hiyo wakati moyomi ansjua yupo safi na hana kosa lolote?
Inafikirisha.
Mzee kama huyo aliogopa kupewa kesi ya uhujumu uchumi akafikiria na reputation yake mbele ya jamii itakuaje akaona amalizane nao.

Lkn baada ya kutuliza kichwa akaona huu ni ujinga lazima nidili nao hawa.
 
Huyo Prof. naye TAKUKURU wamfungulie mashitaka kwa kushawishi kutoa rushwa(Corruption transaction) kama alikuwa hausika kwanini aogope kufikishwa mahakamani ili mahakama itoe maamuzi kama alibambikiwa kesi au la, hayo meno ya kwenda kumbambikizia yeye hao askari waliyatoa wapi kama si walipata taarifa kutoka wa raia wema kuwa kuna pembe za ndovu shambani kwa huyo mzee.

Jeshi la POLISI na TAKUKURU wachunguze account za huyo mzee na wapime biashara zake kama kwa haraka tu ametoa milioni mia inatia shaka.Kosa la hao askari ni kukubali kupokea rushwa baada ya kushawishiwa na mtuhumiwa.
Mil 100 unaona ni nyingi sana?

Hizo ni nyingi kwa wanyonge lkn ungemjua huyo dingi na mishe zake ungeona hio hela ni ya kawaida tu.
 
Tafuta CV ya Prof.J. Maeda. Utagundua ulichoandika umepoteza muda.
CV. peke yake haitoshi kuwa sababu ya yeye kushindwa kujihusisha na makosa ya kiuhalifu wa kutaka kupata pesa nyingi kwa muda mfupi na ukizingatia yupo jirani na hifadhi si mgeni na pembe za ndovu kuna wasomi wana CV nzuri lakini wanapiga dili mpaka unashangaa,ninachotaka kusema uchunguzi wa kutosha ufanyike na huyo Prof.asipoitwa na TAKUKURU kuhojiwa kwanini alijihusisha na kushawishi na utoaji rushwa kama sheria inavyosema mtoaji na mpokeaji wote wana kosa la kujibu hapo tutakuwa na safari ndefu ya kupambana na kuzuia vitendo vya rushwa ambapo mpaka msomi ambaye Prof.aliyetumikia taifa kwa muda mrefu mpaka amestaafu leo hii anaongozana na watu kwenda benki kutoa pesa na kutoa hongo ili asifikishwe mahakamani inasikitisha sana.
 
Askari Polisi saba wakiwemo watano wa kituo cha Polisi Usa Wilayani Arumeru Mkoani Arusha na wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha wamefukuzwa kazi kwa fedheha kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 100.

Wiki iliyopita Kamanda wa TAASISI ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini {TAKUKURU}Mkoani Arusha,James Ruge alikiri kuwakamata askari hao kushawishi na kupokea kiasi hicho Cha fedha ili wasimfungulie Kesi ya uhujumu uchumi ambapo angefia gerezani.

Hata hivyo Ruge alisema uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika na ukikamilika atatoa taarifa kwa vyombo vya Habari juu ya makasa mzima.

Vyanzo vya Habari vilisema kuwa mienendo ya mashtaka ya kijeshi ya kipolisi ilifanyika katika tarehe Aprill 22,23,24 na tarehe 25 mwaka huu , ambapo Askari hao walifukuzwa kazi rasmi ndani ya jeshi la polisi na sasa wanasubiri kushitakiwa katika Mahakama za kiraia wakati wowote.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo alipoulizwa juu ya jeshi hilo kuchukua hatua hizo alisema kuwa hayo ni mambo ya ndani ya Polisi na sio rahisi kutolewa hadharani kwani ni kinyume na maadili ya kazi.

