Arumeru Mashariki hapatoshi ; Kigogo CCM adaiwa kudakwa na rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arumeru Mashariki hapatoshi ; Kigogo CCM adaiwa kudakwa na rushwa

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by nngu007, Mar 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  30 MARCH 2012


  • LALA SALAMA YATAWALIWA NA VITUKO VINGI
  • Kigogo CCM adaiwa kudakwa na rushwa
  • Mbowe arushiwa kombora na lusinde

  Chama cha mapinduzi (CCM) kimedai viongozi wa chadema wamekuwa wakiwapa wafuasi wake pombe kali aina ya viroba kwa lenga la kuharibu mikutano yao.inayofanyika katika maeneo mbalimbali.

  Pamoja na hilo, pia kimemtupia kombora mwenyekiti wa Chadema,Bw. Freeman Mbowe, kwa kujifanya mpambanaji wakati anaishi kwa kutegemea mali za urithi za wazazi
  na babu zake. Madai hayo yalitolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtera, Bw. Livingstone
  Lusinde, wakati akihutubia mkutano ya kampeni katika kijiji cha Njeku wilayani Arumeru jana wakati akimnadi mgombea wa CCMBw.Sioi Sumari.

  Alisisitiza kuwa Chadema inawanunulia vijana viroba vya pombe kwa lengo la kufanya fujo na vurugu kwenye mikutano ya chama hicho, kitendo ambacho ni kinyume na sheria za uchaguzi. Alidai kuwa wafuasi haowakiongozwa na mbunge wa Jimbola Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema wamekuwa wakipita kwenye mikutano ya kampeni ya CCM na kuzomea mikutano yao huku wakifanya fujo, jambo ambalo si
  la kistaarabu hata kidogo. "Nawashangaa Chadema kwa kuwapa wafuasi wao pombe kali ili waje kufanya fujo katika mikutanoyetu lengo lao wanataka kuharibu
  uchaguzi mzima," alisema Bw.Lusinde.

  Alimgeukia Bw. Mbowe akidai amekuwa akijiita yeye ni mpambanaji mbele ya vijana wa Chadema wilayani Arumeru na huku anaishi kwa kutegemea maliza urithi wa wazazi wake.

  Bw.,Lusinde alikanusha vikali kuwa amefukuzwa kwa kufanya kampeni kwa kutumia maneno makali anayoyazungumza katika majukwaa ya kampeni.Kwa upande wake mgombea
  ubunge kwa tiketi ya chama hicho,Bw. Sioi Sumari, aliwaahidi wakazi wa Njeku kuwa endapo watamchagua atahakikisha anatatua
  kero zinazowakabili katika kijiji.

  Wakati huo huo, Bw. Mbowe amesema mafisadi wa CCM katika uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki watapigwa mateke ya kura mchana saa sita. Kauli hiyo imetolewa na Bw. Mbowe wakati akihutubia mkutano.

  wa kampeni katika Kijiji cha Ngongongare. Alisema mafisadi wa CCM waliopo Arumeru Mashariki wataumbuka kwani Chadema imejidhatiti katika kura. Aliongeza kuwa mafisadi hao wanashinda kwa kuiba kura na kutumia mabavu hali ambayo
  inaonesha wazi kuwa wanaiba demokrasia ya Watanzania.

  "Hapa Arumeru MasharikiMafisadi wataambulia patupu kwakuwa kila kijana na mpiga kura atalinda kura yake na baadaye tutahakikisha tunamkesha sasa hawa mafisadi ambao wanasubiri kila mara tukalale na kisha wanaiba kura zetu wataanzaje nawaonea huruma," alisema Bw. Mbowe.

  Naye mgombea ubunge kupitiachama hicho, Bw Joshua Nassari aliwataka wananchi wa jimbo hilo la Arumeru Mashariki kuachana na Propaganda ambazo zinaendelea kuenezwa kuhusu maisha yake.

