Arsenal (The Gunners) | Special Thread

kwa taarifa zilizoingia usiku huu ni kwamba denis Suarez arasafir kwenda London mara baada ya Barcelona kumaliza mchezo wa leo wa copa de ley kwa taarifa za uhakika kutoka kwa kike marin muandishi wa habar kutoka ujeruman ni kwamba Arsenal wameshafikia makubaliano ya kumsajir Suarez kwa mkopo kwa kipengele cha kumnunua mwisho wa msimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
>

Kiungo wa kati wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 28, amekubali kujiunga na Juventus mwezi Juni mwaka huu. (Guardian)

Meneja wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger ameombwa kuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Qatar.

Kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suarez, 25, anataka kuhamia Arsenal mwezi huu wa Januari, ingawa klabu yake awali aikutaka kumuachia lakini imeripotiwa kuwa Suarez amekuwa akiwafosi Barcelona kumuachia ajiunge na Washika bunduki hao wa london na Arsenal ndio klabu pekee iliyomvutia.

Arsenal wanapania kumsajili kiungo wa kati wa Porto Hector Herrera, 28, kupitia uhamisho bila malipo msimu huu kuchukua nafasi ya Aaron Ramsey, ambaye mkataba wake unaelekea kukamilika. (Tutto Mercato web)

Unai Emery ameidhinisha Arsenal kumsajili winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco, 25, kutoka klabu ya Dalian Yifang inayoshiriki ligi kuu ya Uchina.(Football Mercato)

Na habari zilizotufikia hv punde zinasema>> Rais wa Barcelona Joseph Maria Bartomeu amemwambia kiungo wa kati wa klabu hiyo Denis Suarez 25, ambae analengwa na Arsenal anaweza kuondoka Nou Camp. (Marca).

Sasa mambo yanakwenda vizuri na nawasalimia wale waliokuwa wakim,beza Yannick Carrasco kwamba kiwango kilimuishia ndio maana akakimbilia China mujiandae jamaa anakuja kuwaonyesha kiwango cha mbio na uwezo aliojaliwa na hapo tutakuwa tumepata Winger mwenye Skills za kutosha.
IMG-20190111-WA0001.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka aliweza kuchezea vilabu vikubwa ina maana ni bora ..sasa hapo ukimtoa Auba ni nani mwingine anaye mshinda Morata? Lacazzete??

Tatizo la morata ni kupaniki tu, lakini akituliza akili ni bonge la straika..

Sasa unadhani apo Arsenal ni nan atamkata namba Morata?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani nina Morata na Lacazzete halafu nampiga benchi Lacazzete Morata acheze. My friend pass me that kush!
 
NGOJA NIKWAMBIE KITU KUHUSU MTU HUYU.

Anafahimika kwa jina la Sven Mislintat. Kazi yake ni kuzunguka maeneo mbalimbali duniani kutafuta wachezaji wenye vipaji halisi vya vya kucheza soka. Kazi hii inafahamika kama Skauti. Sven Mislintat kwa sasa anafanya kazi kama skauti mkuu wa Arsenal. Mwaka mmoja umepita tangu aanze kufanya kazi hii akiwa Arsenal.

Mwaka 2009 alimbidi asafiri mara sita kwenda nchini Japan, akiwa kama skauti mkuu wa Borussia Dortmund. Safari za kwenda Japan zilikua ni kwa ajili ya kumfatilia kijana mmoja wa miaka 20. Shinji Kagawa. Alimuona mara ya kwanza, akamuona mara ya pili, tatu, nne, tano, sita bado hakujiridhisha na kile alichokua anakiona.

Akatafuta video zaidi ya kumi za kijana huyu. Akiwa na jopo la maskauti wenzake walijiridhisha na uwezo wake. Baadae akapeleka ripoti yake kwamba Shinji Kagawa asajiliwe. Majira ya kiangazi mwaka 2010, Borussia Dortmund ikalipa Euro laki tatu na nusu kumsajili.

Miaka miwili baadae aliuzwa kwenda Manchester United kwa gharama ya Euro milioni 15. Faida ya zaidi ya Euro milioni 14. Huku nyuma Kagawa aliondoka akiwa ameisaidia Borussia Dortmund kushinda mataji mawili ya Bundesliga. Naam. Hii ilikua ni kazi yake Sven Mislintat.

