Ardhi ya Tanzania: Kama kanzu ya Mwarabu

KAUDO

Senior Member
Aug 10, 2011
138
67
Kadri serikali ilivyowakumbatia waporaji wa rasilimali.

Ukiwa na hela zako ni rahisi kumiliki mahekta ya ardhi kama unavyoweza kununua kanzu dukani. Rejea Loliondo, Kilosa, Ranchi za Misenyi na hapo ulipo tayari pameuzwa.

Yaani kwa jinsi walivyolaaniwa wameuza hata 'mboga' ya ziwa Victoria.
 
mulima kilimanjaro si mda mrefu nao utabinafsishwa kwasababu serikali imeshindwa kuuendesha.inapata hasara.tunataka mlima ujiendeshe kwa faida.mtafurahi wenyewe.makofi tafadhali.mia
 
Mbarali muwekezaji kajiongezea shamba kwa kuingilia maeneo ya vijiji,muwekezaji mwenyewe hana uwezo hata wa kuendeleza shamba alilouziwa,amebakia ku kodisha vipande vipande vya wananchi walewale walionyang'anywa akapewa yeye...rukwa huko watu 154,000 wamehamishwa bila ridhaa yao kupisha muwekezaji wa biofuel...tunapoelekea ni kukatana mapanga ndio serekali itaelewa uonevu wa namna hii hatuutaki
 
Baba wa Nation aliwahi kuwatabiria "mkiendelea hivi mtabinafsisha hata magereza" maana wao kila kilicho mbele yao wabinafsisha on Mahakama ya Rufaa tayari ishapigwa bei kwa jamaa aliye muhonga suti tano mkwele' kule london
 
Ukifikiria na kuangalia unaweza changanyikiwa kabisa na kuwa mwenda wazimu!walaaniwe wote watumiao rasilimali za tanzania kwa matumbo na manufaa yao
 
Hiyo ndo inaitwa hari nguvu na kazi mpya na mtaipenda wenyewe
 
Mbarali muwekezaji kajiongezea shamba kwa kuingilia maeneo ya vijiji,muwekezaji mwenyewe hana uwezo hata wa kuendeleza shamba alilouziwa,amebakia ku kodisha vipande vipande vya wananchi walewale walionyang'anywa akapewa yeye...rukwa huko watu 154,000 wamehamishwa bila ridhaa yao kupisha muwekezaji wa biofuel...tunapoelekea ni kukatana mapanga ndio serekali itaelewa uonevu wa namna hii hatuutaki

Wabongo bwana!! sasa kinachowashangaza au wa kuwatia ghadhabu ni nini hasa wakati mlishaambiwa na mama Tibaijuka kwamba ni asilimia 10 tu ya Ardhi ya Tanzania ndiyo imepimwa kisheria. Maana yake ukichukua mikoa yote ya Tanzania hakuna hata mkoa mmoja ambao wote umeshapimwa, kwa maana hiyo kisheria sehemu kubwa ya Ardhi ya Tanzania haina mwenyewe bali iko mikononi mwa serikali. kwenye kila mkoa ni asilmia 10 ndiyo imepimwa tena na kwingine ni chini ya hizo asilimia 10, kwa mfano ni mikoa ya kusini na mikoa ya kanda ya ziwa na Rukwa na Katavi.

Sadaka lawe. Amina! Kipapatio. cha Kuku! kuku gani.Mweupe! Mwenye kupata. Apate! Mwenye Kukosa. Akose!!
 
niwawambia ata kule iringa mashamba ya chai aliyopewa malikia eka 500 watafiti wanasema chini kuna madini shala la bibi hili we ukiwa na pesa ata wilaya nzima unaweza kununua
 
kamanda%20polisi%20mkoa%20wa%20dar%20charles(2).jpg

Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyel


Mapambano yaliyoanzishwa jana na wanaosemekana kuwa ni wavamizi wa ardhi katika maeneo ya Nakasangwe na vitongoji vyake, katika kata ya Wazo, wilaya ya Kinondoni dhidi ya Jeshi la Polisi likiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Jordan Rugimbana, na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyel, yaliishia kwa kutiwa mbaroni zaidi ya wavamizi 15 na huku wengine wakijeruhiwa vibaya.

Mapigano hayo yaliyokuwa kama picha ya sinema yalianzishwa na wakazi wa hao baada ya kuitana kwa njia ya kupigiana filimbi na kupuliza pembe za ng’ombe, ambako wakazi karibu 300 wa vitongoji vya Nakasangwe, Kaza Roho na Mbopo walijitokeza wakiwa na silaha za jadi kama mapanga, mikuki, mishale, shoka na zinginezo kukabiliana na Jeshi la Polisi lililokuwa na silaha na vifaa kama magreda kwa lengo la kulizuia lisiendeshe operesheni ya kubomoa nyumba zilizokuwa zimejengwa kwenye maeneo yanayomilikiwa na wakazi wengine.

