Arsenal (The Gunners) | Special Thread

#Breaking_news Unai Emery aweka historia mpya.
Kocha wa Arsenal Unai Emery ameandika historia mpya apo jana mara tu baada ya
Kuichapa Valencia magoli 4 kwa 2 na kufanikiwa kutinga hatua ya Fainal ktk mashindano ya Europa League.
Kupitia matokeo hayo imempelekea adi sasa kuwa ndio kocha pekee wa kuhistoria.
Kwa kuingia fainal ya Europa League mara nyingi.
Ikiwa ni hii ni fainal yake ya nne kupitia mashindano haya.
2013-14Sevilla
2014-15Sevilla
2015-16Sevilla
2018-19 Fainal Arsenal
Baada ya kuwa na historia nzuri kupitia kombe ili
Je ataweza kufanikiwa tena kulibeba kombe mbele ya mpinzani wake Chelsea.
YOTE KWA YOTE TUKUTANE FAINAL NDANI YA BAKU PANAPO MAJAALIWA 29/5/2019
FB_IMG_1557467652899.jpeg
 
Kwa taarifa yenu mashabiki wa Chelsea msitegemee tutafika penalty siku ya final.... Ngoma ni dk 90 tunamaliza shughuli, Chelsea ni mbwa asiyeng'ata kwe big matches hafurukuti wala hajui kudefend in short Chelsea ataupiga mwing ila ushindi wetu sema woyoooooooo
 
Huyo chelsea tumemgonga 2-0 kwenye ligi EPL, so hawezi furukuta kwa lolote kwanza katimu kadogo tuu kamemtoa maji hadi matuta; Chelsea labda zamani kwa sasa uchochoro tuu............
kwenye Epl Chelsea hajakufunga? mbona unatamba kufunga wakati umefungwa pia au kufunga kwako kulikupa Point 6 na kufungwa kwako ulipoteza point 1,ongea ubora mwingine wa Arsenal sio kuifunga Chelsea Well wakati ilikufunga pia
 
Niseme jambo moja kwa mashabiki fata upepo na wale mashabiki wafia Arsenal au arsenal lialia zaidi sana niongee na wale washabiki damu wanaoifahamu Arsenal.

Ufike wakati tutambue weakness za kikosi na Mwalimu wetu kwa ujumla, zama zile za babu timu inashambuliwa mzee amekaa chini zilishapita. Enzi zile unajishauri ukaangalie game au lah zilishakwenda na babu.

Kwasasa ni wakati wa kujiuliza tumeshiriki Europa mara ngapi bila kugusa Final je!? Tulipo kutana na timu zilizo tusumbua kipindi cha babu hali ilikuaje? Record yetu kwa away game ikoje? Wakati huu na enzi za babu.

Kuna badiriko lolote emery ameleta kwenye hii timu kama jibu ni yes sasa tujifunze kutmbua changamoto za kikosi miaka hiyo na sasa je kosa lolote la kiufundi shida ni Emery mwenyewe au ni aina ya wachezaji?

Binafsi nikimuangalia mwalimu naona yupo 98% right sema sisi hatuna watu ambao kwa asilimia 100 ni demanded players kwenye baadhi ya mifumo yake.

Tuna shamble players wengi sana kikosini kiasi inaumiza wakati mwingine. Sema napenda falsafa zake kiukweli zinatia moyo sana. Unajua nimeshuhudia Ozil akikaba kitu ambacho kilikua adimu kukishuhudia.

Backline yetu ni mbovu na hatuna namna sababu ukweli uko wazi flani akipata shida mbadala ni tatizo.

Lakini tumeshuhudia timu zinazotumia pesa kwenye usajiri zikihaha kutafuta nafasi.

Jambo la Arsenal kufika fainali tu kwangu ni badiriko kubwa ambalo sikuwahi kufikir lingepeta nafasi lakini kwakua tumepata naodha sina shaka tena na Arsenal.

Imani yangu na huyu Kocha ni kubwa sana. Kwanza huu ni msimu wake wa kwanza pili hii mgeni kwenye ligi lakini kwa ugumu wake ametufikisha hapo. Well tumeruhusu magoli mengi lakini at least tunafunga magoli pia. So hilo tu kidogo naona kuna khali flani ya kiushindani japo kuna makosa Madogo.

