Ardhi University wapigwa mkwara

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
SERIKALI imewataka wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) waliogoma, warudi madarasani mara moja na kama wakikaidi, watachukuliwa hatua za kinidhamu kulingana na sheria iliyoanzisha chuo hicho.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Naomi Katunzi, alisema:

“Serikali inasisitiza kwamba mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi hauna mantiki yoyote na migomo hairuhusiwi vyuoni, hivyo watakaobanika kujihusisha na mgomo huo, watachukuliwa hatua za kinidhamu kulingana na sheria.”

Katunzi alisema serikali iliishatoa tamko rasmi Novemba 8 kuhusina na mustakabali wa wanafunzi waliojiandikisha chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhamishiwa ARU kwa sheria ya mwaka 2005 na kueleza kuwa watapewa shahada zao katika chuo kipya.

“Serikali inasisitiza kuwa ARU ni chuo kinachokidhi mahitaji yote yanayohitajika na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na elimu inayotolewa ina ubora uleule kama UDSM, ambacho kimefutwa kwa sheria namba 7 ya vyuo vikuu ya mwaka 2005,” alisema Katunzi.

Aidha, Katunzi alitoa ufafanuzi kuhusu tatizo la fedha za ‘Project’ na mahitaji maalum ya vitivo na kusema taarifa alizonazo ni kuwa Bodi ya Mikopo imeishapeleka hundi chuoni hapo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na kwa wanafunzi wengine wanaoendelea na kustahili mikopo wameishaingiziwa fedha kwenye akaunti zao.

Kuhusu malalamiko ya wanafunzi ambao hawajafanyiwa usaili, alisisitiza kuwa ni vema wanafunzi hao wakaheshimu maamuzi ya serikali ya kuwashirikisha wazazi katika kuchangia elimu ya juu, kwani ili vyuo viweze kujiendesha ni lazima kuwe na fedha.

Katunzi pia alitoa tamko kuhusu wanafunzi wawili waliofeli mtihani na kufukuzwa na kusema kuwa kufeli si jambo geni vyuoni na hasa ARU, hivyo ni vema wanafunzi wakafuata taratibu zilizowekwa za kukata rufaa kama wanaona wameonewa.

Wakati huohuo, wanafunzi wa ARU jana walisitisha mgomo wao na kuingia madarasani kwa kuhofia kufungwa kwa chuo ikiwa wangeendelea na mgomo kwa siku ya tatu mfululizo.

Hayo yalibainishwa na wanafunzi hao walipokuwa wakiongea na Tanzania Daima kwa sharti la kutotajwa majina yao na kusema walilazimika kurejea madarasani kuogopa sheria ya vyuo vikuu inayosema mwanafunzi asipoingia darasani kwa muda wa siku tatu mfululizo, chuo kitafungwa na wanafunzi watarudishwa nyumbani.

Wanafunzi wa ARU walianza mgomo huo Novemba 25, wakipinga kufanyika kwa maafali ya chuo hicho ambayo yamepangwa kufanyika Desemba 22, wakidai kutokutambua vyeti vitakavyotolewa na chuo hicho na kutaka cheti cha kilichokuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Usanifu wa Ardhi na Majengo (UCLAS), ambacho walisajiliwa toka mwanzo.

Pia walishinikiza kurudishwa kwa wanafunzi wenzao wawili waliofukuzwa; Simon Joseph na Elias Nicholaus wa mwaka wa tatu, ikiwa ni pamoja na kushinikiza wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili wasajiliwe.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
 
migomo vyuo vikuu inaisha lini. katunzi naye ana jambo. si yule yule aliyekuwa anariport mambo ya wizara kipindi cha migomo mpaka akansalimu amri wakati hao vijana wamegoma mwaka huu mwanzoni?
 
Back
Top Bottom