Arumeru kunazidi kupamba moto!

Uuuuuii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
Ni ubunge tu???! Ila watu wa Leguruki,Nkoaranga,Kitakiti,Kingori,Maruvango,Nkoansiyo,Mirini,Mbuguni,Maji ya Chai,Tengeru,Usariva,Kibaoni ect watamchangua.
Ni dunia huru,nchi huru,mawazo huru.Kila mtu ana haki ya kufanya chochote including kugombea hata kama baba yake alishakuwa kiongozi.
Honngera mwanamke shujaa kwa kutoa ofa,mimi si kama wengine,bado tunasalimiwa kwa kuanza na Mangi?!!!!
 
Hivi ina maana mbunge anapata malipo mazuri kuliko mkurugenzi wa shirika la umma tena la kimataifa
Hebu jiulize sasa kweli maslahi ya mbunge yanazidi mkurugenzi wa AICC ???? No nadhani kuna kitu cha ziada labda kulenga uwaziri au tamaa tuu ya kujulikana!!!!

 
Baada ya kufanya utafiti wa kina na kuangalia wagombea wanajitokeza kugombea kuteuliwa na vyama vyao kupeperusha bendera ktk katika jimbo la Arumeru Mashariki,naungana kabisa na wapiga kura wengi kuwa hakuna anayeweza kumshinda Sioi endapo atapitishwa na CCM na yeye mwenyewe kujipanga vizuri.
Huu ndio ukweli na CCM inatakiwa iangalie hilo kama wanataka kuwepo ktk jimbo hili.Wengine kwa sababu zao wanasema hana uzoefu ila wengi watakubaliana nasi kuwa uzoefu wa kuongea kwenye majukwa na kutia ahadi hew sii muhimu zaidi ya moyo wa ujasiri wa kukabiliana na changamoto za watu wa Meru.Kule Meru huwa tunaamini Maji yaliko pita mwanzo lazima tu yapite tena.
Nawashauri akina Kaaya's,Urio na Shami kujitoa mara moja na Kuumunga mkono Jemedari Sio Sumari awe mgombea pekee.
Sioi ni mtu wa kawaida sana,anaweza kuongea lugha ya kawaida kabisa hata na mtu ambaye si sawa na yeye.Na huyu ndie mtu anayetakiwa.Yeye si kama wengine wanatumia mifano ya kuwakejeli wananchi wa Arumeru Mashariki.Wananchi hawataki dharau,wanataka maendeleo.
Uko Arumeru nini Mkuu, basi imekula kwako, chomoka maghamba's!!!!!

 
...Kule Meru huwa tunaamini Maji yaliko pita mwanzo lazima tu yapite tena.
...
Aisee! Unasema 'kule' Meru, ina maana haupo huko ingawa unatupa news kuwa umefanya utafiti! Nilitegemea kwa mtu anayefanya utafiti atakuwa site, so nilidhani utasema "Hapa Meru ..." na sio "Kule Meru ...". Halafu hayo matokeo ya utafiti mbona umeyatoa mapema sana wakati zoezi la kuchukua fomu bado halijaisha, ina maana akitokea mtu mwingine kuchukua fomu utaanza upya kutafiti?
 
MBIO za Uchaguzi Mdogo wa Arumeru Mashariki, zimeendelea kushika kasi baada ya makada zaidi wa CCM akiwamo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa Arusha, Elishilia Kaaya, kuchukua fomu kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania nafasi hiyo.

Licha ya Kaaya ambaye ni mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kada mwingine wa CCM waliochukua fomu hizo jana ni Rais wa Mtandao wa Maendeleo ya Vijana nchini (YDN), Elipokea Urio na Elirehema Kaaya, ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza.

Wagombea hao walikabidhiwa fomu na Katibu wa CCM Wilaya ya Arumeru, Edson Lihweuli.
Wakati CCM wakijitokeza kuchukua fomu hizo, pia wanachama wa Chadema amabo ni Joshua Nassari, Samwel Shami, Francis Tembo na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Arumeru (Bawacha), Anna Mwagirwa, wanafanya idadi ya watu saba kujitokeza kuwania kiti hicho.

Akitangaza uamuzi huo jana, Urio alisema anataraji kuchukua fomu Jumamosi wiki hii kwa lengo la kuomba ridhaa ya chama chake kuipeperusha bendera katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika siku chache zijazo.
Wakati vyama CCM na Chadema vikiendelea kupiga mbizi, Chama cha NCCR- Mageuzi hakijafanya uamuzi iwapo kishiriki au la.

Katibu mkuu wa chama hicho, Samwel Ruhuza, alisema wametuma ujumbe maalumu kwenda jimboni humo kufanya utafiti wa awali kujua kama kinaweza kumsimamisha mgombea.
“Sisi tumetuma task force (kikosi kazi) Siku zote tungependa ushirikiano na wenzetu, lakini yote hayo katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki yanategemea ripoti itakayoletwa na timu ya wataalamu wetu walioko katika jimbo hilo kwa sasa,” alisema Ruhuza.

Alisema kazi inayofanywa na tume hiyo maalamu ya NCCR-Mageuzi, ni kufanya utafiti kujua kiwango cha kukubalika kwa chama hicho na kuona mtandao wa vyama vingine kikiwamo CCM na nafasi ya ushindi kwa upinzani.
“Tunaangalia vitu vingi katika hili,mtandao wa chama chetu, vyote vya siasa kiwango cha kukubalika kwa wagombea wao na wetu na nafasi ya ushindi kwa upinzani, hatua hiyo ndiyo itakayotufanya tuamue kusimamisha mgombea au kuunga mkono chama cha upinzani,”alisema Ruhuza.

Kuhusu ushirikiano na Chadema, Ruhuza alifafanua kuwa utategemea ripoti hiyo inayotarajia kukamilika wakati wowote na kutolewa kwa umma.

“Kwa sasa ni mapema mno kutangaza kuunga mkono chama chochote katika uchaguzi huo au kutangaza kusimamisha mgombea, tunaweza kufanya hivyo kumbe mgombea kupitia chama chetu anakubalika zaidi ama tunaweza kusimamisha kumbe wa wenzetu ni mzuri,”alisema Ruhuza.

Huo moto uko wapi sasa kutaka kuwaingiza watu dili ya mtu wako Sioi au Naoa, bila shaka maghamba's watakulipa vizuri!!!!!

 
EL at work!!! Lazima watu waliokwenye payroll yake wampigie debe Sioi kwakuwa ni Mkwewe!!
 
Back
Top Bottom