Mbali na Kagawa, Sven Mislintat alihusika kuwaleta wachezaji wengi kwenye kikosi cha Borussia Dortmund. Robert Lewandowski, Mario Gotze, Matts Hummels, Marco Reus, Pierre-Emerick Aubameyang, Jakub Blaszczykowski, Ilkay Gundogan, Raphael Guerreiro, Ousmane Dembele, Neven Subotic, Sven Bender na Henrikh Mkhitaryan ni baadhi ya wachezaji hao.

May 2016, Sven Mislintat alikamilisha dili la kumleta Osmane Dembele kutoka nchini Ufaransa kwenye klabu ya Rennes. Osmane akajiunga na Borussia Dortmund. Mwaka mmoja baadae, aliuzwa kwenda Barcelona kwa gharama ya Euro milioni 105 ambazo zingeweza kuongezeka hadi Euro milioni 145.

Hii inabaki kuwa biashara nzuri zaidi aliyowahi kuifanya. Ndani ya mwaka mmoja tu, Borussia Dortmund walipata faida ya zaidi ya Euro milioni 100. Ni pesa nyingi sana ambazo zilitokana na kazi kubwa aliyoifanya Sven Mislintat kwa kumleta Osmane nchini Ujerumani.

Ingawaje kwa sasa hafanyi kazi hiyo pale Borussia Dortmund, klabu inanufaika na wachezaji aliowahi kuwaleta. Wiki iliyopita Christian Pulisic alisaini mkataba na kuichezea Chelsea msimu ujao akitokea hapo. Mkataba uligharimu Euro milioni 64.

Pulisic kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa Borussia Dortmund ni kijana aliyeletwa na Sven Mislintat. Mahmoud Dahoud, Julian Weigl, Manual Akanji, Dan-Axel Zagadou, Maximilian Phillip, Jacob Bruun Larsen, Alexander Isak na Sergio Gomez ni baadhi ya wachezaji vijana ambao ni ‘potential’ nzuri kwa Borussia Dortmund hivi sasa.

Kuna bwana’mdogo anaitwa Jordan Sancho pia. Ni muda tu unaosubiriwa ili aweze kuondoka Dortmund. Amekua na msimu mzuri hadi sasa. Huyu nae ni zao la Sven Mislintat alimleta kutoka Manchester City. Kama ataondoka, basi Dortmund itapata fedha nyingi pia, kama ilivyokua kwa Christian Pulisic.

Huyu jamaa husafiri nchini nyingi duniani. Husafiri hadi nchi za Afrika pia. Alishawahi kusafiri hadi Afrika Kusini kumuangalia kijana Tashreeq Matthews aliyekua anacheza klabu ya vijana ya Ajax Cape Town. Hivi sasa Tashreeq ni mchezaji wa Borussia Dortmund.

Nchini Ujerumani alifahamika kama ‘diamond eyes’. Macho ya almasi. Alipewa jina hili kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuvitambua vipaji vya vijana wadogo.

Klabu nyingi zilimuhitaji. Bayern Munich ilimuhitaji sana. November 2017 alijiunga na klabu ya Arsenal akiziba nafasi iliyoachwa na Steven Rowley ambaye alikua skauti mkuu wa Arsenal tangu mwaka 1996.

Baada ya Steven Rowley kuondoka, Arsenal ihitataji mtu sahihi atakaye ‘fit’ vizuri kwenye nafasi aliyoiacha. Kumbuka Rowley alikua ‘master’ kwenye kazi. Arsenal ilisifika kuwa timu inayozalisha vijana wengi wenye vipaji halisi vya soka. Kazi kubwa ilifanywa na Steven Rowley. Alipoondoka akaja, Sven Mislintant ambaye ni ‘master’ pia kwenye kazi hii.

Lucas Torreira na Matteo Guendouzi ni wachezaji walioletwa Arsenal na huyu jamaa. Pierre-Emerick Aubameyang, Henrik Mikhtaryan, Konstantinos Mavropanos, Sokratis Papastathopoulos na Bernd Leno ni baadhi ya sajili zilizofanyika baada ya ushauri kutoka kwake.

Anatarajiwa kufanya mambo makubwa akiwa Arsenal pia kama ilivyokua kwa Steven Rowley. Alipokua anafanya mahojiano hivi karibuni alisema atafurahi kama akifanikiwa kumpata mchezaji mwenye akili ya Andres Iniesta.

