Arobaini za ATCL zatimia kwa Waziri Kawambwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arobaini za ATCL zatimia kwa Waziri Kawambwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jan 30, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,433
  Likes Received: 5,688
  Trophy Points: 280
  Orobaini za ATCL zatimia kwa Waziri
  Stella Nyemenohi
  Daily News; Thursday,January 29, 2009 @21:15  Kamati ya wataalamu iliyopewa kazi ya kuchunguza chanzo cha matatizo ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), imewasilisha ripoti yake serikalini na kutoa mwanya kwa Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kutoa uamuzi kulingana na mapendekezo yaliyomo.

  Ingawa haikufahamika mara moja mapendekezo yaliyomo katika ripoti hiyo iliyokabidhiwa jana Dar es Salaam, lakini Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa alisema serikali ilikuwa ikiisubiri kwa hamu ripoti hiyo kwa ajili ya kuyatumia yaliyomo kutolea uamuzi unaolenga kuboresha kampuni hiyo.

  “Tulisuburi kwa hamu. Baada ya upembuzi wa kina, kazi yetu ya kuboresha ATCL itakuwa rahisi,” alisema Dk. Kawambwa na kusisitiza kuwa baada ya uchambuzi, watatafakari na kuchukua uamuzi uliopendekezwa ndani ya muda mfupi.

  Chini ya uenyekiti wa Profesa Idrissa Mshoro, kamati hiyo ilikuwa ikichunguza kwa kina, kubaini kwa ufasaha matatizo yanayoikabili ATCL na kutoa mapendekezo ya kutatua matatizo hayo. Waziri alisema ana imani mapendekezo yaliyotolewa hayajafungwa na kitu chochote kwa kuwa kamati hiyo siyo ya kichama na wala kiserikali, bali ni ya wataalamu na iliyokuwa huru katika uchunguzi wake.

  Alisema kamati hiyo ilipewa muda mfupi wa siku 21 kufanya kazi hiyo kutokana na dharura ya suala lenyewe la kutaka mapendekezo ya kitaalamu ili kuboresha huduma za kampuni hiyo. Timu ilitumia siku 28 badala ya ilizopewa kutokana na kile alichosema Waziri kwamba ni ugumu wa kazi yenyewe.

  Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Mshoro alisema watu 56 kutoka maeneo tofauti walihojiwa. Vile vile wamepitia nyaraka mbalimbali na kuzichambua. Wajumbe wa kamati hiyo ni Dk. Marcellina Chijoriga, Profesa Ibrahim Juma, Mtesigwa Maugo, Dk. Mussa Assad na Dk. Hamisi Kibola. Katika ripoti hiyo iliyokabidhiwa, Profesa Mshoro alikabidhi vitabu viwili; kimoja kikiwa cha ripoti husika na kingine kikihusisha nyaraka mbalimbali walizoona ni muhimu ziendane na ripoti hiyo
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,433
  Likes Received: 5,688
  Trophy Points: 280
  jamani hii ni habari njema nyingine wenye uwezo wa kupata data zilizopo humo ndani tujulisheni jamani tjaribu kuchangia hoja za ma proffesa wetu
   
 3. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nimefurahi sana kupata habari hizi njema kuwa ile timu ya wataalam imemaliza kazi na kuikabidhi kwa Mh Waziri. Ni matumaini yangu kuwa ripoti hiyo kama alivyosema Mh Waziri si ya kichama wala serikali basi ataonesha ujasiri wa kuiweka wazi ili wadau wote tuisome na kupata mwelekeo wa pamoja.
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kamati ya wataalamu wa Dr. shukuru Kawambwa iliyoongozwa na Prof. Mshoro haitakuja na jingine jipya juu ya masahibu ya kampuni ya ATCL. The injection of adequate working capital is a necessary condition for the rejuvenation of tha ailing Airline but the sufficiency condition is that ATCL should be manned by competent and professional personnel!! Once the necessary and sufficient conditions are met, ATCL will be up and running!! We all know this, we do not have to wait for a task force to tell us about this after spending our millions of hard earned tax payers money. I guess the minister wanted some justification to fire the management and their AMBASSADOR!!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Huko zamani niliwahi kusikia kisa cha timu ya wataalamu waliokusanywa na kampuni moja kutafuta jinsi ya kupunguza matumizi ya chumvi ya mezani. Baada ya utafiti wao uliochukua miezi kadhaa na kutumia karibu dola milioni moja timu hiyo ilitoa taarifa yao yenye juzuu tatu.

  Pendekezo lao la kwanza na kubwa lilikuwa: KUPUNGUZA MATUNDU YA KWENYE SALT SHAKERS!


  well..naweza kusema kilichopendekezwa kwa uhakika wa asilimia 99.9 na sihitaji kufanya utafiti!...... PUNGUZENI MATUNDU YA ATCL SHAKERS!
   
 6. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Teeh eteh hiii aaahha aaahh mmmh. Wee Mwanakijiji ni balaa sana. Jiandae kwa RB kutoka kituo cha Polisi Magomeni kwa kusababisha mtu kuvunjika mbavu kwa kucheka kutokana na huu ushauri wako. Only watu walio na Ph.F (Si Ph.D) katika masuala ya uchumi wanaweza kukuelewa kaka.
  You're really awesome.
   
Loading...