Hata hivyo, nguvu hiyo ya wakazi waliokuwa wamedhamiria kulizuia Jeshi hilo ilizimwa baada ya mapambano ya karibu saa nzima kwa Jeshi la Polisi kuwasambaratisha kwa mabomu ya machozi na wakajikuta wakikimbia hovyo na kuacha baadhi yao wakikamatwa na kutoa njia kwa jeshi hilo kuingiza magreda na kubomoa nyumba hizo.

Akizungumza na NIPASHE kwenye eneo la tukio, Rugimbana alisema wameamua kuendesha operesheni hiyo kama njia ya kutekeleza maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam ambayo imeagiza kwamba, maeneo yote ya watu yaliyovamiwa yanapaswa kurejeshwa kwa wamiliki halali mara moja.

“Na kwa kuwa Kinondoni ndiyo kinara wa tatizo hili, ndiyo maana Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ikaagiza kuwa operesheni hii ianzie huku Kinondoni, hasa sehemu hii ya Nakasangwe na vitongoji vyake ambayo ndiyo ina tatizo kubwa la wavamizi, ambao walikuja kuchukua maeneo ya watu na kujenga nyumba zao na mengine wakiwauzia wananchi wengine, ambao walijenga nyumba zao kama unavyoziona,” alisema.

Rugimbana alisema kibaya zaidi ni kuwa wavamizi hao wengi wao kila wamiliki halali wa maeneo hayo walipokwenda kwa ajili ya kutembelea nyumba walizojenga au mashamba yao, walikuwa wakiitana na kuwashambulia, hali iliyosababisha waumizwe na wengine wakiishia kubakwa.

Alisema eneo hilo na hasa kitongoji cha Kaza Roho kilikuwa kama hakina sheria kwa kuwa kila aliyefika bila kufahamika, alikuwa akiishia kupigwa na kujeruhiwa vibaya.

“Zoezi hili ni la kudumu, na mkoa umeagiza kuwa wale ambao tayari maeneo yao yalikuwa yamevamiwa kabla waende kwenye mabaraza ya ardhi na tayari huko tuna amri karibu saba zinazoelekeza wavamizi waondolewe na amri hizo tutaziingiza kwenye zoezi hili.

Lakini kwa wavamizi wapya kama hawa wa Nakasangwe, tumeamua tusitishe uvamizi wao na mwingine wowote ule mpya utakaotokea na ndiyo maana ya operesheni hii,” alisema.

KENYELA ANENA


Kamanda Kenyela alisema timu nzima chini ya uongozi wa Mkuu wa Wilaya ilifika katika maeneo hayo saa mbili asubuhi ikitokea katika eneo la kukutania lililokuwa katika Kituo cha Polisi Wazo.

Alisema, timu hiyo iliyokuwa imesheheni magari zaidi ya 10 ya polisi wa Kuzuia Ghasia (FFU) aina ya Toyota na Land Rover Defender, karandinga moja lenye namba STH 2508, kenta, magreda manne yenye namba T 578 BNH, T 213 BGQ, T 509 BSS na SM 8611, gari la wagonjwa pamoja na magari ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ya wilaya, iliwasili katika kitongoji cha Kaza Roho na kukutana na ‘wakazi wavamizi’ waliokuwa tayari wamekaa kimapambano kwa kuwa walikuwa na silaha za jadi.

“Mara tulipofika walianza kutushambulia kwa kurusha mishale, mikuki, mashoka na mapanga. Tulijibu mapigo kwa kuwavurumishia mabomu ya machozi na hatimaye tuliwasambaratisha. Baada ya hapo ndipo tuliingia na kuanza kazi ya kubomoa nyumba walizojenga katika maeneo ya watu ili kutekeleza agizo la serikali,” alisema.

Alisema mbali na silaha walizokuwa nazo, wavamizi vile vile waliweza kutega mbao zilizokuwa na misumari kwa ili kuzuia magari ya polisi kupita na kwamba pamoja na kuwasambaratisha, walifaulu pia kuwakamata baadhi yao wakiwa na bangi pamoja na gongo.

Alipoulizwa kwa nini waliwashtukiza wakazi hao bila ya kuwapa taarifa ili waondoke kwa amani, alisema serikali ya mkoa, wilaya na kwa nyakati tofauti kupitia jeshi lake, walishatoa taarifa zaidi ya mara mbili kabla ya zoezi hilo, lakini wavamizi hao hawakuonyesha kukubaliana na maelekezo ya serikali.

Kenyala aliwaasa wale wote waliovamia maeneo ya watu na kujenga nyumba zao waanze kubomoa wenyewe mapema, kabla hawajafikiwa na operesheni hiyo kwa kuwa ni endelevu.

