Arsene Wenger: Tuna matumaini kushinda ligi kuu ya Uingereza

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_94241359_wenger.jpg5.jpg

Arsenal ni sharti iamini kwamba bado inaweza kushinda ligi ya Uingereza msimu huu licha ya pengo la pointi 12 kati yake na viongozi wa ligi Chelsea ,kulingana na mkufunzi Arsene Wenger.

The Gunners, ambao kwa mara ya mwisho walishinda ligi mwaka 2004 walishuka hadi nafasi ya 4 baada ya kushindwa 3-1 na Chelsea Jumamosi iliopita.

Kikosi cha Wenger kinaialika Hull City katika uwanja wa Emirates baada ya kupoteza mechi nne kati ya tisa ilizocheza.

''Bado hatujasalimu amri'', alisema raia huyo wa Ufaransa.''Hata iwapo unadhani tumeshafanya hivyo, mimi bado sijasalimu amri-hatuweza kufikiria hivyo''.

Kwa sasa ni pointi tano pekee zinazotenganisha Tottenham ilio nafasi ya pili na Manchester United iliopo katika nafasi ya sita.

Aliongezea Wenger: Tuko katika eneo ambalo ni gumu sana na ugombeaji wa kila nafasi ni muhimu sana msimu huu ikilinganishwa na ule uliopita.

Chanzo: BBC/Swahili
 
Hapo hiyo habari wangemalizia na maneno "UKITAKA VICHEKESHO KAMA HIVI TUMA SMS VICHEKESHO KWENDA 15344" VODACOM KAZI NI KWAKO.
 
Huyu hana tofauti na msemaji wa ruvu shooting ambaye bado anajigamba kuwa ruvu shooting itachukua kombe msimu huu wakati kuna pengo la point 22 na anayeongoza ligi.
 
Huyu hana tofauti na msemaji wa ruvu shooting ambaye bado anajigamba kuwa ruvu shooting itachukua kombe msimu huu wakati kuna pengo la point 22 na anayeongoza ligi.
Na yule thobias kifaru rugalambwike hawana tofauti "yanga akija hapa manungu watakuta tumewaandalia mashada ya maua "wakapigwa 3 akihojiwa akasema "kuna makosa madogo madogo mwalimu mkenya siang'aa ameyaona hivyo atafanya marekebisho "
 
Labda hao wengine waliowatangulia wafungwe mechi zote zilizobakia.
Katika maisha ukiwa na moyo wa matumaini na kutokata tamaa kama huyu mzee kufanikiwa ni lazima ila sasa kuna matumaini mengine ya kujiongopea hapo ndipo penye utata.
 
Back
Top Bottom