Arumeru Mashariki: Wanachama na viongozi UVCCM kuhamia CHADEMA

Mkuu Freedom Fighter, jina lako zuri atadhani ni la mpiganaji!, kumbe na wewe ni wale wale wapigania tumbo?!. Kwa vile EL akakata fungu, njaa yako inakutuma kila anayemtaja EL katumwa!. Eti kuna nafasi nimeahidiwa!, laiti ungelijua shughuli zangu ni nini kwa sasa, na kazi ngapi na za malipo gani nimezikataa, usingezungumzia hayo!. Njaa... njaa... njaa zitawaponza!.

Mkuu Pasco, ID yangu ni Fredomfighter, pili juu ya shughuli zako hilo siyo ishu, ishu hapa ni nini unakifanya hapa jamvini kuhusu EL. Kwa unavyosomeka hapa ni kuwa kama kuna kazi za malipo umezikataa sawa lakini kazi ya kumpamba EL hapa jamvini hujaikataa.
 
Mkuu Pasco unatia aibu yaani unaandika kitu halafu baadae unakuja kukanusha?
Feedback kaku quote vizuri lakini bado unajibalaguza, acha zako mkuu, watu kama nyie ni zaidi ya fisi....
Labda alikuwa hajaona alichoandika...tumsamehe bure.
 
Unachosema nini na ulichokuwa unapinga nini kwa Feedback,yeye alimwambia Pasco asitumie njaa ikawa sababu ya kuhama chama na wewe unarudia yale yale ya Feedback, au kwa vile kilisemwa na Feedback anayekupaga ukweli wako?

Soma post yangu vizuri na utulie kabla ya kutoa majibu hasa mstari wa kwanza.Sijui unashangaa nini.......!Halafu tafsiri ya ukweli unaijua wewe kulingana na ukomo wa fikra zako,si mbaya.Hata mpika majungu unaweza kumwona analyst,rumour mongering chap you can treat him/her as an expert.

We have lost our sense of outrage that is necessary to make our lootocrats stop stealing from us.

This is the kind of statement these crooks in power want to read to confirm to themselves and their cabal that the common man has a short memory and has not woken up from his deep slumber coma.

Wanakaribishwa sana, Hata hivyo, napendekeza huko mbleleni kuwa tunahitaji mafunzo hata ya siku moja ya kuwabadili kimawazo makada wanaotoka ccm. Wengi wanadhani kuwa siasa za chadema na ccm ni zile zile. Kumbe siyo.

Ni kweli kamanda.lakini swali,je tuwafundishe itikadi wakishakuwa wanachama kamili au tuwe na programme within a specific time baada ya mwanachama kujiunga apigwe brush ya ideology?Wasiwasi wangu ni kwamba wanaweza wakageuka tatizo hata kabla hawajapewa elimu juu ya itikadi yetu.Kama uliona mchango kwenye thread moja nilisema tuna changamoto sasa ya kugeuza fan base yetu kuwa loyal base.Fan base iliyo na affinity towards our party ni kubwa,ikigeuzwa kuwa loyal base tu CCM wamekwisha.
 
Unachosema nini na ulichokuwa unapinga nini kwa Feedback,yeye alimwambia Pasco asitumie njaa ikawa sababu ya kuhama chama na wewe unarudia yale yale ya Feedback, au kwa vile kilisemwa na Feedback anayekupaga ukweli wako?
Easyfit relax...take it easy...ukiona hivyo jua dawa imempata mgonjwa au wazungu wanasema message sent wewe ni kuendelea na shughuli zako tu.
 
Siku zote nasema,usiame chama kwasababu ya kushindwa kupata nafasi fulani au cheo fulani..na kwa kweli CDM tuwe makini sana na watu wa namna hii...mara nyingi uwa inakuwa ni hasira au maslahi binafsi lakini bado wanakuwa na mapenzi na vyama vyao...mfano tunao,huyu mzee wa ujira wa mwiha aka Shibuda bado anadamu ya CCM na aliondoka kwasababu ya hasira za kushindwa kwenye kura za maoni..Mimi nadhani ifike wakati watu tuwe tunaondoka kwenye chama kwasababu ya uovu au kushindwa kufikia malengo ya kuwasaidia watanzania,lakini ukiama chama kwasababu ukuchaguliwa sidhani kama ni sababu yenye afya..si mujarabu kabisa.
 
Ni kweli wanaohama wawe na sababu, lakini hata hawa wameondoka kwa sababu ya rushwa au hayo siyo maovu.
 
Mashibuda hao, ina maana leo ndio wanaujuwa ubaya wa CCM? hawa ni malaya wa kisiasa.
Umewahi kuwa mlokole! ukitaka kuwa mlokole lazima upitishwe kwenye sala ya toba kwanza. Ndipo walipo sasa. kwani hata wewe (sijui umri wako) lakin nina uhakika kama hukuwa mwanaccm ukaondoka basi kuna sababu nyingine ya kuipenda CDM ambayo umeikosa CCM. Hivyo hata wao kama ni wakweli hiyo ndio sababu yao kuu kuikataa CCM. lakini sala ya TOBA muhimu na waikane CCM hadharani kwanza ndio tuwakaribishe
 
Sidhani kama ulikuwa unakemea njaa ila ulikuwa unawatahadhalisha wasiende Chadema kuna njaa kali wabaki CCM, quote 'Chadema, kule watajifia njaa bure na kutamani kurudi walikotoka', maana yake nini, ni kuwa unawashauri wabaki CCM hata kama hawakubaliani nayo kwa vile kuna neema, i think the message is clear.
Mkuu Feedback kwa kusaidia tuu, katika thread yangu ya siku za nyuma niwahi kusema kuna wengi ambao wanajiunga CCM au kuishabikia kimaslahi tuu na sio kufuata sera wala ideology!. Mzee Mwanakijiji aliwahi kuuliza "wapiganaji walioko CCM, wanapigania nini?" mimi nilimjibu "wanapigania nafsi zao na matumbo yao" nikimaanisha walishajua CCM imehodhiwa na mafisadi, kichowafanya waing'ang'anie kubaki CCM ni nini kama sio njaa zao?!.

Kwa sasa CCM inatumia ushawishi wa fedha kwenye kila kitu na kati ya waendekeza njaa wakuu ni UVCCM!.

Mimi eneo ninaloishi niliwahi kusaidia vijana fulani kutega magoli ya biashara ndogo ndogo pembeni ya barabara nikaonekana kama mfadhili fulani, kwenye moja ya mikutano yao ya ndani UVCCM wakapendekeza jina langu nipewe ukamanda vijana eneo langu ili nikiamua kugombea ubunge kupitia CCM, hao vijana ndio wanibebe kamanda wao!.

Nilipowaambia mimi sio mwana CCM hawakuamini!? Eti mbona jina langu limependekezwa na wakuu fulani kwenye vikao vyao?!. Wakanishauri niwapatie kiasi fulani ili wanisimamie tangu ukamanda hadi ubunge!. Niliwaambia sorry bado sijafikiria kujihusisha na siasa na hata nikiamua sio lazima CCM!. Hivyo najua fika harakati nyingi za uongozi CCM its about money!.

Zamani watu waliipenda CCM kwa mapenzi tuu, siku hizi hapendwi mtu ni pesa tuu na CCM inazimwaga kwa kwenda mbele!.

Kwenye mikutano ili kuhudhuria kwanza ni T-shert na kofia, usafiri kwa fuso na kupigwa dala!. Kila mmoja. Wenye boda boda na bajaj wao wanapigwa ten!. Wenye taxi wanapigwa twenty twenty!. Its all about money!.

Nilichosema hawa vijana wa CCM wameshazoea fungu na wengi wao wameingia CCM kufuatia njaa zao sasa ndio wanataka kujiunga Chadema kule hakuna migao!. Watu wanahudhuria mikutano ya Chadema bila kupewa chochote!. Watu wanajiunga Chadema kwa mapenzi yao bila kutegemea chochote japo siku hizi Chadema nao sii haba, wako fit na chochote kitu wanacho japo sijui kama nao wanakata!.
 
Soma post yangu vizuri na utulie kabla ya kutoa majibu hasa mstari wa kwanza.Sijui unashangaa nini.......!Halafu tafsiri ya ukweli unaijua wewe kulingana na ukomo wa fikra zako,si mbaya.Hata mpika majungu unaweza kumwona analyst,rumour mongering chap you can treat him/her as an expert.

We have lost our sense of outrage that is necessary to make our lootocrats stop stealing from us.

This is the kind of statement these crooks in power want to read to confirm to themselves and their cabal that the common man has a short memory and has not woken up from his deep slumber coma.
Ben tabia yako ya kudharau wengine ndiyo inayokuponza, huwa unajiona una busara sana kuwazidi wengine. Mbona hata personal secretary wangu ana PA? Uongozi hautafutwi kwenye JF, nakushangaa unatafuta kura humu badala ya kuja huku AM field kwa wapiga kura. Unataka cheo Bavicha tuonyeshe umefungua matawi mangapi umekifanyia nini chama hadi kikuamini. Wanaokusifia humu wanakupoteza bure kafungue matawi ya chama tukusikie kama wenzako kina Mnyika sio kushinda JF ukitafuta sympathy ya JF members.
 
hapo kwenye nyekundu umemshauri vizuri sana huyu Ben, sijawahi sikia kafanya harakati zozote hata za kufungua matawi ya Chadema sehemu yoyote, Ben kubali ushauri wa Quinine
 
Naomba nikusaidie, kama uko karibu na internet cafe nenda na fungua google halafu tafuta gazeti la mwananchi utaiona hiyo habari!

Sio nipo karibu na Internet na iphone, na Laptop zote zina accsess ya Internet pia nalo gazeti la Mwananchi la leo hiyo habari hakuna.
 