ALIYEVUNJIWA NYUMBA ANENA

Mmoja wa wananchi waliovunjiwa nyumba, Irine Joseph (62), aliyekuwa na nyumba ya chumba kimoja na sebule ambaye alihamia tangu Septemba mwaka jana, alisema aliamka jana saa moja asubuhi na kwenda kuchota maji katika bwawa lililo jirani na eneo hilo la Kaza Roho.

“Nikiwa bado bwawani majira ya saa mbili na nusu au saa tatu hivi, nilisikia mlio wa mabomu yakipigwa na baada ya muda kidogo wakaja majirani waliokuwa wanakimbia na kunieleza kwamba, kitongoji chetu kimevamiwa na askari ambao walikuwa wanarusha mabomu na huku matingatinga yakibomoa nyumba zetu,” alisema.

Alisema alishindwa kurudi kwa sababu watu walikuwa wakikimbia hovyo na ilimbidi asubiri katika eneo la Shule ya Msingi ya Msigano anakosoma mjukuu wake anayekaa naye hadi saa saba mchana, aliporudi kuangalia kinachoendelea.

Alisema anakaa na wajukuu zake wawili Irene Robert anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Msigano na Baraka Robert ambaye hajaanza shule ambao alisema kwa bahati walikuwa wamechukuliwa na baba yao kwenda maeneo ya Mbagala anakoishi baba yao.

Joseph alisema kwamba eneo hilo alinunuliwa na mtoto wake Robert anayeishi Mbagala na ndiye ambaye alimjengea nyumba hiyo na kisha kumtoa nyumbani kwao Kigoma ili aje kumlelea watoto wake.

“Ninawashukuru sana askari waliojitolea kunitolea baadhi ya vifaa vyangu ndani ili visiharibiwe kabisa, yaani magodoro mnayoyaona, masanduku, viti na vinginevyo, ninachoweza kusema ni kwamba nawaomba wasamaria wema wanisaidie namna ya kuondoka hapa kwani sijui nitaondokaje,” alisema.

KAULI YA ALIYEVAMIAWA

Mmoja wa wakazi ambao maeneo yao yalivamiwa, Joyce Lawrence Mkude, alisema eneo lake ambalo ni shamba lenye ukubwa wa eka nane alilokuwa amepanda mananasi, minazi na maembe lilivamiwa tokea mwaka 2008.

Alisema alikwenda siku moja mwaka huo na akawakuta wavamizi hao ambao waliitana kwa kupigiana filimbi na kisha walimvamia na kumpiga vibaya, wakimtuhumu kuwa amevamia eneo lao.

“Walinivunja kidole cha mwisho cha mkono wa kushoto ambapo nilienda polisi Wazo nikatoa ripoti na kupatiwa PF 3 na kwenda kutibiwa katika hospitali ya Mwananyamala. Tumeshapeleka suala letu la kuwavamiwa maeneo yetu siku nyingi kwa RC (Mkuu wa Mkoa) na DC (Mkuu wa Wilaya) ili tusaidiwe. Ninafurahi kwamba hatimaye leo tumesaidiwa,” alisema.

Mkude alisema wavamizi hao walikata miti ya mazao aliyokuwa ameyapanda na kisha sehemu ya eneo lake wakauziwa watu wengine ambao walijenga nyumba zao.

Alisema kila alipojaribu kwenda katika eneo lake aliishia kutishiwa maisha yake na wavamizi hao, ambao wengi wao wanatoka katika mkoa wa Kigoma.

HALI ILIVYOKUWA KATIKA ENEO LA TUKIO

Tingatinga nne zilionekana zikibomoa nyumba moja baada ya nyingine bila ya upinzani kwa kuwa wenyeji tayari walikuwa wamekimbia na kuacha vitu vyao ndani.

Tingatinga lilikuwa likitifuata nyumba na kulipiga paa na kuvunja kuta zake na kuhakikisha kwamba imeanguka kabisa.

GONGO YAGUNDULIKA


Katika harakati za kubomoa nyumba baada ya nyumba, tingatinga moja lilibomoa nyumba moja ambamo ndani yake kulikutwa mitambo inayodhaniwa kuwa ni ya kutengenezea gongo pamoja na mapipa yapatayo 20 yaliyokuwa yamejaa pombe hiyo, pia kulikuwa na madumu yapatayo 12.

Aidha, katika purukushani hiyo, polisi walimkamata kijana mmoja aliyekuwa na dumu la lita 20 linalodhaniwa kuwa lilikuwa na pombe hiyo.

Kijana huyo alikuwa ameshika panga na kutishia kumdhuru askari mmoja, lakini alidhibitiwa na kupata kipigo na hatimaye alifungwa pingu na kupelekwa kwenye gari la huduma ya kwanza kwa ajili ya matibabu kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya hatua zaidi.





CHANZO: NIPASHE

 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom