ARE YOU TRUE TO YOURSELF...? Upo na Mpenzi wako kwasababu ipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ARE YOU TRUE TO YOURSELF...? Upo na Mpenzi wako kwasababu ipi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by AshaDii, Aug 20, 2012.

 1. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Habari wana JF,

  Kabla ya yoote naomba niwasalimu woote, wale tuliozoena tukututanapo hapa Jamvini, wale ambao ni wapya na wale wa zamani pia. It has been long kuja kujumuika hapa MMU hivo namshukuru Mungu na nafurahi kuwepo kwa mara nyingine kuweza share na nyie.

  Hii thread has been inspired by JF, marafiki wangu hapa na mtandao wenyewe - for ilinikaa akilini kuwa nisipokuwepo hapa jamvini nawa miss sana. Na kama nawa Miss then ina maana NAWAPENDA, Na kama nawapenda ni lazima kuna nasababu ya kuwapenda... Hivo sababu tuko MMU na virefu vyake vyajieleza nimeona bora iwe kwa Msingi wa Mapenzi. Hivo kurudi kwenye mada;

  Umewahi jiuliza upo na MPENZI/MWENZA wako kwa ajili gani?

  Mapenzi ni mchezo wa ajabu saana. Wanadamu hutaka awe na wa karibu wake hasa Mpenzi for the simple reason kuwa anapendwa na yeye kupenda pia. Ila as we grow up we learn the hard way… Kuwa mahusiano is not always about LOVE. Kwamba LOVE is just secondary to Relationships… na what is important ni Amani, Furaha na Contentment. Unaweza usiwe na LOVE katika mahusiano yako BUT ukawa na Amani kuliko hata walio katika Mapenzi ya dhati. Hii ni kwa wale wenye wapenzi whether wameoana or wapo pamoja… Kwa mda mrefu ama mfupi.

  Kwa mtazamo wangu yafuatayo ndio baadhi ya sababu
  ambazo mimi naona ambazo huwafanya watu wawe pamoja;


  UTEGEMEZI

  Upo nae kwa ajili yeye ndie anayekuweka mjini, unajuwa kuwa bila yeye maisha yako yatakuwa hayana muelekeo au hata kutokuwa na guaranteed secure future. Upo wise enough to know kuwa maisha hayakupi kile ambacho unataka na sio happiness is not only about being with the one you love… saa ingine hata Yule ambae you need anatosheleza.

  Utegemzezi upo wa ki-akili pia. Kuna watu wana bahati mbaya saana ya kuwa na low self esteem kiasi kwamba anahitaji mara kwa mara kuambiwa nini la kufanya na namna ya kufanya hilo jambo.

  VIHAMASISHI

  Hii ni zaidi kwa ajili ya circumstances… as in huko nyumba mlikuwa katika mahusiano ya kufurahia tu company then mkajikuta mko katika situations kama kupeana mimba both of you mwaamua kuwa pamoja. But wote mnajua hampendani kabisa.

  INSECURITY

  Hujiamini… hujitambui… na wala hujui bado. Na kama wajua basi huamini utambuzi wako. Unaona kana kwamba huyo mpenzi wako ni your lucky charm, hata kama unafanya kazi na una maendeleo hasa kama uliyapata ukiwa naye unaona kama vile bila yeye haitawezekana kuendelea. Unaona kama vile huwezi mpata mpenzi mwengine aliye bora kama huyo… aidha kimuonekano, ki maisha, ki maslahi, kimaendeleo n.k. Unaona kama vile kuwa nae ni bahati sana lasivyo utampata beneath huyo mtu.

  UFAHARI

  Hii mara nyingi hutegemea nafasi, jina, wasifu kwa mpenzi wako. Maybe ana jina kubwa… kazi nzuri… Maisha mazuri… anaheshimika katika jamii… demands respect and attention.. ako hot… anakubalika ki mvuto/hasa urembo na utanashati. Hii inakufanya uwe naye. Humpendi lakini unaona ni bora kuwa nae sababu wakisikia/ukionekana/ukijulikana upon a huyo mtu inakuletea sifa, kukujengea jina, kukuletea heshima katika jamii. Unajua kabisa humpendi ila anakufaa kuwa mpenzi wako katika macho ya jamii.

  KUKATA TAMAA

  Umehangaika katika ulimwengu wa mapenzi… umetafuta mtu ambae tokana na mtazamo wako anakufaa lakini hujapata. Kila mpenzi uliempata yeye alikuvunja moyo, nguvu na amani kwa njia moja ama nyingine. Unapata mtu ambae angalau ana mwelekeo… ana madhaifu but ya kibanadamu. Toka upo nae walau upande wa mapenzi kumekuwa afueni. Unaona ni bora uridhike na hata ikiwezekana uoane na huyo huyo ingawa watambua humpendi kidhati but kikawaida.

  GUNDI ASILIA

  Hii ipo sana kwa wale ambao ni wanandoa; yaani mtu na mwenza wake.. wamejijenga pamoja. Wana watoto, rasilimali na maisha yao yapo so tangled pamoja tayari. Lile wazo ama kitendo cha kutengana ni disruption ya maisha kwa kiasi kikubwa sana. Mara nyingi watoto ndio force kubwa… unaweza kuta mwatambua hampendani but you acknowledge na mwaheshimiana na mwatambua that is enough.

  ULILAZIMISHWA

  Aidha ulilazimishwa kuwa nae… au unaweza kuta ni wa kurithi. Kuna kabila na mila ambazo hadi leo inatakiwa utafutiwe mtu wa kuoana nae… labda katika ukoo ama kwa wakaribu wa familia. For instance dada kaolewa kazaa watoto wawili then anafariki na soln inaonekana ni bora aolewe mdogo wa marehemu. OR kaka anafariki then kaka ama mdog wa marehemu anaoa mke wa marehemu kwa njia na nia ya kurithi.

  COMPATIBILITY

  Hampendani, ila heshima kwa saana. Wote mmeweza na kufaulu katika ku compromise. Yale ambayo mwenzio hapendi umeweza epusha na wala hujaona tofauti yoyote with the justification kuwa sio ya msingi sana kuendelea na vivo hivo kwa mwenzio. Mmekutana tabia, maybe wote ni wacheshi/wapole, wote hupenda privacy yake mwenyewe na huheshimu ya mwenzie… vitu kama kufuatiliana, kuchunguzana, kushikiana simu, kupelelezana au kuchokonoana hakupo. Watu hawa mmoja wapo anaposafiri akakaa huko hata kwa kipindi kirefu mawazo kama kusalitiana hata hayawatembelei kichwani kwao (hata kama kweli wanafanya); hawa complicate maisha, kama hawapo pamoja simu mara moja or mbili kwa siku… more out of obligation than love. Hawa mmoja wao hata awe na mpenzi mwengine anajua kabisa hawezi kuwa as perfect as huyo alokuwa committed kwake.

  FED UP

  Yaani hapa hujali kuwa upon a nani as long as upon a mtu… mtu wa namna hii hata kama mwenza/mpenzi wake hayupo akaja mwengine ataona sawa tu sababu s/he does not give a damn who's at the opposite side.

  :A S-heart-2:L.O.V.E :A S-heart-2:

  Hapa niseme nini? In short kama yeye HAKUNAGA…. S/he is the one. And that is PERIOD!! Mapenzi kila mmoja ukimwambia aelezee atakuja na jibu lake, maelezo tofauti lakini at the end of the day yote yakibeba uzito wa jinsi gani mtu fulani katika maisha yake humfanya ajisikie raha, ajisikie tofauti, ajisikie unique, ajisikie vyovyote vile in the lines of what is best in the line of feelings...