  Wakati huo huo, habari ambazo gazeti hili limezipata wakati likienda mitamboni, zilieleza kuwa kigogo mmoja wa CCM alikamatwa akidaiwa kugawa rushwa. Taarifa
  hizo zilieleza kuwa tukio hilo lilivuta hisia za wingi, na kuamua kufuatilia suala hilo kwa kina. Wakati huo wafuasi wawili wa Chadema katika Jimbo la Arumeru Mashariki wametekwa nyara na watu wasiojulikana, huku mmoja kuibiwa gari na mwigine akiwa ajulikani alipo kwa siku ya nne sasa Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo Kamanda wa Polis Mkoa wa Arusha, Bw. Thobias Andengenye, alisema mtu wa kwanza ambaye amemtaja kuwa ni Bw. Ally Juma (32) mkazi wa Tengeru alitekwa na watu wasiojulikana na kisha kuumizwa vibaya. Bw. Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa mbiliza usiku, ambapo watu wanne walimchukua Bw. Ally na kisha kumuomba wampeleke katika eneo la Makumira ambapo alikubali kutokana na makubaliano ambayo walifikia.

  Alifafanua kuwa mara baada ya makubaliano hayo aliwapeleka,lakini ghafla watu hao walimtaka awashushe ili mmoja ateremke kabla hajafika Makumira."Dereva huyo alipokuwa akisimamisha gari ili mtu huyo ashuke ghafla alikabwa na kupigwa
  na kitu kizito katika paji la uso," alisema Bw. Andengenye.Alisema watu hao walitowekana gari. Alisema mara baada ya wasamaria wema kutokea walimpa
  kijana huyo msaada na kisha kumpeleka katika hospitali ya wilaya ambapo hadi sasa anaendelea na matibabu. Watu hao waliondoka na gari aina ya T 563 BTM rangi ya Peal Wanted ndogo. Mtu huyo aliyeporwa gari inadaiwa kuwa mfuasi wa Chadema.

  Katika hatua nyingine mfuasi mmoja wa Chadema aliyefahamikakama Bw. Omary Abdul, mkazi wa Sakina jijini Arusha naye amepotea katika mazingira ya kutatanisha
  ambapo hadi sasa hajulikani alipo.Kwa mujibu wa rafiki wa karibu na Bw Omary, ambaye ni Bw Christ Mbajo, alisema kuwa rafiki yakehapo awali alikuwa na ugomvi na kiongozi wa CCM (jina tunalo) kwa kuvaa vazi linalofanana na yale ya
  Chadema. Bw Mbajo alisema kuwa rafiki yake huyo alitoka katika mkutano
  wa kampeni katika eneo la Ngarasero ambapo alielekea katika
  viwanja vya Triple A jijini Arusha ambapo mara baada ya kufika ndipo
  alikutana na kada huyo wa CCM aliyemtaka avue mavazi hayo.
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ungeiedit hiyo habari kabla ya kuileta hapa...
  Ukicopy inabidi pia ufahamu kupaste!
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  kanawe uso kwa maji ya baridiiiiiii kisha rudia kuisoma utaelewa, wenzio tushaielewa.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  lol...
   
 5. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kalipwe na bwana yako kwa kukrash kila kitu hata kama ni ukweli , Lowasa mmeo anakulipa ngapi kwa kila post?
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Watanzania Wengine Mnaanza ku-act kama Wakenya Nimeisoma nimeiielewa hii Topic nimeipenda nimeona neshare na Wana Jamii Forum but when pesting to the Jamii Forum It did not come the way I wanted and I'm ferfectionist...

  So damn few Members are a little clever to say better things; kweli tutafika?
   
 7. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hakuna tatizo la kukopi,kuedit wala kupaste katika habari hii,ni magamba wachache sana wanaosoma na kuelewa post kama hizi.msalie lowassa
   
 8. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Ngoja niingie kunakohusika nitafute FILE la Bwana Livingstone Lusinde! Halafu nitarejea.
   
 9. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  HAkuna tofauti kati ya Lusinde na halufu ya Kwapani ya Mbeba saruji
   
 10. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ccm = chama cha mauaji.
   
 11. nexus white

  nexus white JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  lakini ujumbe umeeleweka
   
Loading...