Ardhi Yetu? - Kwanini tunawakubalia wengine isipokuwa wa Afrika ya Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ardhi Yetu? - Kwanini tunawakubalia wengine isipokuwa wa Afrika ya Mashariki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 13, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Mojawapo ya mambo ambayo Watanzania tunaonekana kutokuwa na msimamo wa ukweli ni suala la ardhi na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Wapo watu wanaoshangiilia kuwa TZ imeweka ngumu na kuzuia ardhi yetu kuja kuchukuliwa na Wakenya baadaye na hivyo kufanya ardhi kuwa mojawapo ya hoja nzito zinazochelewesha kuundwa kwa shirikisho la AM. Watu wanaona vibaya sana kwa Wakenya, Waganda, Warundi na Wanyarwanda kuja kupata ardhi yetu na wengi wanafanya hivi kwa uzalendo. Hata Sitta anapongezwa kwa "kupigania maslahi ya nchi" pale alipoweka ngumu kiasi cha kulazimizha kuondolewa kipengele cha suala la ardhi kwenye mazungumzo ya kuelekea shirikisho.

  Lakini kinachonishangaza - na sijui kama wengine wamekiona - ni kuwa wakati hatutaki Waafrika wenzetu na majirani zetu kuhusiana hadi kwenye masuala ya ardhi tunaendelea kugawa maeneo makubwa kwa makampuni makubwa ya Kimarekani, Kichina, Uarabuni, Indonesia na Malasyia kwa ajili ya kilimo cha mazao ya mafuta na ya chakula kwa ajili ya nchi zao. Najiuliza, hivi kwanini tunaamini kuwa maslahi yetu ya ardhi yamefungamana na ya nchi hizo za mbali lakini nchi hizi majirani zetu hatutaki kusikia? Hivi ni kweli tunaamini Indonesia, Malaysia, China, Qatar na Marekani ndio wana maslahi sana na sisi kuliko watu ambao njaa ikija kwao inatugusa na sisi au sisi tukiguswa na wao wanaguswa?

  Au chuki dhidi ya Wakenya (ambao tuna trade nao zaidi kuliko karibu nchi nyingine yeyote) imetufanya tushindwe hata kufikiria kuwa hatuko consistent kwenye hili suala la ardhi? Kwanini Sitta asituambioe kwanini tunagawa ardhi kwa mashirika ya mbali na siyo kwa Wakenya au majirani? Kama suala ni "ardhi' kama watu wanavyotaka kutuaminisha kwanini tusipige marufuku kugawa ardhi kwa watu wa nje wote - bila kujali kama wako Asia, Marekani au Ulaya! Kama ni Ardhi yetu basi tuwakatalie wote au tuna tatizo jingine na majirani zetu ambalo hatuna na hizo nchi nyingine zisizo za Kiafrika?
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  kuna chuki kubwa sana kwa watanzania dhidi ya wakenya'hujawi kumwona mtu ananunua kwa mhindi na kuacha kununua kwa mtanzania mwenzake?'mimi binafsi napendelea hayo makampuni makubwa yakodishiwe ardhi yetu na kupewa masharti ya kutoa ajira kwa watanzania'hii ardhi ni mali yetu vizazi vijavyo'kama wakenya walishamaliza ardhi yote sasa wanataka kuja kichukua ya kwetu hatukubali'tutatumia ardhi hii kwa biashara na sio kuwapa wakenya iwe ya kwao'itakuwa ni makosa makubwa sana
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hoja ni rahisi tu, hao wageni wengine ni rahisi kuwafahamu kwa muonekano wao na siku tukitaka kuwango'a ni rahisi tu na ardhi wanaikodisha kama wawekezaji, whether kihalali au la. kwa hawa 'majirani' zetu wao wanataka haki sawa na sisi wazalendo ktk taratibu za kumiliki ardhi, kwa gia ya shirikisho spirit na free-movement and settlement, kitu ambacho hakuna mzalendo wa tz anaeweza kukubaliana nacho. Kama wageni 'majirani' wanataka kukodi hiyo ardhi kama wawekezaji sidhani kama wamezuiwa, milango iko wazi. Bottomline.
   
 4. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,086
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Mkuu MMK kama kawaida yako na topiki zako za kizushi lakini poa tuu...

  Ni kwamba tunachokipinga siyo wakenya bali tunataka sheria zitakazo linda maslahi yetu, iwe madini, ardhi na mailasili zote. Binafsi napinga kuona wanyonyaji wa republicans wakipewa ardhi bila kuwa na sheria madhubiti ya kuilinda kwasababu ni walafi wakubwa na hawana huruma hata kwa watu wao wenyewe sembuse masikini wa kitanzania?