Naye mhanga wa tukio hilo ambaye ni mfanyabiashara wa mji wa Usariver,Profesa Justin Maeda{77}akizungumza nyumbani kwake katika Kijiji cha Nshuku kata ya Nkoaranga wilayani Arumeru alisema pamoja na mkasa wote alioupata na kuishukuru Polisi kwa hatua walizochukua ila amesikitishwa na kitendo cha polisi hao kukiuka maadili ya kazi na kuomba rushwa katika kituo cha Polisi Usa hatua ambayo ilimshangaa na kushindwa kujua OCD na OC CID washindwe kujua tukio hilo.

Profesa Maeda ambaye alianza kufundisha UDSM Mwaka 1970 na kuwafundisha viongozi wengi wa serikali kabla ya kuwa Mshauri Mkuu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1981-1985 Ikulu sasa ameanza kuamini maneno ya watu wa Usa kuwa ndani ya kituo cha polisi Usa kinanuka rushwa na kuna askari wa kituo hicho kitendo cha upelelezo ni miungu mtu kwani wako hapo kwa miaka mingi sasa wamejivika ufalme wa kuomba kiasi chochote cha rushwa ndani ya kituo mhicho bila kuogopa chochote.

Alisema kama yeye amebambikiwa kesi ya nyaraka za serikali na kuchomekewa shambani kwake na kutakiwa kutoa rushwa ya shilingi milioni 200 kabla ya kufikia makubaliano ya shilingi milioni 100 kuna raia gani Arumeru wameshafanyiwa unyama wa aina hiyo kwani hiyo ni hatari na viongozi wakuu wa polisi Mkoani Arusha na Makao makuu wanapaswa kutupia macho zaidi kituo hicho maana dhuruma na uhuni umekithiri kupita kiasi hivyo hatua zinapaswa kuchukuliwa sasa.

Profesa Maenda ambaye ana Mke na Watoto watatu ambao wote wako nje ya nchi alisema polisi hao ambao walikuja nyumbani kwake na gari mbili za polisi marchi 19 mwaka huu majira ya kati ya saa 7 mchana na saa 8 wakiwa wamejaa kwenye gari na wakiwa na silaha na gari ndogo aina ya Rv4 ambayo hakufanikiwa kushika namba walijitambulisha kuwa ni polisi ya Us ana makao makuu na alimtambua mmoja{jina tunahifadhi} wameagizwa kwenda kwake kupekua kwa kuwa wanataarifa za kiitelejesia kuwa anafanya biashara ya nyara za serikali ikiwemo meno ya tembo na Ngozi za chui.

Alisema kwa kuwa hajawai na hajui kitu kinaitwa Nyara za serikali na hajawahi kufanya biashara hiyo aliwaruhusu kufanya upekuzi lakini cha kushangza hawakufanya ndani ya nyumba bali walikuwa wakipita nje ya kwenda moja kwa moja shambani kwenye mizinga ya nyuki.

Profesa ambaye ameshafanya kazi UN hususani UNICEF nchi mbali za kiafrika na kumalizia nchi ya Zimbabwe mwaka 2002 alion aaskari mmoja akichukua mzinga na kutoa ndani ya mzinga kitu alichodai ni meno ya tembo na kusema hicho ndio kitu walichokuwa wakikitafuta.

Alisema kuwa yeye alisema shambani kwake hukaa zaidi ya miezi miwili au mitatu kuingia hivyo aliwauliza askari hao hii imeletwa na nani kwani hajawahi kufanya biashara hiyo ila alijibiwa na askari hao kuwa hiyo imekula kwake kwani hii ni kesi ya uhujumu uchumi na angefungwa Maisha hivyo anatakiwa kuweka mambo sawa.

Mzee huyo ambaye isema alistaafu miaka ishirini iliyopita alilipwa kiinua mgongo chake{PENSHENI} cha kiasi cha shilingi milioni 74 na kuweka benki ya CRDB na NMB alichukuliwa hadi kituo cha polisi Us ana kuanza kuchukuliwa maelezo na kuombwa rushwa ya shilingi milioni 200 wakati akitoa maelezo.

