Artumas asks Dar for $7m bailout for Mtwara gas-to-power project

safi kwa detail nzuri..

jamani hivi uelewa wa wawakilishi wetu (wabunge) achilia mbali ukereketwa wao wa kijinga, nadiriki kusema wana upeo wa chini sana wengi waooo...hawastahili hata kidogo kuwa law makers na wawakilishi wa wananchi...ni mambumbuuuuuuu...

ukifuatilia mijadala yao wakati wa kujadili mambo muhimu kama nishati, utagundua upeo wao mdogo kwa kuleta mipashoo zaidi kuliko hojaaa...
sio watu makini jamani....wengi hawajui wajibu wao kama wabunge, wengine ni wapenda kuchangia kwa sifa ya kusikika kwenye media zetu ambazo pia ni zao la yale yale upeo mdogoooo...

tumeshuhudia wabunge wachache wa upinzani (dr slaa, hamad, zitto, nk) wakichangia kwa umakini unaostahili katika bunge.

haya matatizo ya tanesco/richmond/dowans na sasa yaongezeka arthumas ni dalili za umbumbu wetu katika kukabiliana na tatizo la nishati nchinii..

haiwezekani kila siku tudai mafisadi wanaingilia miradi yetu, wansheria wanakosea mikatabaa, viongozi hawatambui wajibu wao...na bado wananchi tupo tupo tuuuu...

kuna zaidi ya tatizo....hatuna rasilimali watuuu (we desperately need HUMAN CAPITAL)

Tuna wanasheria waliobobea kwenye mikataba ya nishati??? tuna wabunge makini katika kujadili kuhusu sekta ya nishati? tanesco wakoje kwa upande wa menejimenti (bodi na wafanyakazi wa shirika)? Mgeni wetu EWURA anajenga vipi uwezo wa kuregulate sekta ya nishati? Media yetu ina watu makini(waandishi) wenye upeo na uchumi na sekta ya nishati????????????


Tunao hao wataalamu tatizo ni njaa na ufisadi
 
Hebu nisaidie, hivi kweli haya mambo mtu kama waziri mkuu hajui?? Jamani mi mpaka najisikia vibaya kuona watu wanafanya vitu utadhani wamerogwa!
 
Si kitu kipya kuchelesha projects hizi... Songosongo Gas to Power pia ilikutana na dhahama ya kifisadi ikawa delayed kwa urasimu wa kijinga ili kuipa IPTL mwanya. Matokeo yake tunayajua. 300MW project ilikuwa inaleta giza kwenye Dowans deal. Barrick wanatoa hela za mradi watu wanagoma kwa sababu za kishenzi!

Tanesco walitaka waingizie USD 400Milioni waanze kuzifisadi kwa kujinunulia magari ya bei mbaya ....manake ndio viongozi wengi wanaloliweza.
 
mpendanchi 2 thanks much,seems unaelewa nini kinaendelea kwenye hiyo Energy sector Tanzania kuliko wapuuzi wengi waliojaa Dodoma na magogoni,hiyo 300MW project ya Artumas nafikiri jamaa ndio bets zao zote zilikuwa pale na wakajua ita offset loss ya charity project nyingine kama hiyo ya Ruvuma/mtwara/Songea electrification,niliwahi kusikia jamaa wanazalisha umeme mwingi kuliko wanaoweza kuwauzia TANESCO ndio maana wanapata hasara maana Tanesco walikuwa wanawachezea game ya kukataa kununua umeme wao kwa madai wano mwingi huku wakitumaliza kwa migao,hapa kuna ufisadi mkubwa sana upande wa serikali na Tanesco na press/wananchi inabidi iwaweke kiti moto mawaziri kupata ukweli maana ukweli nchi haina umeme na umaskini unaongezeka kumbe tuna gas na uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosheleza karibu nchi nzima,na hiyo fertillizer factory kama wangecheza game yao vizuri leo watu wangepata kazi na kilimo kukua na tunge save dollar nyingi sana za kununua mbolea na chakula nje lakini mafisadi wanatumaliza na deal zao za kishenzi,nafikiri umeme na mbolea serikali ingeweza kufunga macho na kuchukua hizo project zenyewe maana zina multiple effect kwenye economy ya nchi then baada ya muda wangeweza hata kuuza hizo project kwa wananchi...cha ajabu Richmond,Dowans,IPTL zimekula pesa nyingi kuliko pesa zinazohitajika kusimama 300MW artumas projects,nasikia yule Nigerian billionaire wa Dangote group anataka kuweka pesa zake mtwara kwenye hizo mbolea...siwaamini lakini hawa Nigerians ukizingatia ata deal na mfisadi anaowajua basi tujue ni umaskini kwenda mbele!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom