MWITONGO MAARIFA
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 276
- 1,428
Mhe. Rais yupo ARUMERU kuzindua mradi wa maji ambapo Mbunge wa Arumeru hayupo katika uzinduzi huo. Wabunge wa ccm waliopo wanadai Mbunge huyo amelikimbia Jimbo na hivyo wananchi hawana wa wakuwasemea lakini kila wanapozungumza wanaonyesha kabisa hata jeographia ya wilaya hiyo hawaijui na hawakuwa tayari kujifunza kabla ya Rais kufika.
Mhe. Milya wa simanjiro badala ya kutoa hoja amekariri mstari mmoja wa biblia ndo anauzungumzia lakini pia anampongeza Rais ka kumteua DC wa Hai Bw.Sabaya akidai kuwa ni uthibitisho kuwa Rais siyo mbaguzi. Kwa tafsiri nyepesi huyu mbunge ubaguzi kwake ni kuteuliwa kuwa DC lakini anashindwa kujua huyo ni mwanaccm na anayohaki yakuteuliwa hata angekuwa mbondei
Hakuna anayezungumzia ugumu wa maisha, hakuna anayezungumzia madhara ya kushuka kwa utalii, hakuna anayewazungumzia wafanyabishara wanaonyanyaswa kwa Kodi lukuki, hakuna anayeomba kibali Cha kuuza mazao ndani na nje ya nchi kulingana na soko badala yake wamebaki kusifia bila kujiuliza chanzo cha fedha za hiyo miradi ni Nini?
CCM jaribuni kutafuta wajenga hoja achaneni na Mambo ya kusifia kila Jambo hata Kama Ni baya maana mnawafanya viongozi waamini Hali ni shwari kumbe si swari