Huyu ndiye Sven Mislintant. Jamaa iliyebeba mafanikio ya Borussia Dortmund kwa kipindi chote alichofanya kazi. Wachezaji aliowaleta kwa kiasi kikubwa waliisaidia Borussia Dortmund kushinda ubingwa wa ligi kuu nchini Ujerumani, mara mbili mfululizo mwaka 2011 na 2012. Mwaka 2013 Borussia Dortmund iliingia fainali ya UEFA Champions League pia. Sasa anafanya kazi kama skauti mkuu wa Arsenal
IMG-20190111-WA0022.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HII NDIO NAFAS NINAYOAMIN AKIPEWA AICHEZE ,BAS DUNIA ITATAMBUA KIPAJI CHA HUYU DOGO

󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Maitland-Niles reveals his desire to the winger for Arsenal:

“I’d like to be a winger. I feel more comfortable there...

...I like to think of myself as a winger at 25 years old, starting every week for Arsenal, scoring and assisting goals.”

[Sky Sports] #AFC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Manyumbu ni kitonga, anakufa vzr, tena majeruh wamerud karibu wote, halafu man u kwa FA ni mnyonge kwa arsenal

Toka nimejitambua ,ni mara 2 tu nimeshuhudia man u akimfunga arsenal kwenye FA ni mwaka 1999 goli la giggs, na 2016 ,

Kumbuka pia nina advantage ya home,

Sent using Jamii Forums mobile app

Ahhahahahahaah

Mkuu usije kubadili gia angani tu nasema, tarehe tajwa bado wiki mbili tu
 
Itakuwa bahat mbaya, ila kiufund sion wakitoka

Japo lolote laweza kutokea

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapo umenena kijana, Manchester United sio ya Kocha Mourinho tena ni kocha mpya ambae amekuja kwa hatua nzito nzito. Kushinda hiyo mechi inabidi mcheze kama ile Arsenal iliyompiga Van Gaal 3-0 katika siku ile sio Arsenal tunayoijua
 
NGOJA NIKWAMBIE KITU KUHUSU MTU HUYU.

Anafahimika kwa jina la Sven Mislintat. Kazi yake ni kuzunguka maeneo mbalimbali duniani kutafuta wachezaji wenye vipaji halisi vya vya kucheza soka. Kazi hii inafahamika kama Skauti. Sven Mislintat kwa sasa anafanya kazi kama skauti mkuu wa Arsenal. Mwaka mmoja umepita tangu aanze kufanya kazi hii akiwa Arsenal.

Mwaka 2009 alimbidi asafiri mara sita kwenda nchini Japan, akiwa kama skauti mkuu wa Borussia Dortmund. Safari za kwenda Japan zilikua ni kwa ajili ya kumfatilia kijana mmoja wa miaka 20. Shinji Kagawa. Alimuona mara ya kwanza, akamuona mara ya pili, tatu, nne, tano, sita bado hakujiridhisha na kile alichokua anakiona.

Akatafuta video zaidi ya kumi za kijana huyu. Akiwa na jopo la maskauti wenzake walijiridhisha na uwezo wake. Baadae akapeleka ripoti yake kwamba Shinji Kagawa asajiliwe. Majira ya kiangazi mwaka 2010, Borussia Dortmund ikalipa Euro laki tatu na nusu kumsajili.

Miaka miwili baadae aliuzwa kwenda Manchester United kwa gharama ya Euro milioni 15. Faida ya zaidi ya Euro milioni 14. Huku nyuma Kagawa aliondoka akiwa ameisaidia Borussia Dortmund kushinda mataji mawili ya Bundesliga. Naam. Hii ilikua ni kazi yake Sven Mislintat.

Mbali na Kagawa, Sven Mislintat alihusika kuwaleta wachezaji wengi kwenye kikosi cha Borussia Dortmund. Robert Lewandowski, Mario Gotze, Matts Hummels, Marco Reus, Pierre-Emerick Aubameyang, Jakub Blaszczykowski, Ilkay Gundogan, Raphael Guerreiro, Ousmane Dembele, Neven Subotic, Sven Bender na Henrikh Mkhitaryan ni baadhi ya wachezaji hao.

May 2016, Sven Mislintat alikamilisha dili la kumleta Osmane Dembele kutoka nchini Ufaransa kwenye klabu ya Rennes. Osmane akajiunga na Borussia Dortmund. Mwaka mmoja baadae, aliuzwa kwenda Barcelona kwa gharama ya Euro milioni 105 ambazo zingeweza kuongezeka hadi Euro milioni 145.

Hii inabaki kuwa biashara nzuri zaidi aliyowahi kuifanya. Ndani ya mwaka mmoja tu, Borussia Dortmund walipata faida ya zaidi ya Euro milioni 100. Ni pesa nyingi sana ambazo zilitokana na kazi kubwa aliyoifanya Sven Mislintat kwa kumleta Osmane nchini Ujerumani.

Ingawaje kwa sasa hafanyi kazi hiyo pale Borussia Dortmund, klabu inanufaika na wachezaji aliowahi kuwaleta. Wiki iliyopita Christian Pulisic alisaini mkataba na kuichezea Chelsea msimu ujao akitokea hapo. Mkataba uligharimu Euro milioni 64.

Pulisic kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa Borussia Dortmund ni kijana aliyeletwa na Sven Mislintat. Mahmoud Dahoud, Julian Weigl, Manual Akanji, Dan-Axel Zagadou, Maximilian Phillip, Jacob Bruun Larsen, Alexander Isak na Sergio Gomez ni baadhi ya wachezaji vijana ambao ni ‘potential’ nzuri kwa Borussia Dortmund hivi sasa.

Kuna bwana’mdogo anaitwa Jordan Sancho pia. Ni muda tu unaosubiriwa ili aweze kuondoka Dortmund. Amekua na msimu mzuri hadi sasa. Huyu nae ni zao la Sven Mislintat alimleta kutoka Manchester City. Kama ataondoka, basi Dortmund itapata fedha nyingi pia, kama ilivyokua kwa Christian Pulisic.

Huyu jamaa husafiri nchini nyingi duniani. Husafiri hadi nchi za Afrika pia. Alishawahi kusafiri hadi Afrika Kusini kumuangalia kijana Tashreeq Matthews aliyekua anacheza klabu ya vijana ya Ajax Cape Town. Hivi sasa Tashreeq ni mchezaji wa Borussia Dortmund.

Nchini Ujerumani alifahamika kama ‘diamond eyes’. Macho ya almasi. Alipewa jina hili kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuvitambua vipaji vya vijana wadogo.

Klabu nyingi zilimuhitaji. Bayern Munich ilimuhitaji sana. November 2017 alijiunga na klabu ya Arsenal akiziba nafasi iliyoachwa na Steven Rowley ambaye alikua skauti mkuu wa Arsenal tangu mwaka 1996.

Baada ya Steven Rowley kuondoka, Arsenal ihitataji mtu sahihi atakaye ‘fit’ vizuri kwenye nafasi aliyoiacha. Kumbuka Rowley alikua ‘master’ kwenye kazi. Arsenal ilisifika kuwa timu inayozalisha vijana wengi wenye vipaji halisi vya soka. Kazi kubwa ilifanywa na Steven Rowley. Alipoondoka akaja, Sven Mislintant ambaye ni ‘master’ pia kwenye kazi hii.

Lucas Torreira na Matteo Guendouzi ni wachezaji walioletwa Arsenal na huyu jamaa. Pierre-Emerick Aubameyang, Henrik Mikhtaryan, Konstantinos Mavropanos, Sokratis Papastathopoulos na Bernd Leno ni baadhi ya sajili zilizofanyika baada ya ushauri kutoka kwake.

Anatarajiwa kufanya mambo makubwa akiwa Arsenal pia kama ilivyokua kwa Steven Rowley. Alipokua anafanya mahojiano hivi karibuni alisema atafurahi kama akifanikiwa kumpata mchezaji mwenye akili ya Andres Iniesta.

Huyu ndiye Sven Mislintant. Jamaa iliyebeba mafanikio ya Borussia Dortmund kwa kipindi chote alichofanya kazi. Wachezaji aliowaleta kwa kiasi kikubwa waliisaidia Borussia Dortmund kushinda ubingwa wa ligi kuu nchini Ujerumani, mara mbili mfululizo mwaka 2011 na 2012. Mwaka 2013 Borussia Dortmund iliingia fainali ya UEFA Champions League pia. Sasa anafanya kazi kama skauti mkuu wa Arsenal
View attachment 991708

Sent using Jamii Forums mobile app

Msiwaige Monaco bana,

Mkiwa kama Monaco Arsenal itakuwa ile ile tuliyoifahamu

AHHAHHAHAHHAHAHA
 
Hapo umenena kijana, Manchester United sio ya Kocha Mourinho tena ni kocha mpya ambae amekuja kwa hatua nzito nzito. Kushinda hiyo mechi inabidi mcheze kama ile Arsenal iliyompiga Van Gaal 3-0 katika siku ile sio Arsenal tunayoijua
Kama umewafatilia man u kipimo halis kinaanzia kwa tot

Ukiangalia man u wanajipandia tu mbele , kwa tot ndio kipimo halis

Sent using Jamii Forums mobile app
 
138 Reactions
Reply
Back
Top Bottom