  Suala la wakenya linaleta hisia zaidi kwasababu inaonekana wao wanataka kuja kama wajomba kwa mgongo wa usharika wa Afroka mashariki.
   
 5. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  We don need our land 2 be confiscated by Nyang'au..
   
 6. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,512
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Watanzania kigeugeu
   
 7. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  nadhani hata wakenya pia wanamiliki maeneo makubwa sana pale Arusha,jaribu kufanya uchunguzi utagundua hilo

  nadhani pia ule uhisani ndio unaotuumiza,kwani tunalazimika kuwapa maeneo hawa wamarekani na wengine ni kwa ajili ya kulinda zile pesa tunazopewa na hawa wafadhiri

  lakini tungeweza kusimama wenyewe na kuitumia hii mali asili ya ardhi vyema ktk kuzalisha mazao na kupambana na njaa inayotusumbua kilakukicha
   
 8. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  MMK nilisema haya pia katika mchango wangu wa wale waliopendekeza maandamano kupongeza serikali kwa kuzuia ardhi kwa wanaAfrika mashariki, wakati hawajafanya hivyo kuishinikiza nchi kurudisha ardhi inayoendelea kuigawa kwa malaki ya ekari kwa hao uliwataja hapo juu. Haiingii akilini kuwazuia wenzetu tuliogawanywa nao na mipaka iliyowekwa na hao hao wanaopewa ardhi kwa malaki, wakati njaa na kila dhiki katika ukanda huu tunashiriki pamoja. Nilikwenda mbali na kuhiji, Mkenya na Mrundi akiwekeza Tanzania, inakuwa rahisi kwa yeye kupafanya kuwa nyumbani kwake kama vile ambavyo hadi leo wapo wengi. Ni maelfu ya warundi, wanyaruanda, wakongo, waganda n.k wanaishi na kuitambua Tanzania kama nchi na nyumbani kwao, lkn sijui ni Wamarekani wangapi au Wakorea wangapi leo wanajiona wao kuwa ni Watanzania.

  Kimsingi, huu ni ubaguzi mbaya, kwani mwisho wa siku hakuna mantiki ya Mchaga kumiliki aridhi Mtwara, wakati Mmakonde wa Mtwara anashabihiana sana na Mmakonde wa Msumbiji? huu ni mfano tu.

  Kinachotusumbua Tanzania na hasa serikali yetu, ni hofu ya hatua za kasi wanazopiga wenzetu wa Afrika mashariki hasa kutilia maanani uwezo wao wa kibishara na kielimu walionao kulinganisha na Mtaji wa serikali ccm (Waache Watanzania waendelee kuwa wajinga, ili iwe rahisi kututawala), sasa linapovuka mipaka wanajigundua kuwa hata wao hawataweza tena kuvuma.

  Ni vyema tukawa na sera ya ardhi inayoeleweka na isyokuwa ya kibaguzi. Kama kuna haja ya kuwekeza kwenye kilimo kwanza tuanze na chakula ambacho kitaondoa njaa katika eneo letu la Afrika mashariki na afrika kwa ujumla kabla ya kukimbilia kilimo cha mafuta.

  Unaweza kujiuliza suala la kijinga, je hayo mazao yawe ya chakula au mafuta kutoka kwenye mashamba ya mabwenyenye yatatumika Afika? Je, leo gesi inayozalishwa Tanzania, inatumiaka kama nishati ya kupikia kwa Watanzania (Labda, kama Oryx ni songosongo)?
   
 9. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu unajua kuna kitu kimoja tu kinatusumbua kwenye hili,hao wamarekani na wakorea wamekodi hiyo ardhi na wakati wowote mkataba unaweza kusitishwa,kwa wakenya wanataka waichukue iwe yao milele,sasa watoto wetu itakuwaje?watarithi nini?tutakuwa tumefanya makosa makubwa sana,tatizo lenu nyie wengi humu sio raia wa nchi hii,mmeishi hapa miaka mingi na kupewa uraia uchwara wa rushwa,tuachieni tuamue kuhusu nchi yetu
   
 10. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2011
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Soma hii repoti hapa chini :

  Angalizo: Mambo ya 'double standard' kwenye masuala nyeti ..nahisi pia harufu ya rushwa na sheria mbovu mbovu za uwekezaji ambazo zimesimamia katika mambo ya kudesa (copy and paste), na kuamini kila kitu kutoka benki ya dunia ni kizuri kwa nchi bila ya kukichanganua kwa kina na kupima mazuri na mabaya yake:

  Source: http://www.eaffu.org/go/downloads/Kiriro%20Presentation%20AFDB%20meeting%20on%20Land%20and%20Policy%20Initiative%20Lisbon%20June%202011.pdf
   
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Tusitoe majibu mepesi yaliyojaa ushabiki wa kisiasa kama ilivyo kawaida yetu. Mimi naamini kama tungekuwa na sera nzuri ya ardhi na tukaweka utaratibu mzuri ambako majirani zetu watapata ardhi hakuna sababu ya kuogopa. Tusiendekeze watawala walioshindwa,wanaoishi kwa hofu.
   
