Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Utawala wa Mwendo kasi unaendana na Ukiukaji wa Katiba
Nimeona clip inayosambaa mtandaoni ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akielekeza polisi kumkamata mwananchi huku akidai “Kama mmeshindwa kuishi kwenye hii nchi katafuteni nchi nyingine.”
Huu siyo uongozi bali ni udikteta uliopitiliza. Ukiona viongozi wananchi kutamka nchi yangu, serikali yangu, mtanyooka, katafuteni nchi nyingine ya kuishi nk tambua hana maono wala malengo anayopanga kufikia.
Suala analozungumzia la upimaji wa ardhi si suala la kulazimisha ni suala la kisheria na linapaswa kuendeshwa kwa majadiliano na ukilazimisha utawanya watu wanyamaze kwa sababu ya nafisi yako na matumizi ya vyombo vya dola ila ukiondoka au dola ikiondkka mgogoro utakaozaliwa hautasuluishika kirais.
Nakumbuka Mhe. Lukuvi alipita huko Arusha akazungumza na wananchi maeneo mbalimbali na hakukuwepo na ukinzani anaopata Muro, hivyo inaleta tafsiri kuwa yeye anatafuta sifa kwenye kamera bila kuwa na maono.
Usipobadilika utajikuta unawagawa wananchi Kama kiongozi badala ya kuwaunganisha...