Tuwe makini na watu wa aina hii,tukumbuke hawaji cdm kwa sababu wanaipenda bali wanaenda cdm ili kukomoa wenzao,they are not good ppo,tuwakaribishe ila tuwe makini nao sana
Wakija tutawapa kazi ya kufagia ofisi na kupika chai,kwani sasa ndio wanauona ubaya wa Magamba,mamluki wakijasalimisha wanakuwa wajakazi,ndio maana watapewa kazi ya kufagia ofisi na kupika chai
 
Ben tabia yako ya kudharau wengine ndiyo inayokuponza, huwa unajiona una busara sana kuwazidi wengine. Mbona hata personal secretary wangu ana PA? Uongozi hautafutwi kwenye JF, nakushangaa unatafuta kura humu badala ya kuja huku AM field kwa wapiga kura. Unataka cheo Bavicha tuonyeshe umefungua matawi mangapi umekifanyia nini chama hadi kikuamini. Wanaokusifia humu wanakupoteza bure kafungue matawi ya chama tukusikie kama wenzako kina Mnyika sio kushinda JF ukitafuta sympathy ya JF members.

Quinine/Feedback,

Ha hahahahhahh!...Roho inakuuma eeh,Asante sana kwa ushauri though.kumbe wewe ulipokuwa unajibu post ulikuwa unajifanya unabusara kuliko wengine siyo? Nikiwa nashinda JF wewe ulikuwa wapi ama uliniona je? Kufungua matawi ndiyo kazi pekee kwa chama cha upinzani kama chadema?Je,kila ukifanya kazi ya chama ni lazima utangaze?Je,kila anayeandika JF ni mtu anayetaka uongozi wa BAVICHA? .........Hypocritical vagabond !

hapo kwenye nyekundu umemshauri vizuri sana huyu Ben, sijawahi sikia kafanya harakati zozote hata za kufungua matawi ya Chadema sehemu yoyote, Ben kubali ushauri wa Quinine

Mkuu,kufungua matawi ndiyokazi pekee ya chama cha siasa au mwanasiasa?Kufanya kazi za chama ni lazima wewe usikie?Mkuu,nipo mikoani nafanya kazi na nafanya kazi kubwa ya kukijenga chama changu,katibu mkuu anajua hilo.Wanaokalia majungu na kupotosha watu hapa uwe nao makini tu. Hata hivyo asante kwa ushauri wako,nitazingatia ushauri wa Quinine/Feedback.

Wewe mbona ulikuwa NCCR Mageuzi uliondoka kwa nini?

Ritz.....Ha hahahah,rudi kwenye mada bwana usituharibie moods.Kwani ni lazima kila mtu abakie kwenye chama cha siasa wakati hakuna maslahi kwake?kuhama ni muhimu hata kama chama unachohama na unachohamia haviendani kiitikadi ati.sana sana cha muhimu ujikite kwenye itikadi majungu,fitna,kujipendekeza(kama unavyona hapa JF) na siasa za u-simba na u-yanga tu.Ukiweza hayo unaweza kuwa mwanasiasa .ha ha haa!
 
Quinine/Feedback,

Je,kila ukifanya kazi ya chama ni lazima utangaze?Je,kila anayeandika JF ni mtu anayetaka uongozi wa BAVICHA? Mkuu,kufungua matawi ndiyokazi pekee ya chama cha siasa au mwanasiasa? Kufanya kazi za chama ni lazima wewe usikie? Mkuu,nipo mikoani nafanya kazi na nafanya kazi kubwa ya kukijenga chama changu, katibu mkuu anajua hilo. Wanaokalia majungu na kupotosha watu hapa uwe nao makini tu. Hata hivyo asante kwa ushauri wako,nitazingatia ushauri wa Quinine/Feedback.
Siasa si kazi ya siri hadi ujifiche, umekuwa unyago? eti hata Katibu mkuu anajua nafanya nini , ni huyu huyu Slaa aliyekuambia unataka kupindua katiba kwa kuanzisha alliance ndani ya chama? Hatutaki Malema type ndani ya Chadema. Fanyeni kazi vijana acheni majungu, majungu hayatawafikisha popote mtakuwa mnaishia reception tu pale mtaa wa Kongo, mara 19mil mara Mnyika kalundikiwa vyeo kama vijana wenyewe ndio nyie yes acha alundikiwe hata vyeo 20.
 
Duh! bado tu mnaendelea kutukanana? Sii mpange tu mkutane Leaders mzichape weee kisha mwanamme asimame na kujitapa maana haya matusi ya JF wala hayana mvuto. Jamani nyie vijana mnajisifu kwa kufungua sijui matawi na kadhalika mnayafanya haya kwa mapenzi ya chama ama kujionyesha!..Sisi wengine wanachama tu, tunapoona viongozi wenyewe ndio hawa basi inatupa shida sana kuamini kwamba tutafika!
 
Back
Top Bottom