Rai yangu kwenu wote Arsenal wenzangu, msiwe wepesi kuhukumu tuwe wepesi kusoma mchezo na kuhusianisha Uzoefu na Muda.

Jurgen klopp aliomba misimu mitatu. Then after wamjudge leo hii msimu watatu amewafikisha Liverpool panpostahili who knows?.

Kuna aliyejua pep angefikia alipo sasa, he mnakumbuka msimu wake wa kwanza alianzaje?

Ni swala la muda tu wanazuoni.

Remember mema timu sio kejeli wazee.
 
Huyo chelsea tumemgonga 2-0 kwenye ligi EPL, so hawezi furukuta kwa lolote kwanza katimu kadogo tuu kamemtoa maji hadi matuta; Chelsea labda zamani kwa sasa uchochoro tuu............
Pigeni kelele zenu lakini Asernal hamuwezi kuwafunga Chelsea anayebisha aendelee kubisha lakini ukweli unabaki palepale,mjiaandae kisaikolojia.
 
Kwa taarifa yenu mashabiki wa Chelsea msitegemee tutafika penalty siku ya final.... Ngoma ni dk 90 tunamaliza shughuli, Chelsea ni mbwa asiyeng'ata kwe big matches hafurukuti wala hajui kudefend in short Chelsea ataupiga mwing ila ushindi wetu sema woyoooooooo
Haya ni maneno ya mtu aliyekata tamaa,uzuri mpira hauchezwi kwenye majukwaa,ila kwakifupi sijaona timu ya kumfunga Chelsea labda itokee bahati iwe kwenu,kinyume chake lazima mtaukalia.
 
Pigeni kelele zenu lakini Asernal hamuwezi kuwafunga Chelsea anayebisha aendelee kubisha lakini ukweli unabaki palepale,mjiaandae kisaikolojia.
Ivi wewe unaongelea chelsea ipi kwani ipo nyingine tofauti na hii iliyofungwa 2-0 na arsenal kwenye mchezo wa ligi ya England? maana nakumbuka Arsenal walimfunga chelsea wanaojiita the bluess 2-0............
 
Hebu jaribu kunisoma vizuri, ingawaje mara nyingi kiswahili changu hakijanyooka.
Iwapo timu yoyote ambayo tayari ipo top4 ya EPL itashinda kombe la UEFA au EUROPA basi England itaendelea kubaki na nafasi nne za kushiriki UEFA. Iwapo mshindi wa Either UEFA au EUROPA atakuwa nje ya top4, basi mshindi huyo atashiriki UEFA, ikiwa na maana kuwa England atakuwa na washiriki watano UEFA, na watatu EUROPA. Iwapo ManCity atachukua FA basi timu iliyopo nafasi ya 7 itashiriki Europa, Iwapo Watford atachukua FA basi itashiriki Europa na timu iliyopo nafasi ya saba haitashiriki Europa.
Asante kwa kunisoma

King of London is back ..

Timu za London zinakuja kutawala tena soka la England na pengine Europe nzima.

Huwezi amini Spurs anabeba UEFA uku matajiri wa London kaka zao tukifanyua EUROPA.

Msimu huu Looserfool hubebi chochote...

Kwani ni Mwaka gani Timu za London zilipowahi Kutawala Soka la England?
 
Huyo chelsea tumemgonga 2-0 kwenye ligi EPL, so hawezi furukuta kwa lolote kwanza katimu kadogo tuu kamemtoa maji hadi matuta; Chelsea labda zamani kwa sasa uchochoro tuu............
Kwa wewe uyo assanal akugongwa 3 pale darajani? Au mnajisahaulisha tu...
 
Kwani ni Mwaka gani Timu za London zilipowahi Kutawala Soka la England?
London imetawala EPL misimu kadhaa apo nyuma ukiondoa misimu wa jana na huu unaoishilia. Wewe na Liverpool yako ulikuwa unagombania kucheza Europa uko na akina arsenal, Leicester ..

Sasa tunarudi tena. London is back on top soon!!
 
Kwa taarifa yenu mashabiki wa Chelsea msitegemee tutafika penalty siku ya final.... Ngoma ni dk 90 tunamaliza shughuli, Chelsea ni mbwa asiyeng'ata kwe big matches hafurukuti wala hajui kudefend in short Chelsea ataupiga mwing ila ushindi wetu sema woyoooooooo
Jidanganye hivyo,

Europe league itawahusu tena
 
Back
Top Bottom