Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Ila arsenal MNA dharaurika.eti kuna jamaa anamuuliza mwenzie kwenye simu.vipi mandondocha yetu yanaendeleaje?
 
Ahahaa..,.. Huyu Mzee ni wa kumuondoa tu hata kama akisajiri akina nani.
Ila mashabiki wa arsenal mna mioyo migumu sana na ya uvumilivu.

Leo tayari hasira zenu kazipoza kwa kiwango kikubwa Mr.Wenger.

Sisi ngoja tujikongoje na OT yetu.
 
Hongereni wapendwa......mkapambane sasa angalau mwaka huu mpate cha kuwafuta machozi,all the best wana Wenger.
 
Arsene Wenger ameendeleza rekodi yake nzuri katika kombe la FA hatua ya nusu fainali kwa kushinda michezo 8 kati ya 11 na kufungwa michezo 3 sawa na 72.3% ya ushindi
Arsenal wamecheza mpaka mda wa ziada katika michezo 3 ya nusu fainali
2014 Vs Wigan
2015 Vs Reading
2017 Vs Manchester city
Alex Sanchez mpaka sasa amehusika katika upatikanaji wa magoli 13 katika michezo 13 ya FA
ameshinda magoli 7
ametoa pasi za magoli 6

Alex Sanchez ameendeleza rekodi yake ya kufunga katika uwanja wa Wembley katika michezo mitano aliocheza Wembley ameifungia magoli manne Arsenal na magoli mawili ameifungia timu yake ya taifa
 
IMG_2135.jpg

MOTM
IMG_2136.JPG

AW anaturudisha Wembley tena,thanks much mtu mzima.
 
Arsene Wenger ndie kocha pekee alieweza kumfunga Pep Guardiola akiwa Barcelona,Bayern Munich na Manchester City
99a5730ce1c628111f86775090c183d9.jpg
 
"Usicheze na Wenger wewe yule kocha sio mchezo "nimenukuu kauli ya shabiki mmoja kindakindaki wa arsenal baada ya ushindi wa jana.
 
Arsenal imeshinda michezo yake saba mfululizo katika uwanja wa Wembley

Arsenal imeandika historia kuwa timu ya kwanza kufuzu kwa mara 20 hatua ya fainali katika kombe la FA
6848f63ebb705569d6acfdbee18f5bc9.jpg
 
TETESI ZA USAJILI KUELEKEA MSIMU MPYA WA 2017/18
Rodrigo Fernandez ambaye ni wakala wa mchezaji Lucas Perez amekanusha habari zinazomuhusisha mteja wake za kuhitajika na Deportivo "habari hizo sio za kweli na atujafanya mazungumzo na timu yoyote ile kwa sasa,Perez kwa sasa amebakiza mkataba wa miaka mitatu na Arsenal.katika kipindi cha majira ya joto baada ya msimu kumalizika tuna weza kuanza mazungumzo na timu zitazo muhitaji kwa sasa tunafikilia zaid kuhusu arsenal" (Goal.com)

Marseille itajaribu kufanya usajili wa Olivier Giroud katika kipindi cha majira ya joto na wapo teyali kutoa dau lenye thamani ya £20m kama ada ya uhamisho wake (skysportstatto)

klabu mpya iliopanda daraja katika ligi kuu ya nchini uingeleza (EPL) kwa msimu mpya wa 2017/18 Brighton wameonyesha kumuhitaji winga wa arsenal Joel Campbell kwa mkopo.imeripotiwa na Futbol centro America ya kuwa Brighton wanataka kumrudisha Campbell nchini uingereza msimu ujao kwa mkopo ,Campbell ambae kwa sasa yupo kwa mkopo wa mda mrefu na klabu ya sporting Lisbon ya nchini ureno ambao utamalizika mwisho mwa msimu huu na ikiwa lisbon wataitaji kumbakiza itawapasa kulipa ada ya uhamisho wake wenye thamani ya £10m ambayo ilianishwa kwenye mkataba wako (readarsenal.com)
927baa2ec2de9d5adb18870b8bc5fdc7.jpg
4cf83059a42e48d49d9416e752d38daf.jpg
49d6fb904f1d9095234ed1611145243f.jpg
 
Arsenal wamethibitisha kurudi kwa Emirates Cup kwenye majira ya joto (kabla ya kuanza kwa msimu 2017/18).Sevilla,Benfica na RB Leipzing ni timu zitakazoshiriki
93529246fd1a313e6b920257000d800b.jpg
 
Arsenal wapo tayari kumlipa Mshahara wenye thamani ya £100,000 kwa wiki kiungo Mshambuliaji wake Oxlade Chamberlain ili kuendelea kumbakisha kwenye viunga vya Emirates. (Daily_Mirror)· Je unadhani anastahili kuendele kuitumikia arsenal?
122641b0a982975a5c7827327cb2653b.jpg
 
HT
Arsenal 0-0 Lei
Solid defence ni kitu wanachojivunia Lei City leo wana kaba kwa nidhamu sana wanajua udhaifu wetu wa kujazana kwenye box lao.
 
138 Reactions
Reply
Back
Top Bottom