are we this Dull, bado week 2 kabla ya uchaguzi ndio unaleta grader mtaani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

are we this Dull, bado week 2 kabla ya uchaguzi ndio unaleta grader mtaani?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by bang, Oct 24, 2010.

 1. b

  bang New Member

  #1
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Roho inaniuma mno kuona ni jinsi gani baadhi ya watanzania wenzetu especially walioko madarakani wanavyotufanya wananchi wajinga na tusio na uelewa wowote.

  - Hivi ni kweli bado week 2 kabla ya uchaguzi ndio unaleta grader kurekebisha barabara ambayo for the last 5 years, ulikua unaipita barabara hio hio kama huioni? Hii ni Keko Toroli karibu na soko kuu la keko, vile vile barabara ya chang'ombe TCC

  - hivi ni kweli bado siku 11 kabla ya uchaguzi ndio unaleta kijiko na malori busy kuanza kuchota na kuchimba mchanga kwa ajili ya ujenzi wa daraja. kweli hii ni akili? hii ni Mwisho wa lami njia ya kwenda Ulongoni B.

  Hakuna kitu kibaya duniani kama kumfanya mwenzio mjinga angali anajijua kuwa unamwona mjinga. Hebu nyie wagombea acheni ujinga huu kama mlishindwa kufanya mambo katika muda wenu basi waachieni wenzetu wafanye kwa maendeleo ya Taifa na sio kuvimbiana utafikiri panya wa jalalani.

  Hii inaonyesha wazi ubabaishaji wa hawa viongozi wanaotaka kurudi tena madarakani, kama kweli walikua na nia na uwezo wanaotaka kuuonyesha sasa kwanini hawakufanya kipindi hicho chote cha miaka 5 iliopita?
   
 2. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Dawa mujarabu
  Mwalimu Nyerere alijaribu kutafuta dawa ya kunywesha wahujumu uchumi lakini akafanikiwa kiasi; baadaye wakaja kuhujumu nia safi ya Rais Mwinyi kulegeza masharti ya kiuchumi, wakamnasa Mkapa na sasa Kikwete hawezi kufurukuta.
  Kwa kuwa imejulikana mafisadi wamo ndani ya CCM na ndio wanaendesha serikali, dawa ni kung’oa mizizi ya ufisadi—kuiondoa CCM ili kiingie chama kingine ambacho hakitakomoa wananchi wala kuhujumu afya zao na elimu ya watoto wao.
  Sababu nyingine ya kuing’oa CCM ni kutokana na Mtendaji Mkuu, Yussuf Makamba kukiri wazi kwamba wagombea wote wa CCM wametoa rushwa kwa kuzidiana dau. Jamii inataka ushahidi upi zaidi ya huo?

  Gazeti Mwanahalisi
   
Loading...