Arusha: Ashikiliwa na Polisi kwa kumuua kaka yake kwa kumzuia kumwingilia shemeji yake kimwili

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha linamshikilia Melita Ndaletyan(34) kwa tuhuma za kumuua jwa kumchinja kaka yake Kiseri NdaIetyan ( 38),baada ya marehemu kumzuia mtuhumiwa aliyekuwa akitaka kumwingilia kimwili mke wa kaka yao mkubwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha leo, Justine Maseju, tukio hilo lilitokea Jana majira ya saa 6:30 usiku katika Kitongoji cha Naamalasin, Kata ya Noondoto wilayani Longido mkoa wa Arusha.

Alidai kuwa Kiseri alifariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mdogo wake ambapo wote wawili ni wafugaji na ni ndugu wanaoishi boma moja na kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alitaka kuzini na mke wa kaka yake ambaye hakuwepo nyumbani wakati huo.

Kamanda amesema kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni tamaa ya kimapenzi ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kutaka kumwingilia kimwili mke wa kaka yake na kuzuiwa na marehemu kufanya jambo hilo jambo lililosababisha ugomvi kati yao.

“Mtuhumiwa,marehemu pamoja na kaka yao mwingine wote walikuwa wanaishi kwenye boma moja hivyo mtuhumiwa wakati anataka kumwingilia kimwili mke wa kaka yake(mkubwa) ambaye hakuwepo nyumbani,marehemu alitokea na kumkataza kufanya hivyo ndipo mtuhumiwa alimchoma na kitu chenye ncha kali,”

“Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa kumfanyia ukatili ndugu yake na mara baada ya upelelezi kukamilika jalada litapelekwa Ofisi ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria,”

Kwa mujibu wa Kamanda ,mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa familia kwa ajili ya taratibu za maziko baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi

Wakati huo huo mwili wa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne ulikutwa umetelekezwa Julai 6 mwaka huu majira ya saa 6 mchana katika maeneo ya Burka, Kata ya Olasiti jijini Arusha.

Kamanda huyo amedai kuwa mtoto huyo ambaye jina lake pia linahifadhiwa ni mkazi wa eneo la Majengo.

“Taarifa za awali zilibaini kwamba mtoto huyo alifanyiwa ukatili wa kipigo pamoja na kuwekewa majani mdomoni na baba yake wa kufikia na Jeshi la Polisi liliendelea na upelelezi na kubaini kwamba, kuna mgogoro wa kifamilia kati ya mama wa mtoto huyo na baba wa kufikia (jina linahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi),”amesema

“Mara baada ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia na Jeshi la Polisi mkoani hapa tulifanya jitihada za kumtafuta kwa kushirikiana na raia wema na kufanikiwa kumkamata. Nitoe wito kwa wananchi kutoa taarifa dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa watoto kwa Jeshi la Polisi ili kukomesha au kumaliza kabisa tatizo la unyanyasaji kwa watoto,”

Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na baadhi ya mashuhuda waliomkuta mtoto huyo katika eneo hilo walidai kuwa aliwaeleza kuwa amefanyiwa ukatili wa kulawitiwa na baba yake wa kufikia na baadaye marehemu alipoteza Maisha na mwili huo kutelekezwa eneo la tukio.

“End.....
 
Really man?

Mbona wanawake wapo wengi sana tena wengine wakununua mpaka utake mke wa kaka yako?
Yaani mtu unatoa uhai wa mtu tena ni brother kisa ngono?

Huu ni ujinga usio'make any sense.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom