Arusha: Aliyekuwa Meya na Mkurugenzi wamwaga machozi makabidhiano ya Ofisi

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Madeni.PNG

Aliyekuwa mstaiki meya wa jiji la Arusha na diwani wa kat ya sokoni one kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bw Kalisti Lazaro amesema kuwa alikuwa anapita wakati mgumu sana hasa pale ambapo chama hicho kilipokuwa kinamtaka ahirishe vikao au kususa vikao vya mabaraza ya madiwani kwa ajili ya maslahi binafsi ya chama hicho alichoondoka.

Pia mbali na kulazimishwa kususa au kuhairisha vikao vya mabaraza ya halmashauri alikuwa analazimishwa kufanya mambo ambayo wakati mwingine yalikuwa yanauweka uzalendo wa taifa mahali pabaya sana.

Kalisti aliyasema hayo mapema leo mara baada ya kukabidhi ofisi na kuwaaga watumishi wa halmashauri ya jiji la arusha ikiwa ni siku chache baada ya kujivya nyadhifa zake zote ndani ya chadema na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM).

Alidai kuwa amekuwa akipitia wakati mgumu sana kwa kuwa alikuwa anatakiwa afanye mambo ambayo yalikuwa kinyume na uzalendo lakini kamwe hakurudi nyuma alitanguliza uzalendo huu.

"Nimekuwa kama Meya wa jiji hili kwa kipindi cha miaka kama minne hivi kipindi naingia hapa watu walifikiria sana namna ambavyo kutakuwa na fujo nyingi sana lakini kamwe sikukibali bali nilitanguliza uzalendo mbele japo nilikuwa nikipokea matamko mbalimbali" aliongeza.

Katika hatua nyingine alidai kuwa anatamani kuona kilichokuwa chama chake cha awali kikimtakia kila laheri kwa kuwa hatamani kuacha siasa kabisa na anatarajia ataacha siasa pindi atakapofariki dunia.

"Chadema wanatakiwa kuniombea kila laheri na pia nikishindwa hata siasa natarajia kufungua kanisa na nitaomba mje kama waumini kwani bado inawezekana kabisa hata siasa zikaendelea huko" aliongeza Kalisti.

Hata hivyo alimshukuru Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt Maulidi madeni kwa kuweza kumshawishi hadi kufikia hatua ya kujiunga na CCM na alishawishika baada ya kuona mazuri ambayo yanatanguliza uzalendo mbele.

Naye Mkurugenzi wa halmashauri wa jiji la Arusha Dkt Maulid Madeni alisema kuwa kwa mara ya kwanza ameanza kazi ya ukurugenzi akiwa na Meya huyo na amemfanikisha sana katika kuboresha kazi za jiji.

Dkt Madeni alidai kuwa akiwa kama mkurugenzi ambaye yupo karibu sana na meya huyo waliweza kufanikisha miradi mbalimbali ya jiji la Arusha na hata kufikia katika ngazi ya taifa.

"Kwenye elimu, afya, mazingira, Meya bora tumepata tuzo zote hizo ni kwa sababu huyu meya alifanya kazi kwa karibu sana na sisi na hakutupa vikwazo vya aina yoyote ile tunamshukuru sana na tutamkumbuka kwa hali na mali" aliongeza Dkt Madeni.

IMG_20191125_124744_5.jpeg
IMG_20191125_132821_1.jpeg
IMG_20191125_131910_3.jpeg
IMG_20191125_131222_8.jpeg
 
ALIYEKUWA Mstahiki Meya wa halmashauri ya Jiji la Arusha,Kalisti Lazaro, leo amekabidhi rasmi ofisi kwa mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Dakta Maulid Madeni,na kuwaaga rasmi watumishi wa halmashauri hiyo na kuwashukuru kwa ushirikiano wao katika kipindi chake cha miaka minne .


Akizungumza wakati wa kuwaaga watumishi kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo, Meya mstaafu Lazaro,amesema ameachia ngazi akiiacha halmashauri ikiwa na mafanikio makubwa ya maendeleo ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ,ongezeko la ukusanyaji wa mapato pamoja na jiji kufanya vizuri kielimu.

Amesema kuwa licha ya kuwa yeye ni meya aliyetokana na Chadema, aliweza kukataa maelekezo ya chama chake ya kuahirisha vikao vya baraza la madiwani kwa ajili ya kuendeleza vurugu kwenye jiji yeye alisimamia masilahi ya wananchi na halmashauri.

Meya mstaafu ,Kalisti, amesema ameiacha halmashauri ikiwa juu kwenye Nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo ukusanyaji mapato kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali ,pia ameiacha halmashauri ikiwepo kwenye utulivu wa kisiasa na amekuwa ni meya bora tangia mwaka 2016 hadi Novemba 19 mwaka huu alipoachia ngazi na ameweza kutunukiwa tuzo mbalimbali.

Ameyataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na ujenzi wa hospital ya wilaya inayojrengwa Engutoto, ujenzi wa shule za misingi za maghorofa, pamoja na wenyeviti wapya wa serikali za mitaa waliochaguliwa Novemba 24 mwaka huu kwa asilimia 100 ,

Ameongeza kwamba halmashauri ipo kwenye ubora wa elimu ambapo matokeo ya shule ya msingi mwaka huu imekuwa ni ya kwanza katika mkoa na ya tatu kitaifa .

Amewapongeza madiwani wote wa halmashauri ya jiji la Arusha kwa mshikamano wao na kukataa kugawanywa.

Awali mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji ,Dakta Maulid Madeni, amesema meya mstaafu alikuwa ni kiongozi mwenye uwezo na maono na mwelewa sana na amekomaa katika maswala ya siasa.

Amesema meya hakufanya kazi kwa majungu wala msimamo wa Chama chake bali alifanya kazi kwa masilahi ya halmashauri na wananchi wa jiji la Arusha.



Amesema wakati wa uongozi wa Meya mstaafu,mapato ya halmashauri hiyo yaliongezeka kwa kiwango kikubwa na kuifanya halmashauri hiyo kuongoza kitaifa katika ukusanyaji wa mapato.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi serikali za mitaa mkoa wa Arusha, Suleimani Kikingo, amesema kuwa walipokea kwa mshutuko na fedheha kubwa ya Meya kujiuzulu uongozi kwa sababu alikuwa ni kiongozi mahili na kusema kuwa watamkumbuka kwa utendaji wame.


IMG_20191125_130220.jpeg
IMG_20191125_132826.jpeg
IMG_20191125_125041.jpeg
IMG_20191125_111404.jpeg
IMG_20191125_111431.jpeg
 
Kifupi huyu meya Mimi Ni mmoja niliyekuwa namuunga mkono kwa kazi zake akiwa chadema.Mimi chadema Nina watu watatu tu ninaosifu kwa utendaji wao huyu meya wa Arusha Kalisti Lazaro,meya wa Moshi mjini na mbunge wa Momba.

Calisti Lazaro alikuwa na uwezo mkubwa Hadi wa kutafuta wafadhili wa nje kusaidia Manispaa ya Arusha .Kwa chadema meya mwingine ninayemkubali utendaji wake ni meya wa Moshi mjini.Yuko vizuri

Kwa wabunge Ni mbunge wa Momba tu.Wabunge wengine wa Chadema vichwani sifuri.Huyo mbunge wa Momba Ana akili sio utani chadema Haina mbunge mwenye akili nyingi Kama wa Momba
 
Eti uchaguzi wa wnyeviti wa mitaa nalo ni jambo alilolifanya kama meya, huyu nae kasifiwa kachanika msamba.
 
Wa CCM unawakubali wangapi?...hehehe!!!
Kifupi huyu meya Mimi Ni mmoja niliyekuwa namuunga mkono kwa kazi zake akiwa chadema.Mimi chadema Nina watu watatu tu ninaosifu kwa utendaji wao huyu meya wa Arusha Kalisti Lazaro,meya wa Moshi mjini na mbunge wa Momba.

Calisti Lazaro alikuwa na uwezo mkubwa Hadi wa kutafuta wafadhili wa nje kusaidia Manispaa ya Arusha .Kwa chadema meya mwingine ninayemkubali utendaji wake ni meya wa Moshi mjini.Yuko vizuri

Kwa wabunge Ni mbunge wa Momba tu.Wabunge wengine wa Chadema vichwani sifuri.Huyo mbunge wa Momba Ana akili sio utani chadema Haina mbunge mwenye akili nyingi Kama wa Momba
 
Huyu bwabwa amepewa kazi ya kumtoa Lema kwenye jimbo la Arusha mjini ...huwezi hao jamaa wana itikadi kali kama Mbeya
 
Kumbe kashawishika kujiunga na ccm..hapo kuna jambo lasiri..ila kwa kweli hawana chao.na hawapewi kazi..waliounga juhudi ni wengi na kzi ni chache sana
 
Chadema ni shetani anayetembea ,wanawezaje kumshurutisha mayor avuruge utendaji wake for political gain ,very cheap politics


State agent
 
Sasa huyo Mkurugenzi analia nini wakati atarejeshwa kwa mlango wa uani! Upinzani una safari ndefu sana.
 
Wanaume wawili wanaliliana.....kwa maamuzi ambayo wao wawili wameshauriana...walikua hawajui nn kitatokea??
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom