Ardhi ya Tanzania inatumikaje?

Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,071
1,364
Nimekuwa nikijiuliza hivi hii ardhi inayoachwa wazi hapa Tanzania ni kwa faida ya nani? Na hali watu wanakufa na njaa na uchumi wetu bado hauridhishi?

Ukiwa unatoka Dar-es-Salaam kwenda mikoani utakuta ardhi kubwa tu nzuri lakini ipo tupu. Nilipojaribu kuchunguza nikaambiwa eti hatuna teknolojia ya kuilima na hapohapo tunaletewa nyanya mbogamboga toka South Africa na matunda; Je, kweli serikali imeshindwa kuitumia ardhi yetu kwa maendeleo ya taifa letu ili at least tuondokane na njaa na kupungua bei ya vyakula.

Sisi sio wabunifu, mapesa yaliyoibiwa BOT na yale ya RICHMOND hayakuweza kuwekeza katika kilimo basi kwa kununua matrekta na kufanya kilimo cha kisasa mbona viongozi wetu sio wabunifu? Ila nawasifu kwa ubunifu wa kujilimbikizia mali na techniques za kifisadi. Watanzania wenzangu it's time to get up and be creative with the technology we have.And you future leaders, you need to be creative naona hawa waliopo wamechoka na hawataki kushaurika it is us who are going to change this nation.
 
Iron Lady,

Karibu JF. Some guys will be responding to your post soon. It's nice to have your comments in here.

BTW: Nimeirekebisha topic yako kidogo tu na naamini ni kwa ufanisi zaidi.

Invisible
 
Nimekuwa nikijiuliza hivi hii ardhi inayoachwa wazi hapa Tanzania ni kwa faida ya nani? Na hali watu wanakufa na njaa na uchumi wetu bado hauridhishi?

Ukiwa unatoka Dar-es-Salaam kwenda mikoani utakuta ardhi kubwa tu nzuri lakini ipo tupu. Nilipojaribu kuchunguza nikaambiwa eti hatuna teknolojia ya kuilima na hapohapo tunaletewa nyanya mbogamboga toka South Africa na matunda; Je, kweli serikali imeshindwa kuitumia ardhi yetu kwa maendeleo ya taifa letu ili at least tuondokane na njaa na kupungua bei ya vyakula.

Sisi sio wabunifu, mapesa yaliyoibiwa BOT na yale ya RICHMOND hayakuweza kuwekeza katika kilimo basi kwa kununua matrekta na kufanya kilimo cha kisasa mbona viongozi wetu sio wabunifu? Ila nawasifu kwa ubunifu wa kujilimbikizia mali na techniques za kifisadi. Watanzania wenzangu it's time to get up and be creative with the technology we have.And you future leaders, you need to be creative naona hawa waliopo wamechoka na hawataki kushaurika it is us who are going to change this nation.

iron lady,
Umegusa eneo nyeti ambalo viongozi wetu hawapendi kulitilia maanani. Huku mjini utasikia kwmba kwenda kulima ni adhabu wala si maendeleo.
Angalia hata miundombinu ilivyotawanywa, huwezi kusafirisha mazao ya ziwa Tanganyika au mawese kutoka Kigoma kulleta Dar kwenye soko kubwa ndani ya siku moja. Ukitaka kusafiri kwa gari toka Mwanza kuja Dar ndani ya siku moja hadi upite Kenya anbako kuna barabara nzuri.
Bukoba kuna ndizi na mihogo mingi tu lakini sasa hivi nasikia hata meli hakuna, uwanja wa ndege wao ni sawa na kiwanja cha mpira. Npanda nasikia mahindi unaweza kulima mara tatu kwa mwaka, lakini barabara iko wapi?
Siasa zetu za ujamaa na kujitegenea badala ya kuhimiza kilimo cha kisasa kw kuleta matrekta madogo madogo walijenga kiwanda cha Ubungo Farm Implements ambacho kimekufa tayari. Bado watawala wanokuja nyuma hawajaona hilo hasa ktk kuwaleta wawekezaji wakubwa wenye mtaji wawekeze humo au kuwawezesha wajasiriamali wa kitanzania kwa kuwapa pembejeo na mikopo.
 
Good observation iron lady,
kuna swali moja tulikuwa tunajadili sekondari, miaka ile tunasoma. Ninalikumbuka kwasababu hiyo iliyokukereketa mpaka ukaanzisha thread hii. Swali lilikuwa hivi, "Although, Africa is a vast continent but still suffer from overpopulation?"

Kwamba ukubwa wa ardhi tuliyonayo hautusadii, akili na jitihada zinaelekezwa katika eneo lililokwisha endelezwa. Ndiyo maana, watu wanalima hapo hapo mpaka ardhi inakosa rutuba (angalia mikoa ya Iringa na Mbeya) ile Isimani tuliyoisoma shuleni miaka ileee kwa uzalishaji wa mahindi hakuna kitu leo.

Nilichangia kwenye thread ya SUA Haitumiwi vizuri, kwamba tatizo letu hatuwatask watalaam ili waonyeshe ujuzi wao. SUA imezalisha watalaam wengi je wanatumiwa vipi? Mbona hatuoni impact? mbona kilimo cha miaka ya 1980 kilikuwa bora kuliko leo?

Lakini suala la kulima eneo kubwa siyo hoja, hoja ni je kilimo kinachofanyika kina tija? (productivity). Je mazao yanayozalishwa yanaubora wa kiasi gani? Nasikia kwamba nyanya zinazozalishwa Ilula (Iringa) haziwezi kuwekwa supermarket kwakuwa zinaoza haraka. Hapa ndipo tunapo wahitaji watalaam.

Shida iliyopo ni vipaumbele, serikali haijaweka kipaumbele kwenye kilimo!! angalia badget za miaka ya karibuni.

Hata fedha za Kikwete, waliokopeshwa ni wafanya biashara ndogondogo (Machinga). Nchi imeamua kuzalisha machinga siyo mazao ya kilimo. Vijana wanaondoka vijijini na kwenda Mjini kutembeza bidhaa.

Hatuwezi kuendeleza nchi kwa vijana kuwa machinga. kilimo ndiyo uti wa mgongo (japo ni wimbo tu kwasasa). Angalia nchi kama China, Thailand hizi ndizo nchi zenye maendeleo ya kasi duniani kwasasa. ni nchi za kilimo (agrigarian societies).

bila kilimo bora, Tanzania yenye neema hakuna!
 
Back
Top Bottom