  Ubaya tu wa haya mahusiano, ni rahisi sana kutodumu. In the long run kama Penzi lenu damu yake ya kuishi ni mapenzi ya dhati mliyonayo dhidi yenu; inapotokea yakanyauka, kila mmoja humuona mwenzie kama kero Fulani hivi…. Wapo wenye bahati zao na hudumu till death does them part.

  Fellow JF Members…. Are you true to yourself? Mpenzi ama mwenza ulie nae uko nae kwa ajili gani? Tafakari, ukiwa radhi unaweza kushare, ama unaweza toa sababu zingine ambazo zinapwaya hapa. Bila kusahau kama kuna ya ziada ambalo sijagusia, nitashukuru kupata ziada hio... Karibuni.


  Pamoja Saana with Love

  AshaDii


  P.S "I had missed you guys kwa saana"
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  karibu tena
   
 3. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ntakuja kumalizis baadae maana ni ndefu mno..Ila imekaa vizuri
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Long time no see...! Karibu tena...
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  AshaDii karibu sana jamvini. Mimi kwa upande wangu sijui bado sababu ya kuwa na mama ngina wangu zaidi ya kupenda.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Asante Boss, am glad you have already confirmed you are good.

  Mkuu, pole na hongera kwa kumaliza swaum, Asante kwa ukaribisho. Pamoja sana.

  Asulo mbona unaniangusha, mida hii si upo bed ndio mda wa kusoma soma kidogo? lol. Karibu tena...
   
 7. Taz

  Taz JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 305
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Aisee, karibu sana. We missed you bad!
   
 8. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Nashukuru Ndahani... Naamini wewe na familia ni wazima kabisa. Ila jibu lako siamini kabisa.. na sababu its late labda ni uchovu wa kazi, nitakuvumilia kesho naomba jibu bana! lol

  Asante kwa ukaribisho... pamoja saana.
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Taz it has been long broda, you good? Mie missed you too...
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  sio all is fair in love and war?
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Bora umeona mapema...nimechoka ila kifupi, hujafa hujaumbika.
   
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Acha mzaha Boss a kukwepa maswali... hebu jibu why are you with each of them?
   
 13. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Pole Ndahani, basi pumzika kama inshallah utabahatika kupata jibu nitashukuru nikilipata.... Kwa hio hapa utaendelea kutusoama ama unaenda kulala?
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Karibu sana ADii,

  Umesalimika huko ulikofichwa??

  Tulisema sana hapa (wakati ume-hibernate) kuwa maslahi yanabeba sehemu kubwa katika kuimarisha mahusiano!!

  CLICK HERE


  By the way, mie si muumini sana wa mahusiano (especially ndoa) yaliyosimama kwenye msingi wa LOVE!!

  Babu DC!!
   
 15. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Mzee DC,

  Nimesalimika kabisa mzee wangu, na nipo salama. Nimeona huo mjadala.. worth passing by, naahidi kesho kama tutajaaliwa kuamka salama nitapitia na kuweka senti zangu pale. Naamini uko salama kabisa pamoja na familia... Na Asante kwa ukaribisho.. Pamoja saana.
   
 16. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Fade up au fed up?
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Nasoma...kesho asubuhi ntakuwa na kuongea.
   
 18. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #18
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Bwa'Nchuchu mzima wewe? hebu nisaidie kwa kuenda google ipi ipo rite, maana mie hapa sina dictionary na English kwa kiasi fulani sipo fluent kivile... hivi hapo ni ipi ni ipi? ni edit kuweka hio?
   
 19. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Miye mzima wa afya!

  Sina hakika ulikuwa unamaanisha nini hasa. Kama ulimaanisha ile hali ya mtu kuchoka na mizengwe mizengwe basi ni 'fed up'.
   
 20. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  None of the above. lol.
  Alter, it is so good to have you back, I was feeling amputated...
   
Loading...