 12. N

  Nakei Member

  #12
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Watanzania wengi hatujui matumizi ya ardhi, tuwape wakulima wa nje ambao ni wasomi, wasomi wetu wanawinda kazi za maofisini na wakulima wetu vijijini wanafanya kazi nusu saa kwa siku then wanapumzika muda wote kwenye mikeka. wengine mto unapita karibu na shamba yeye anasubiri mvua.
   
 13. fige

  fige JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo letu kubwa kwa majirani na marafiki zetu ni moja tu.Kwamba urafiki wetu unategemea sana tulicho nacho sisi na si kushea tulivyo navyo wote
   
 14. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  MM hujawa mkweli pengine makusudi,
  Kenya ni moja ya nchi zilizowekeza TZ na serious investors toka Kenya wanamiliki ardhi kubwa tu, kama sikosei kuna mashamba makubwa ya chai na misitu wanamiliki kule Iringa, sijuhi kwa nini hilo hujalisema.
  Nchi za EAC wakija kama wawekezaji hata bila mkataba mpya ardhi wanapata.

  Pia kumbuka Kenya unaowatetea nao ardhi yao wamewamilikisha Wa-UK na mataifa mengine, tena wana ardhi kubwa sana sana mpaka wananchi huwa wanalalamika, wanasiasa waliwadanganya katiba mpya ikija basi hiyo ardhi watarudishiwa, mpaka sasa sijasikia kitu.
  Wanachokataa waTZ ni wakulima maskini wa EAC kuja kuchukua ardhi kwa manufaa yao na si manufaa ya kitaifa kama tunavotegemea wawekezaji wafanye.
  Ok na kama wakija wakachukua ardhi yetu sisi tupate nini kwao?
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Wakenya iko janja nyingi. Ila haina maana sisi tumepeleka likizo fikra zetu. Maana akija mthungu, vyose vyake kama enzi zile za machief
   
 16. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  MM, that's a good and valid question. Thanks for being in same wave thinking.

  Everyone but EAC, particularly Kenya. As far as I know, I consider Rwanda then Uganda as most "potent" allies. I reserve the details till when time is ripe.

  As for current EAC situation, I always puke when see people said one member has some so and so interest.....as if the rest don't have or something. The fact is each member has self-interest and want to forster it best in the EAC....it is not a community of holy angel states.

  And Why, WHY Tz should keep doing what she doesn't believe in? Is it called hypocrites or intelligence?
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Bila ya sisi kuacha domo kaya na kuanza kuchapa kazi wageni kutoka kila mahali watatutawala kiuchumi kwa sababu dunia haina subira na mzembe...........
   
 18. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  In a long run .... Hatasalimika yeyote ...awe kutoka sehemu yeyote duniani au afrika ya mashariki!! WHY? Simply ARDHI NI YETU na Siyao!! HAKIKA! Wasidangayike!!! au wasidanganywe na FISADI yeote kwa sasa!!! Finally it will not work for a foreigner!
   
 19. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Kuna watu wana ego zao & bifu zao, na maslahi za hao wakubwa zaidi wa dunia.... sasa wamezi-transform into national policies...ni hatari sana.
   
 20. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #20
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  MMK Thanks for useful post.
  Mji mpya hizo faida za wawekezaji wengi sana tulionao kwa zaidi ya miaka 10 iko wapi? Hakuna.
  Mimi nadhani heri hao wakulima maskini ( as you call them) ambao wakija wanaweza kukaa meza mmoja na mimi na wewe ili tufanye biashara/kilimo pamoja. Hapo ndo faida ya kitaifa inapatikana.
  Kwa maoni yangu, Tatizo kubwa la Tanzania ni sera dhaifu sana inayotokana na viongozi subjective badala ya kuwa objective wakati wa kuziunda. Sera na Sheria zikiwa safi tusingekuwa na matatizo yote haya. Tusingekuwa na cha mkenya wala mmarekani.
   
Loading...