Arsenal (The Gunners) | Special Thread

UEFA hairuhusu timu yenye owner mmoja kucheza mashidhano yake!! Sasa inakuwaje RB leipzig na RB Salzburg zimeruhusiwa kushiriki UEFA kwa pamoja???

NB zote zinamilikiwa na Red Bull

Embu wataalam mtujuze
Ujerumani kuna kitu kinaitwa 50+1 ownership rule, ambapo mashabiki wanakua na nguvu zaidi kuhusu timu kuliko commercial investors,

Walichokifanya Redbulls kwenye timu ya Leipzig ni kubadilisha majority share holders na kwamba mashabiki wao ndio wenye timu then Redbulls ni second owner (kwa upande wa arsenal ni kama vile kroenke na Usmanov, kroenke ndio kama mashabiki alafu Usmanov ndio kama Redbulls) kitu ambacho uefa walikikubali.
 
Duh uko deep.... Nashukuru kwa maelezo yako murua mkuu
 
IMG_20180319_152131.jpeg
 
Nimekumbuka enzi za Wacha1 huyu mdau alilifanya hili jukwaa liwe active muda wote yaani amsha amsha za kutosha full mapicha picha,ama kweli jukwaa lilipambika likawa na mvuto kuliko majukwaa yote ya sports humu jamvini........aseeeeehhhhh
 
Tetesi

Arsenal na Chelsea wanatarajiwa kushindana katika jaribio la kumsajili kipa wa Atletico Madrid na raia wa Slovenia Jan Oblak, 25. (Sunday Express)
 
MSHAMBULIAJI wa Ujerumani, Mesut Ozil amemweka pabaya Andres Iniesta baada ya kumfanyia mambo makubwa kwenye mechi yao ya kirafiki.

Mshambuliaji huyo wa Arsenal, alifanya mambo makubwa na adimu na kutoa asisti katika mchezo uliopigwa huko Dusseldorf, Ujerumani na kumalizika kwa sare ya 1-1.

Ozil alikuwa akipokea mipira kwenye chaki akiwepo mchezaji huyo wa Hispania, inaonekana kwamba hawezi kumtoka, lakini alikuwa akimtoka hapo hapo.

Alikuwa akitoa mapende kwa miguu yote huku akimwacha Iniesta akiwa anahaha uwanjani.

Kwa upande wa Iniesta,naye alikuwa akifanya vitu vyake kwani alisaidia kutoa pasi kwa Rodrigo ambaye alifunga bao la mapema kabisa, dakika ya sita.

Ozil, amerejea kwenye klabu yake ya Arsenal baada ya kuondolewa kwenye mechi ijayo na Brazil. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid atakuwa na kikosi cha Gunners Aprili Mosi dhidi ya Stoke City huko Emirates.
 
138 Reactions
Reply
Back
Top Bottom