ARUMERU: Aliyejaribu kumfufua marehemu nusura auawe

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Arumeru.JPG

Hali ya taharuki imetokea katika Kijiji Cha Oldadai wilaya Arumeru, Mkoani Arusha mara baada ya kuibuka mtu mmoja anayejiita nabii na kuzuia kuzikwa kwa mwili wa marehemu akidai ana uwezo wa kumfufua hali iliyolazimu mamia ya wananchi kufurika kushuhudia tukio hilo .

Tukio hilo la kustaajabisha limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika familia ya marehemu Remmy William aliyefiwa na mtoto wake aitwaye Hance Remmy (19) aliyefariki kwa ajali ya pikipiki siku sita zilizopita ,ambapo Mara baada ya kukamilika kwa shughuli za ibada ya mazishi mwili huo ulipelekwa kaburini ndipo nabii huyo alipoibuka na kudai marehemu yupo hai na anauwezo wa kumfufua.

Mtu huyo alifika katika kaburi la marehemu akiwa amevaa nguo ya kimasai na ndugu wa marehemu na kuingia ndani ya kaburi lililofunikwa kwa turubai na kuanza kumwaga maombi ya kumfufua marehemu akidai mungu amemwonyesha maono kuwa marehemu hajafa Ila alichukuliwa kimazingara na bado yupo hai .

Hata hivyo wachungaji kadhaa walipokuwa makaburini kwa ajili ya shughuli za mazishi walilazimika kuondoka na kumwacha nabii huyo wa uongo aendelee kufufua marehemu.

Mtu huyo aliendesha maombi hayo kwa zaidi ya saa tano hadi saa 11 jioni bila mafanikio Jambo lililoibua hasira kwa wananchi waliokuwa wamefurika kushuhudia tukio hilo lisilo la kawaida.

Baada ya kuona hakuna dariri za marehemu huyo kufufuka,nabii huyo aliamua kutoka ndani ya kaburi , ndipo wananchi walipokuwa wamekusanyika walipoanza kumzonga wakitaka kumshambulia ndipo alipotimua mbio na kutokomea migombani.

Baadhi ya shuhuda wa tukio hilo waliokuwa wamefurika katika eneo la tukio wamekerwa na hatua ya familia ya marehemu kuwa na Imani potofu ya uwepo wa mtu mwenye uwezo wa kufufua marehemu ,kwani mwenye mamlaka hayo alikuwa ni Yesu kristo pekee.

Diwani wa kata ya Oldadai ,Oberd Mollel ambaye alimnusuru mtu huyo asipigwe na wananchi wenye hasira Kali baada ya kushindwa kumfufua marehemu,alidai kuwa hakuna mwenye uwezo wa kufufua marehemu na kwamba mtu huyo nitapeli.

Diwani huyo alisikitishwa na kitendo Cha familia hiyo kuamini kwamba ndugu yao hajafa na kwamba alichukuliwa kimazingara na kuamua kuruhusi nabii wa uongo kuja kujaribu kumfufua marehemu Jambo ambalo halikuwezekana badala yake ameondoka kwa aibu.

"Kwa kweli Jambo hili limetusikitisha Sana na kuibua hisia tofauti kwa wananchi ndio maana nimeita polisi ili wakamhoji mtu huyo anayejiita nabii kwa kuzua haruki kwa wananchi''alisema

Hata hivyo Askari Polisi walioofika eneo la tukio kujaribu kumtia mbaroni mtu huyo walishindwa kufanikiwa baada ya mtu huyo kufanikiwa kutoroka na kwamba hadi kipindi hiki kinaondoka eneo la tukio jitihada za kuzika mwili wa marehemu zilikuwa zinaendelea.

Ends.....
 
Nimegundua kwa nini Maaskofu Gwajima na TB Joshua kwenye msiba wa marehemu JPM walijikausha kama vile hapajatokea hapa duniani kuishi watu wa matendo na majina yao.
sorry TB Joshua alikuwepa kwenye msiba wa Magufuli?
 
Matagaaaaaaaa matagaaaaaaaa matagaaaaaaaa matagaaaaaaaa uuuuwwiiiiiiii uuuuwwiiiiiiii uuuuwwiiiiiiii njoooniii huku njoooniii huku njoooniii huku

Kumekuchaaa kumekuchaaa kumekuchaaa kumekuchaaa
 
Mimi nimeshangaa mtu aliyekaa kaburini masaa matano akipiga mikelele huku kafunikwa na turubai anawazidi vipi mbio hadi kufika migombani?
Hata hivyo Askari Polisi walioofika eneo la tukio kujaribu kumtia mbaroni mtu huyo walishindwa kufanikiwa baada ya mtu huyo kufanikiwa kutoroka na kwamba hadi kipindi hiki kinaondoka eneo la tukio jitihada za kuzika mwili wa marehemu zilikuwa zinaendelea.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom