Ari, Kasi na Nguvu Mpya Zimedoda, Kilimo Kwanza jee kitafikia wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ari, Kasi na Nguvu Mpya Zimedoda, Kilimo Kwanza jee kitafikia wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Sep 4, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Ari Mpya, Kasi Mpya, Nguvu Mpya! Matokeo=Sifuri!

  Kilimo Kwanza, ndio wimbo mpya nao matokeo yake kuwa Sifuri!
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Sep 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ohh!...usinichekeshe miee!
  usisahau pia ahadi za starehe..Hiyo Ari mpya ilituhakikishia Taifa Stars kucheza final za World Cup - South Afrika. Sijui hilo deni litalipwa vipi maanake tuliondolea sijui round ya kwanza au ya pili tena na wachovu ile mbaya..
   
 3. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hii ndo kali kuliko zote. Kilimo kwanza na wakati wananchi wanaendelea kulima kwa jembe la mkono na tena kwa kutegemea mvua za msimu ambazo hazitabiriki maana hata wataalam wa hali ya hewa hawana uhakika na wanachokisema na vifaa ni vya miaka ileeee. Na mbaya zaidi hakuna MPANGO MKAKATI as they call it in goverment wa kuhakikisha haya yanatatuliwa. As usual the county of great propagandaz ilimradi siku zinasonga
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Mkuu Rev, ukitaka kujua hii ni sanaa just imagine serikali hata haizungumzii ni wapi tulikwama tukaanzia pale bali is just jumping in, ooh matrekta, ruzuku ya pembejeo nk.

  Lakini kilimo Tz ilishawahi kuwa sekta iliyokomaa kwelikweli kulikuwa na research centres ambazo ziliweza kugundua mbegu stahili za eneo husika, wataalam waliobobea na up to this date hakuna sekta yenye watu waliosoma mno Bongo kama kilimo you go to even some unrecognized institutes like say Kilimo Gairo, shirika la kilimol Uyole etc. na utakutana na PHd za kumwaga......... Ok so why we failed and we keep on failing? JK amefanya utafiti wa hili kabla ya kurukia kilimo kwanza???????

  Hii inanikumbusha mwaka jana nilikutana na mzee mmoja Mbeya akaniambia kilimo hakina maana. Nikamuuliza kwa nini? Akasema toka azaliwe hajawahi kuona bei ya mfuko wa mbolea kuzidi bei ya baiskeli. Na ofcourse watu walikuwa wanalima wanunue baiskeli. Sasa Kuna haja gani ya kulima wakati hela ya kulimia ekari moja ni zaidi ya baiskeli kumi???????????

  Anyway I am kinda busy lakini ntarudi kutoa ushuhuda thru self experience............. Kilimo kwanza???????????? what a joke?

  Sorry Kilimo kwanza imo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM? Maana of recent akina Mkamba kila wakiwa challenged jibu rahisi na la haraka ni hiyo haimo kwenye ilani ya CCM.

  TGIF
   
 5. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 910
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu umenikumbusha kitu, tuliambiwa kuwa Real Madrid wangekuja na kamati ya maandalizi ikaundwa! Mpaka sasa ahadi ni chali a.k.a kifo cha mende!
   
 6. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kasi na ari mpya ya kuendelea kuchota mali...
  Hivi mheshimiwa naye alipata zile nyumba walizopeana?
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Wakuu michango yenu inaleta maana kubwa kwangu. Tumekuwa hodari wa maneno kuliko vitendo. Mazao machache yaliyopo sasa ambayo yanalimwa kwa jembe la mkono mengi yanaishia kuharibika mikononi mwa wakulima.Kilimo kwanza kimeangaliwa katika mapana yote nikiwa na maana kulima kwa tija, ku add value kwenye mazao hayo ya kilimo na kuwa na masoko ya uhakika ndani na nje? Tusisahau pia suala zima la quality assuarance lazima liwepo kwa mazao tunayozalisha. Tumejiandaa vipi kwa hayo?

  Vinginevyo tukae kimya maana hatuna jipya...jipya litakuwa ni kuibua misemo isiyobeba maana halisi toka ndani ya mioyo yetu yenye kufanana na misemo ya nyimbo za taarabu.
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kilimo kwanza!!!!!!! halafu what next ie ......pili

  Anyway tanzania imekuwa ikiendeshwa na kilimo toka tumepata uhuru. Kilimo cha jembe la mkono ndicho kilichosomesha majority ya watanzania, mbolea hamna na kama ilikuwepo basi kidogo sana na wakati wote sikuwahi kusikia kuwa kuna njaa tanzania na au tunaagiza chakula toka nje.

  Tulisoma kuwa uchumi wa tanzania unatokana na chai, pamba, kahawa tumbaku ambayo in reality haikulimwa na settlers zao pekee lililolimwa na settlers ni mkonge na tumbaku kidigo sana, zao la mkonge na settlers wa tumbaku waliondoka baada ya azimio la Arusha na kufanya mazao hayo yaendeshwe na wananchi walalahoi na bado kilimo kiliendelea kuendesha nchi kwa biashara na chakula.

  Tunaposema leo kilimo kwanza naona kizunguzungu, labda ndio maana mwanakijiji na jembe lake amedisappear, look at theso called big four regions kilimo chao bado ni kilekile cha kizamani yule tajiri ni mwenye kambaku ( ng'ombe dume) na plau ya kizamani kwani ufi na zzk sasa hivi kwisha kazi.

  inakuja idea ya power tillers eti ndo solution na au kichocheo cha kilimo kwanza, mafundi tunao, mafuta tunayo vijijini do they need such advanced things bila hata kuwatayarisha. Ardhi wanayo jee serikali inaithamini ardhi wanaweza kuitumia kama collateral, kwa mfano serikali ilileta kitu kinaitwa lleseni za makazi ambayo walisema itakuwa kama title nyingine mpakaleo benki zinakataa leseni za makazi kama collateral.

  Lets go back to the drawing board and see how we can improve the lives of our poor, forgotten and neglected farmers we should ask them what they need to emancipate themselves na sio sisi kuwapa terminologies tamu ambazo kwao ni kizunguzungu.
   
 9. K

  Koba JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  lazima tukubali sio kila sekta ili iendelee serikali ndio imwage pesa,nafikiri swala la kilimo linaweza kuwa la binafsi kwa kutumia juhudi zao wenyewe...kuna ardhi ya kumwaga kwa hiyo lolote kwenye kilimo linawezekana,nchi kama marekani nafikiri uzalishaji mkubwa ni juhudi za watu binafsi ambao wako motivated na profit na sio serikali ingawaje good policy za kuongoza masoko zinawekwa na serikali lakini kusema serikali ianzie sifuri kuwainua wananchi hizo ni ndoto,watu wafanye kazi serikali itasaidia kidogo na itaweza kuona pa kuanzia lakini tuache ndoto za serikali...hamjifunzi baada ya wananchi kuanza kuacha kutegemea serikali kuhusu Elimu wanafunzi wanaoingia sekondari kwa mwaka wameongezeka kwa zaidi ya 10000% kutoka 1984 mpaka 2006,watu wafanye kazi kwa bidii na waelewe kilimo kina faida maana biashara ya chakula haiishi na masoko yapo maana TZ baado tunaagiza chakula kingi sana kutoka nje
   
 10. Violet

  Violet Member

  #10
  Sep 4, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tangu tupate uhuru hakuna kilimo cha kisasa, uchumi wetu unategemea misaada tuu
   
Loading...