Arusha: Ally Bananga arudi CCM kwenye mkutano wa Rais Samia Suluhu

seedfarm

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
260
2,654
Mwanachama wa Chadema, Bananga arudi CCM

Alikuwa Diwani wa Kata ya Sombetini Katika Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA 2015 hadi 2020.

Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Ally Bananga leo Jumapili ametangaza kurejea tena CCM mbele ya Rais Samia Hassan “nawashukuruni vijana wenzangu wa CCM ambao niliwasubiri mje Chadema lakini hamkuja na leo nimerudi nyumbani.”

Nawaomba wana CCM wenzangu, mniruhusu niwe miongoni mwao ili tusaidiane na mama yetu katika kueleza mazuri yanayofanyika kuelezea mazuri yanayofanyika na mama nchi inatabasamu, inapumua- Ally Bananga, aliyekuwa Chadema sasa amerejea CCM

Pia, soma;
Ally Bananga: Nina kiapo na mke wangu, nitamlinda kwa gharama ya damu yangu

Bananga.jpg

Bananga 2.jpg

Rais Samia akimvisha Ally Bananga kofia ya CCM baada ya kurejea CCM
 
Aliyekuwa diwanu na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Ally Bananga amerejea CCM leo jijini Arusha.

Bananga ameomba msamaha kwa Rais Samia na wanaccm wote kwa mambo yote ya hovyo aliyowafanyia akiwa Chadema.

Source: ITV
 
PMU Ya Ccm Imeanza Upya Kununua Bora, Kafungua Njia Wanataka Wengine Watakwenda Haraka
 
Tatizo la Vyama ambavyo havina ideological Differences bali ni Platform ya Kujipatia Uongozi...

Ingekuwa ukienda Chama A kutoka B kuna Utofauti wa Ideology; Mtu kamwe asingetoka huku na kwenda kule no matter Uongozi wala kutokuelewana..., Kwa mtindo huu motivation ya watu ni Kura na Kula;
 
Back
Top Bottom