Arumeru: Wafanyakazi wa Hotel ya Ngurdoto waandamana kwa DC, wakidai Mishahara

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Wafanyakazi zaidi ya 50 wa hoteli ya Kitalii ya Ngurdoto iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha, wameandamana ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakimlalamkia mwajiri wao Joan Mrema kwa kushindwa kuwalipa mishahara yao ya miezi mitatu mfululizo.

Wakiongea mbele ya Mkuu huyo wa wilaya wamedai kuwa pamoja na kutolipwa mishahara yao ,wanadai makato ya mfuko wa kijamii wa NSSF yamekuwa hayapelekwi na kupatà usumbufu mkubwa wanapoacha ama kuachishwa kazi .

Madai mengine ni wafanyakazi wa kike wa hoteli hiyo pindi wanapokuwa kwenye likizo ya uzazi (Maternity Leave) mishahara yao husitishwa hadi atakaporejea kazini.

Baadhi ya wafanyakazi hao Yona Estomi,Stela Shayo na Dominy Kwayu wamedai kwamba kuanzia mwaka Jana mwezi wa 12 hawajalipwa mishahara yao na kusababisha hali ya maisha kuwa ngumu na baadhi yao kufukuzwa kwenye nyumba wanazopanga wanazoishi.

"Hivi sasa unapotuona hapa baadhi yetu tumefukuzwa kwenye nyumba tunazoishi na watoto wetu wamerudishwa shule tunadai mishahara ya miezi mitatu hatuelewi tutalipwa lini tunaomba serikali itusaidie tuweze kulipwa " Amesema Shayo.

Naye mfanyakazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Matata alisema kuwa,amefanya kazi kwa muda wa miaka 17 sasa kama kibarua na hajawahi kuajiriwa ,ambapo alipojaribu kudai fedha zake alifukuzwa kazi na haelewi cha kufanya,hivyo anaomba Mkuu wa wilaya hiyo aweze kuwasaidia ili wapate hali zao .

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro baada ya kuwasikiliza wafanyakazi alisema amepokea malalamiko ya wafanyakazi hao na kuahidi kutatua suala hilo ikiwemo kuwakutanisha na mwajiri wao ambaye aje kueleza kwanini hataki kulipa mishahara ya wafanyakazi.

"Nimewasikiliza vya kutosha kinachofuata ni kuwakutanisha na mwajiri wenu unajua huyu ni mwekezaji mzawa lazima tumlinde ili kuhakikisha analipa malipo yote ya serikali ikiwemo mishahara yenu"

"Mimi kama Mkuu wa wilaya yenu nimeyachukua malalamiko yenu na kuanza kuyashughulikia muwe wavumilivu ndani ya wiki moja tunamaliza suala lenu"Amesema Muro.

Kwa upande wake meneja wa hoteli hiyo baada ya kupigiwa simu na DC Murro,Beatrice Dallas aliomba apewe wiki moja aweze kushughulikia suala la malipo ya wafanyakazi kwa sababu hali ya kibiashara ni mbaya sana.

" Mheshimiwa tunaomba wiki moja utupatie tuweze kushughulikia malipo ya wafanyakazi maana hali ya kibiashara ni mbaya sana najua wanatudai ila lazima watupe muda"Amesema Beatrice.

Hata hivyo DC Muro amemtaka meneja huyo kufika ofisini kwake kesho Ijumaa Machi 6/2020 saa tano, asubuhi ili kujibu kwanini wameshindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wao.

Ends...

.
IMG-20200305-WA0021.jpeg
IMG-20200305-WA0022.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nishafanya kibarua hapo 2006-2007 kuna wafanyakazi waonevu sana na vyeti vyao uchwara. Walimfanyiaga fitina Chef flani akafukuzwa kwa kumuwekea mafuta ya taa kwenye maziwa wageni kutoka mtoni wakamaindi kichizi.
 
Tangu mzee Mrema afariki na awamu ya tano kuingia wafanyakazi wa hizi hoteli huko Arusha wanapitia vipindi vigumu sana. Ni maisha magumu sana kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Biashara nzuri iende na nguvu ya soko, of course ni biashara nzuri lakini pia kulikuwa na nguvu ya serikali kupeleka vikao na shughuli kibao za serikali (kwa aina hii ya biashara wengi ndio wanaolia awamu hii na wale walioanzisha kampuni leo na baada ya miezi mitatu wanapewa tenda nono za serikali)
 
hotel ambyo kunakakijito kanaktiza chini ya ukuta w uzio wa hotel hiyo. ukuta ambo ulikua umetengeneza kona kali ya barabara inayo enda arusha national p. enzi za kikweteenzi za unajua mi ni nani?
 
Sio hizo tu Impala na Naura Spring nazo zinapumulia mashine tu hali imekuwa tete sana Tangu Mrema afariki na pia Tangu hii awamu ishike hatamu basi vikao vya kiserikali ambavyo sio sensitive haviendi tena kwenye hizo hotel za kifahari
 
Back
Top Bottom