Are we a Police state where are militaries

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,930
3,803
Kuna nchi duniani hazina jeshi zaidi ya polisi,fire fighters and serikali na wanaenda vizuri tu.

Kwa Zanzibar kama una ndugu polisi au mwanajeshi basi hata ukiguswa inakuwa rahisi mambo yako kusawazishwa na kuachiwa,
Kisa kimoja mbali ya kile cha JKU kikosi cha SMZ kumkamata au kumeka polisi wa usalama barabarani ,kilichotokea kinajulikana.

Kisa kingine cha zamani kidogo hiki kilihusisha JWTZ na Polisi wote hawa ni vikosi vya Serikali ya Muungano (SMT),polisi walimkamata mjeshi mmoja maeneo ya Kiembe Samaki, kwa ndani ipo kambi ya jeshi nyuma ya aiport kama sikosei.

Polisi wakampeleka mjeshi makao makuu yao maarufu Muwembe Madema habari kutoka kwa raia wema zikawafika majeshi kituoni kwao kuwa fulani amekamatwa na amepelekwa madema kilichotokea ni wajeshi wakiwa wapo ful nondo wakaingia kituo cha madema kwanza wakakizunguluka kama mala mbili ya tatu wakaingia counter na kusema tunamtaka mtu wetu bila ya suali lolote lile wala ucheleweshaji la si hivyo kitanuka,aliekuwepo kituoni hakuwa na la kufanya alipiga simu na akawakabidhi watu mtu wao,jamaa hao wakaondoka nae.

Ndio nikasema kama huna ndugu au jamaa utapata shida na kuwa hakuna wa kukusikiliza haswa hapa Zanzibar,SIjui upande wa Tanganyika kama hayo ya kutoleana uvivu kwa vyombo hivi yapo ?

Juzi kwenye uchaguzi yupo mtu alipigwa kiasi na polisi ila ikajulikana ni ndugu na polisi ambae kituo chake kipo Mkoani Pemba,klipu iliwahi kurushwa kwenye mitandao nae aliachiwa ila alikuwa keshaumizwa kwa kiasi fulani,nikajisemea kama angeuliwa huyu kaka mtu angekubali ?

Je, wananchi nao wakiona hatuna wa kutusaidia ni kila mtu kivyakevyake ,si nchi itakuwa haina tena uslama raia wanawindana na polisi?

CCM mnaipeleka nchi kubaya kwa tamaa zenu,haya mambo mwisho yatawageukia,wananchi hawatakubali kuuliwa kama mbwa wenye vichaa na wao watataka kulipiza visasi kila mtu kwa wakati wake yaani ni ile ya liwalo na liwe ndugu yangu ameuliwa na polisi na mimi kumuuwa polisi ni haki yangu.

Je kuna haja ya kufika huko kote,maana watanzania tulivyohusiana upo kama mizizi,inawezekana jamaa yako wa damu ni usalama wa taifa,ni jeshi ni polisi akisikia umeuliwa kishenzi kwa mambo ya kisiasa unafikiri atakubali yaishe ?

CCM lawama ni zenu na haziepukiki huko tunakotoka haya tuyaonayo hayakuwepo na chaguzi zilikuwepo hizohizo za kuibiana lakini hukusikia watu kuuliwa au kupigwa mapanga au tuseme Zanzibar ndio inasababisha Tanzania nzima kutaka kukoseshwa misaada,tusijidanganye leo hii mafuta yakizuiwa kuingia Tanzania misafara ya waheshimiwa itapanda punda ?

TUFANYENI CHAGUZI ZISIZO NA mAUAJI HATA YA MDUDU. Hata kama kutafanyika wizi wa matokeo kura lakini kuuwa iwe mwiko.
 
Back
Top Bottom