Profesa alisema yeye aliwaambia kuwa jana yake yaani marchi 18 mwaka huu alikwenda benki na kuchukua kiasi kidogo cha pesa hivyo kiasi hicho hana na kuwataka wapokee milioni 100 na ndipo alipokwenda benki akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi na kuchukua shilingi milioni 74 na baadae alikwenda dukani kwa mdogo wake hapo Usariver na kuchukua kiasi cha shilingi milioni 30 na zote aliwapa polisi katika kituo cha Usa kwani rushwa ilifanyika hapo.

Alisema na kuiomba serikali iweze kumrudishia kiasi cha pesa yake kwani ni kiunua mgongo cha utumishi wake wa kazi wa miaka mingi kazi.

Mwisho

Angesemeaga 250m ndio ako wamechukua
Usa sio kama Tanga. Tanga ukiwaambia takukuru mambo yako wanamtafuta mlengwa na kula hela. Ukikutana na mlengwa anakuambia kila ulichosema huko. Jamani jamani Tanga eeeee Mungu waonee watu wako huruma. Japo mkuu wa takukuru alisimamishwa kazi lakini hakuna jipya sana. Hongereni takukuru huko Arumeru.
Wizara Katiba Na Sheria kuna mutu inalalamikaga kuhusu @takokuru tanga please report the case and save the community
 
CV. peke yake haitoshi kuwa sababu ya yeye kushindwa kujihusisha na makosa ya kiuhalifu wa kutaka kupata pesa nyingi kwa muda mfupi na ukizingatia yupo jirani na hifadhi si mgeni na pembe za ndovu kuna wasomi wana CV nzuri lakini wanapiga dili mpaka unashangaa,ninachotaka kusema uchunguzi wa kutosha ufanyike na huyo Prof.asipoitwa na TAKUKURU kuhojiwa kwanini alijihusisha na kushawishi na utoaji rushwa kama sheria inavyosema mtoaji na mpokeaji wote wana kosa la kujibu hapo tutakuwa na safari ndefu ya kupambana na kuzuia vitendo vya rushwa ambapo mpaka msomi ambaye Prof.aliyetumikia taifa kwa muda mrefu mpaka amestaafu leo hii anaongozana na watu kwenda benki kutoa pesa na kutoa hongo ili asifikishwe mahakamani inasikitisha sana.
Mbona ako amesha-justify kwanini vile alikubali kuwapa iyo pesa wako wanaidemand? You better listen to understand before rushing into arguments
 
Wakat anakusanya izo hela mda wote huo alishindwa kuwasiliana na takukuru ili awakamatishe mazima kuliko kutoa then kulud mda mwingine ambapo ushahidi ushapotea, uyu mzee kuna kitu nyuma ya pazia, ila kwa sababu ana mkwanja mrefu ndo maana unaona yupo kitaa anakula zake bata tu but kiuhalisia kwa makosa ya rushwa alitakiwa nayeye awe nyuma ya nondo
 
Huyo Prof. naye TAKUKURU wamfungulie mashitaka kwa kushawishi kutoa rushwa(Corruption transaction) kama alikuwa hausika kwanini aogope kufikishwa mahakamani ili mahakama itoe maamuzi kama alibambikiwa kesi au la, hayo meno ya kwenda kumbambikizia yeye hao askari waliyatoa wapi kama si walipata taarifa kutoka wa raia wema kuwa kuna pembe za ndovu shambani kwa huyo mzee.

Jeshi la POLISI na TAKUKURU wachunguze account za huyo mzee na wapime biashara zake kama kwa haraka tu ametoa milioni mia inatia shaka.Kosa la hao askari ni kukubali kupokea rushwa baada ya kushawishiwa na mtuhumiwa.
Acha uporipori, mtu kafanya kazi za uhakika na zenye malupulupu kibao kwa zaidi ya miaka hamsini + biashara binafsi kuwa na milioni 100 kawaida.
 
Back
Top Bottom