Arumeru hali si shwari mabomu ya machozi yatumika kusambaratisha watu.

Habari ninazo zipata sasa hivi ni kwamba wawekezaji wameanza kutoa malalamiko kwenda balozi zao jijini Dr es salaam ili walalamikie serikali kutokana na kukiuka mikataba ya uwekezaji.
 
Haya huo ni mwanzo tu, Mh. Pinda naye ajiandae huko kwake iko siku kitanuka, wakati Mh. mdee anamkumbusha bungeni mwaka jana, Pinda alisema watu wasiwaonee wivu na wao huu ndiyo wakati wao kuwekeza kwa kuuza aerdhi sasa kiashiria ni arumeru, huko tuendako kuhusu sual la ardhi lazima vita ipiganwe.
 
kwa Wadau tu, hivi inakuwaje Mzungu toka ulaya, america au kwingineko apewe ardhi ktk maeneo ambayo tayari wazawa wana tatizo la ardhi. Hivi tuko tayari kuua raia wetu kwa ajili ya wakoloni kweli jamani. tufike mahali tuone aibu na kuwapendelea WATZ
wanasema wananchi watapata ajila na miundo mbinu ya maji, hospital na shule zitaletwa na mzungu si ndoo maana jamaa yupo hewani mda woote, halafu bora angekuwa anaenda uarabuni tujue moja lakini kwa hao anaokwenda maadili yamekwisha bwana wanakubali wanaume kuoana! SASA HUWA SIMUELEWI SANA HAPA!
 
Ni majinga haya majamaa yapo kama makondoo atakapo pita mmoja yoooteee yanafuta hata kama yanafanya kosa

we ndo mpumbavu unaeringia hela chafu za kifisadi huku watz wenzako wakifa kwa mateso ya serikari ya ccm,. Huo ndo mwisho wa ccm make hzo posho unazo pewa zinamwisho wake
 
Kwani hiyo ardhi ilikuwa ya nani kabla ya Dolly kuuziwa?
hahahah....huhitaji elimu ya juu kupata jibu...swala hapa ni kwamba wanachi hawana aridhi huku wawekezaji wana mashamba makubwa na mengi hawaya tumii huku wananchi wakibaki vibarua....Kumbuka issue ya zimbambwe...
 
wanasema wananchi watapata ajila na miundo mbinu ya maji, hospital na shule zitaletwa na mzungu si ndoo maana jamaa yupo hewani mda woote, halafu bora angekuwa anaenda uarabuni tujue moja lakini kwa hao anaokwenda maadili yamekwisha bwana wanakubali wanaume kuoana! SASA HUWA SIMUELEWI SANA HAPA!
Lakini cha kushangaza Deni la taifa limeongezeka kwa 3.9 trillion ndani ya mwaka mmoja....sijui zimetumikaje, sasa deni ni trillion 14.4.....
 
CCM na Poli-CCM wasije wakaanza kusema kuwa na mbunge ndiye aliyewaambia wafanye hivyo. Nassari wewe bado ni kijina, nakushauri usije ukaingizwa kichwa kichwa katika mambo kama hayo. Najua haki ya wananchi kusikilizwa ipo lakini isitafsiriwe kuwa hawakufuata sheria. Jambo kama hilo linaweza kuchochewa na CCM kwa kutumia 'system' yake ili kuonesha kuwa CDM wanawaongoza watu kuleta vurugu.

Kama kuna sheria ya raia halali wa tz anyanyasike kwa kukosa ardhi ndani ya nchi yake, na mgeni kupewa maeneo makubwa, huku mwananchi akilalamika anaambiwa asubiri sheria, hiyo sheria haifai kufuatwa na mapambano ni njia pekee ya kudai haki!!
 
Wananchi wa Jimbo la Arumeru waishio pembezoni mwa eneo la Dolly (eneo ambalo wazungu wamemilikishwa)kuanzia jana jioni wameandamana kuelekea eneo hilo na kuanza kungoa fensi inayozunguka eneo hilo.Na hali ilizidi kuwa mbaya pale polisi wa kutuliza ghasia walipo fika eneo lile bila hata kuwauliza wananchi nini hoja yao wakaanza kuwarushia mabomu ya machozi wananchi waliokuwa kwenye eneo hilo na hapo ndipo na wananchi wakaanza kuwajibu kwa mawe maaskari wale hali iliyopelekea idadi ya maaskari kuongezeka na wananchi nao kuongezeka.

Na hoja au madai ya wananchi wa eneo lile kwanza kabisa wanataka barabara iliyokuwa ikitumika kuunganisha kijiji cha MAJI YA CHAI na Maroroni iliyofungwa baada ya hao wazungu kuchukua eneo hilo ifunguliwe kwani imekuwa ikiwalazima kuzunguka mbali sana baada ya barabara hiyo kufungwa.

2.Kulikuwa na shule ya msingi ndani ya eneo hilo wazungu walio milikishwa ambapo baada ya wazungu kuchukua eneo hilo na kulifensi shule iliamishwa na kupelekwa eneo ambalo ni mbali na makazi hivyo kuwasababishia usumbufu watoto.

3.Wanadai baada ya muafaka wa barabara na shule kupatikana watataka sasa wajue nini muafaka hiyo ardhi iliyomilikishwa kwa mzungu mmoja huku wananchi wa eneo husika wakiteseka kwa kukosa ardhi.

4.Wanasema huu ndiyo wakati muafaka wa wao kudai haki yao ya msingi na kufanya hivyo ni kumkumbusha Mheshiwa Nassary kuanza kufanyia kazi ahadi alizozitoa kwenye kampeni kubwa likiwa ni hili swala la ardhi kubwa kumilikiwa na watu wachache.Na wanamatumaini huu sasa ndio wakati wao wa kukomboa ardhi zao umefika.

Nipo maeneo ya hapa nitajitahidi niane kama naweza nikawaletea na picha ili mueze kuona huu umati wa wananchi ulivyumkubwa hapa.

Na kwa Wananchi wa MBARALI Mbeya ni muda mwafaka kumtimua mwekezaji kwenye Mashamba ya Mpunga Mbarali(NAFCO) na pia kupora maeneo yote yaliyopewa wawekezaji kati ya 2007-2009 kwa kisingizio cha kupanua Hifadhi ya Ruaha.NI WAKATI WA KUREJESHA ARDHI YOTE ILIYOPORWA MKOA MZIMA WA MBEYA NA VIUNGA VYAKE.Julius Malema na Robert Mugabe Njooni mtusaidie mbinu za kuwaondoa hawa Mabepari
 
"3.Wanadai baada ya muafaka wa barabara na shule kupatikana watataka sasa wajue nini muafaka hiyo ardhi iliyomilikishwa kwa mzungu mmoja huku wananchi wa eneo husika wakiteseka kwa kukosa ardhi"

THIS IS NOT TRUE THERE MANY TANAZANIA'S HAVE BOUGHT LAND AT DOLLY FARM AND SIO YA MZUNGU MMOJA.
 
kwa Wadau tu, hivi inakuwaje Mzungu toka ulaya, america au kwingineko apewe ardhi ktk maeneo ambayo tayari wazawa wana tatizo la ardhi. Hivi tuko tayari kuua raia wetu kwa ajili ya wakoloni kweli jamani. tufike mahali tuone aibu na kuwapendelea WATZ
Wananchi wa Arumeru tukajifunze mbinu katika mashamba kule Babati, maana walikuja mawaziri wanne baada ya kitu fulani katika mashamba ya wale wanaojiita ni waingereza na watanzania wenye asili ya kiasia. Hapo jirani pia tujifunze kwenye mashamba ya Kimaro tutapata suluhu tu, wala tusisubirie Nassari aje, tutamweka mazingira magumu. Sisi ni kujua kuwa ardhi ya Arumeru ni ya wa Arumeru kama kuna mwingine aliipata na wala hana hata mchumba Arumeru, na ardhi yetu ni ya serikali lakini ni ya koo zetu...tumuulize si kwa uungwana tu bali kwa uungwana na matendo alikotoa ujasiri wa kuja kwetu kuchukua ardhi bila ya ridaa yetu
 
Back
Top Bottom