ART of WAR Katika Siasa za Tanzania

Rutayuga91

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
449
249
Robo mwaka imeisha na kwa namna fulani lile joto la siasasa limepungua kidoogo. Wengine watampongeza Rais na wengine wanadai kwamba mgonjwa amemeza Panadol. Ila ningependa tuangalie jinsi siasa ililvyokwenda tukitumia kitabu cha Art of War cha Sun Tzu ili tujue nani ana dalili ya kushinda katika hii vita ya kisisasa. Tuchukulie 2020 kama vita na hii mihemko ya kisiasa kama kampeni.

1. If your opponent is of choleric temper, seek to irritate him. Pretend to be weak, that he may grow arrogant.

Wapinzani wamefanikiwa kum-irritate Raisi naRais akaingia mtegoni kiuraisi kabisa. Walipo ng’ang’ania habari fulani jamaa akatoa matamko ya ajabu ikiwemo kutishia vyombo vya habari. Jambo hili linampelekea Rais kuonekana kama mbabe hivyo kumpa nguvu Tundu Lissu. Ila la kuigiza kuwa dhaifu kwa kweli sijaliona kwa yeyote.

2. If he is taking his ease, give him no rest. If his forces are united, separated them.

Wapinzani wamefanikiwa kumpeleka Rais mchakamchaka wa maana. Lilipoibuka la vyeti vya PCM-DAB wakashambulia sana, hawajamuacha apumzike wakashambulia na uvamizi wa Clouds. Alipekamata makontena ya mchanga wa dhahabu bado wakashambulia tena. Kumtengua Nape bado wakashambulia tena. Nahisi kwa sasa Rais anapumua kiaina.

Marais waliopita walifanikiwa kuwagawanya wapinzani ila kwa huyu wa sasa naona kama wapinzani ndio wanagawanya vikosi vyake.

3. Attack him when he is unprepared, appear where you are not expected.

Wapinzania walishambulia katika sehemu ambayo serikali haikutarajia. Pale alimpomtimua Nape walidhani watu watashagili kwa kuwa ndiye aliwaondolea Bunge Mubashara. Wapinzani wakageuka na kuwa upande wa Nape, jambo ambalo halikutarajiwa kirahisi hivyo. Alipokamaya kontena za mchanga na Range Rover kwenye kontena la mitumba alidhani atanyamazisha upinzani. Bila kutarajia wapinzani wakashambulia.

4. In a war, let your great object be victory not lengthy campaigns.

Pande zote zimecheza vyema. Hii mihemko ya kisiasa ukiiendeleza kwa muda mrefu haina maana. Acha la zamani lipoe kidoogo kisha anzisha jipya. Kama la zamani litakuwa na manufaa baadaye, wanaweza kulifufua.

5. To secure ourselves against defeat lies within our hand, but the opportunity to defeat the enemy is provided by enemy himself.

Sijaona kama kuna mwnye ulinzi mzuri. Kwa upande wa serikali wamekuwa wakitoa nafasi nyingi za kushidwa na wapinzani. Siju strategists wa serikali wapo wapi.


Kila mhusika ajitathmini kwa hayo machache niliyoandika. kama kuna uwezekano basi watafute kitabu hicho cha Art of War wakisome ili kukwepa makosa madogo madogo.
 
Ujinga mtupu, 2020 Bashite ndio atakuwa agenda ya upinzani ? Unaona ni ufahari kumpinga Rais katika inshu ya madini, inamaanisha nyie hamna uzalendo, kupinga chochote ndio furaha yenu.
 
naona unamap matukio lkn kwa akili yangu ndogo, hayo yote yametokea bila kupangwa.

Tsu NZu(General anaesadikika alikuwa mchina ingawa wa kwanza kuonekana na kitabu hicho ni mzungu) alikuwa anaelezea Mipango. Wapinzani wanadandia matukio ya kijamii na kuweka kambi.

Unafananisha visivyofananishwa, Unawapa sifa wasizostahili
 
Kifupi upinzani wamepoteana kabisaaaa!.
Itachukua miaka mingi sana kuimarika.
Wabnafsi sana.
Kitabu cha Art of War akibebi yanayotokea kwa wapinzani nchini.
Naona unajaribu kuwafariji tu.
Ni kundi LA wachumia tumbo waliojificha nyuma ya mgongo wa siasa.
Kwa mfano Mboe kutolipa kodi serkalini,kisha kuumbuliwa na yeye kukaa kimya,in ishara tosha kua hafai kua kiongozi.
Lowassa nae alizunguka nchi nzima na kuambulia kiti kimoja kati ya viti 21 vya serikali ya mtaa.
Vita ya ufisadi wapo kimya!

Kumbe wengi wao ni wauza ngada.

Siraha waliobakiza in front page za magazetini,na kauli tata za Magufuli.
Kifupi upinzani kwa sasa in bora liende tu.
 
Suala la Bashite, macontena ..yasingetokea wapinzani wasingeongea lolote? Tumia akili sana mtoa mada kabla ya kutoa maana humu ndani kuna watu ni very critical tofauti na udhaniavyo
 
Hakuna hata mmoja aliyetumia Art of War. Ila nimeeleza ni kwa namna gani matukio hayo yanaelezewa kwenye Art of War. Kama watapata nafasi ya kusoma Art of War wataweza kutengeneza nafasi nyingine nyingi tu. Rais wetu pia apitie mule ili ajue namna ya kujilinda na kuandaa mashambulizi dhidi ya maadui zake.

Pia nilipoandika wapinzani sikuwa na maana ya vyama vya upinzani pekee. Hawa ni wale wote wanaompinga Rais na serikali yake kwa namna yoyote ile. Iwe chama, taasisi, mfanyabiashara na hata mwananchi wa kawaida.
 
Back
Top Bottom