Armed Robbery sasa ina dhamana Tanzania

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,367
18,995
Kwa wale wanasheria wenzangu, mnakumbuka kesi ya Dickson Paulo Sanga, Rufaa ya madai Na.175 ya 2020 Mahakama ya Rufaa (DSM) ilitoa miezi 18 sheria kubadilishwa kwa ujambazi wa kutumia silaha ili iwe na dhamana, miezi hiyo 18 imeisha November, 2021, endapo kwa kipindi hicho sheria itakuwa haijabadilisha, kuanzia muda huo armed robbery itakuwa inadhaminika Mahakamani. Kwa maana hiyo, kuanzia sasa armed robbery ni bailable.

Ni wakati muafaka kwa mawakili kwenda kuwatoa wateja wetu mahakamani kwasababu sasa kosa ambalo halikuwa na dhamana, linadhaminika. Tuwatoe kabla ya christmass hii ili wakatafute pesa za sikukuu, watajua wenyewe watatafutaje.

Nimewawekea na kesi ya Dickson paulo sanga hapa chini.
 

Attachments

  • AG vs Dickson Paulo Sanga.pdf
    1.1 MB · Views: 37
Afadhali Mungu amenusuru likafungwa
but, mawakili wengi hawajastuka hili kwasababu hawafuatilii mapya ya sheria, ukiona wamejua hili, armed robbers wengi watapata dhamana na lazima waingie mtaani kutafuta pesa za sikukuuu, lazima pachafuke mtaani.
 
Aisee!. Omba isikutokee.

Yaani mtu aliyekushikisha bunduki kutaka kukutoa roho, akachukua hela zako za biashara then kesho na keshokutwa umkute mtaani, nakuapia nitakupiga bastola ya kichwa.

Bora wahujumu Uchumi wangepewa dhamana. Siyo unyang'anyi wa kutumia silaha.

Kupewa dhamana ni kuwapa uhuru wa kuendelea kupora tena na tena.

Imenikumbusha 2019, waliniibia zaidi ya 27 Million cash,Mashine na simu.

Kama siyo kuamua kuwaachia, wangenipasua ubongo.
 
Aisee!. Omba isikutokee.

Yaani mtu aliyekushikisha bunduki kutaka kukutoa roho, akachukua hela zako za biashara then kesho na keshokutwa umkute mtaani, nakuapia nitakupiga bastola ya kichwa...
kesi hiyo niliyoweka hapo ya Court of Appeal ilielekeza kwamba kama sheria itakuwa haijabadilishwa, kuanzia NOvember mwaka huu unyang'anyi wa kutumia silaha utakuwa na dhamana. hivyo kama mahakimu hawawaambii washitakiwa kuwa sasa wana dhamana, watakuwa wanakiuka wajibu wao tu. na kesi ikienda mara ya kwanza wanatakiwa kupewa dhamana kuanzia mwezi huu.
 
Sometimes kufuata Sheria hakutatupeleka popote, au Sasa ndio kila mtu atataka kuwa na silaha kujilinda
 
Sometimes kufuata Sheria hakutatupeleka popote, au Sasa ndio kila mtu atataka kuwa na silaha kujilinda
Mahakama pamoja na wanasheria wameona mtuhumiwa wa unyang'anyi wa kutumia silaha akinyimwa dhamana ni kitu kibaya, ananyimwa haki yake ya msingi ya kuwa huru na kutowekwa kizuizini, wakaamua hivyo. lakini majaji walioamua hivyo wana ulinzi wa polisi majumbani kwao, but wanasheria waliohamasisha hawana ulinzi. na ninaamni hawajawahi kuingiliwa majumbani kwao na majambazi. wanayasikia tu.
 
Back
Top Bottom