Armenia - Azerbaijan Military and Political Turmoil: Wizara ya Mambo ya Nje inatoa tamko gani juu ya usalama wa watanzania waishio katika nchi hizo?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Wizara ya mambo ya nje inatoa tamko gani juu ya usalama wa watanzania waishio Armenia pamoja na Azerbaijan?

Kuna mapigano makubwa ya kijeshi yanaendelea kwa siku ya 3 mfululizo leo baina ya nchi hizo mbili?

asdcdcdcdfdfdf.jpg

Mgogoro huu inasemekana ni wa muda wa karibu miongo minne. Lakini ulikuja kuwa mkubwa sana baada ya nchi hizi mbili kupata uhuru wao kamili miaka ya 1990 na kuendelea.

Inasemakana Russia inawaunga mkono Armenia huku Uturuki ikiwaunga mkono Azerbaijan. Jumapili hii ya juzi ya tarehe 27 September 2020 kumetokea kurushiana risasi, ndege kuangusha vifaru kulipuliwa mpakani mwa nchi mbili huku kisa cha haya ikiwa ni sehemu ya Nagorno-Karabakh inayogombaniwa na nchi hizi.

Wizara ya mambo ya nje inatoa tamko gani?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Wizara ya mambo ya nje inatoa tamko gani juu ya usalama wa watanzania waishio Armenia pamoja na Azerbaijan? Kuna mapigano makubwa ya kijeshi katika ya nchi hizo?

View attachment 1584584

Mgogoro huu inasemekana ni wa muda wa karibu miongo minne. Lakini ulikuja kuwa mkubwa sana baada ya nchi hizi mbili kupata uhuru wao kamili miaka ya 1990 na kuendelea.

Inasemakana Russia inawaunga mkono Armenia huku Uturuki ikiwaunga mkono Azerbaijan. Jumapili hii ya juzi ya tarehe 27 September 2020 kumetokea kurushiana risasi, ndege kuangusha vifaru kulipuliwa mpakani mwa nchi mbili huku kisa cha haya ikiwa ni sehemu ya Nagorno-Karabakh inayogombaniwa na nchi hizi.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Ngoja wanadiplomasia waje mzee baba. Mimi bado kilaza wa mambo haya.
 
nadhani swali hili wangeulizwa mabalozi wa huko nategemea watakuwa na cha kujibu
Sisi tunamuuliza Waziri kwa maana yeye ndiye Mbunge wetu na Top Political Figure ndani ya wizara anayepaswa kumhoji balozi wake. Balozi sio mbunge wetu.
 
Ubalozi unaohusika na eneo hilo hauwezi kutoa tamko au taarifa?
Waziri ndiye mbunge wetu ambaye sisi tumempigia kura ili aende kusimamia usalama pamoja na maslahi yetu. Sisi hatukumpigia kura balozi.

Sisi tunamsukuma Waziri ili na yeye amsukume Balozi wake huko Ulaya.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom