Ardhi ni Bomu ambalo litavuruga amani ya Tanzania, Ubinafsi wa watawala utatuponza!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ardhi ni Bomu ambalo litavuruga amani ya Tanzania, Ubinafsi wa watawala utatuponza!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPadmire, Mar 31, 2012.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hata hao wawekezaji wanaopewa ardhi kwa bei ya kutupwa waangalie hali halisi ya jamii inayoizunguka.

  Wawekezaji wasome alama za nyakati, wawekeze mabilion yao halafu muda mfupi ujao wataacha wakimbilie kwao. kukitulia watakuja kukuta kila kitu kimebadilika na hawana chao tena.


  Wimbi la vijana kukosa ajira, uchumi kudorora, umasikini kuongezeka, idadi ya masikini kuongezeka tanzania ni hatari.

  Viongozi wa serikali kugawa ardhi kwa wageni wa nje na kuwasahau watanzania ni bomu lililotegwa. Litalipuka muda wowote. Wapo viongozi wameweka hela nje ya nchi, sijui ndo watakimbilia huko? Ila sina imani sana na benki za nje, maana kikinuka huku, hata pesa zao hutaifishwa. Hawako salama sana, ni ujinga wao tu. Angalia Mobutu, Ben Ali tunisia, Misri, gadaffi na wengineo.

  Hii ya vigogo kumiliki ardhi kubwa sana -kwa maefu (ref Budget ya wizara kivuli ya ardhi -Upinzani) na kuwanyima wananchi walio wengi ni hatari.

  Pia sehemu nyeti za makazi na kuishi zinamilikiwa na vigogo kama Mwanza, Mbeya, Njiro, Burka, n.k

  Nyumba za serikali wamepeana vigogo kwa bei ya kutupa, unakuta vigogo wanamiliki mpaka nyumba kumi.


  haki hapo ipo kweli? Halafu tukisema tunaitwa wachochezi,
   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Ndugu Ardhi yetu kwa sasa ndio imekuwa kitanzi kwa mtanzania.
  Kinachofanyika hivi sasa ni kwamba, anajitokeza mtanzania ananunua ardhi ya mtanzania mwenzake kwa 30M, then anaiuza ardhi hii kwa mgeni kwa 1Billion, kodi zote na kila kitu kinalipwa vizuri kabisa.

  It appears to be very genuine, lakini the issue is dirty money has find its way into our economy, worse enough that one transaction shift the land price level such than no black Tanzanian can afford.

  The government with all the softicated security machinery is there looking at all this
   
 3. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  what hapening over land is the aftermath of bad governance that heading by c.c.m goverment,in fact c.c.m fail to run URT
   
 4. h

  haki na usawa JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 476
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Naomba wauze sana ili tuwahi kufika maana mkulima ukimwambia hakuelewi
  Ni bora wafanyanye hivyo na hii ni laana kwa vile hawaoni na hawasikii na wanataka kila kitu
  Na mwananchi atakapokatazwa au kuawa kwa ajili ya ardhi ndo atajua yanayoongelewa katika jukwaa la siasa za chama chake na je kina msaada gani
  Mimi naomba wachukue maeneo yote mazuri wawape wawekezaji kupitia TIC na wafanyanye haraka maana bei ya ardhi ni ndogo sana kwasababu ya umasikini uliokidhiri
  Na mfano shamba la miwa Bagamoyo hawana muda mrefu nao watakiona cha mtema kuni
  Na kama si mashamba wapewe wachimbe madini na askari wawachape risasi watakaokaribia waya au geti la mgodi na wafanye hivyo katika nchi yote ili wananchi wazoee risasi haraka
  Na wawape viwanda vyote ili maskini tuwe wengi na ili tutakapoingia barabarani tuwe wengi
  Na dada zetu waruhusiwe kuvaa vyovyote kwani mila zetu ni mbaya na tunaficha miili sana bora tuiweke hadharani na tuweze kununuliwa na wenye hela kwa ajili ya starehe
  Na watakaoichoka na milli haiuziki tena na wale tutakuwa nao barabarani kudai haki yetu
  Na naomba madarasa ya kutwa yawe mengi kuliko ya bweni ili tuimarishe ukabila na tukose umoja haraka ibaki umoja katika shida na mateso ya watawala
  Na wajenge hospitali kwa kuchukua ardhi mapema ili vifo vipungue na wadai tuwe wengi
  Na madini nayapitikane nchi yote ili wawahi kututoa na kumpa mwekezaji nasi tuweze kuunganisha nguvu mapema kwa shida zetu na kutolewa katika ardhi ya mababu zetu
  Na kila msitu au pori zuri apewe mwekezaji ili alime Jatropha na sisi tukose kuni na madawa ya asili ili tuwe wengi tunaoumia kwa manyanyaso
  Na naomba wawekezekezaji wataopewa ardhi waweke fence ya umeme haraka ili watakaokufa kwa kutokujua kuwa umeme unaua ili watakao taka ndugu kwenda kumzika kwanini aligusa na wapigwe bakora za kutosha
  Na naomba waekezaji watumie polisi kwa kuwaadhibu wananchi waliokaribu na maeneo yao ili wakione cha moto mapema
  Na naomba wawekezaji watumie sumu sana ili madhara yasambae mapema na wawakodishie wabunge ndege na kuwalipa malipo mazuri ili madhara yaendelee
  Na naomba wawekezaji wawalipie NEMC nauli na posho ili kuja kukagua na wasiseme chochote
  Na naomba kila mwanasiasa apate eneo la madini ili naye awe na mgodi na awalete wawekezaji mwenyewe na waingie ubia na wananchi waambulie kibarua na mikong'onto
  Na naomba kila sehemu yenye maji pia apewe mwekezaji ili wananchi wakose maji ili tuwe wengi barabarani
  "NASHUKURU KWANI UKOMBOZI UKO KARIBU BAADA YA KUANZA CHA WOTE KUWAPA WAGENI ILI TUKOSE PA KUSHIKA NA ILI TUAMKE KUDAI UHURU UPYA!"
   
 5. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kazi nzuri sana mkuu...keep it up.
   
 6. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Kweli haki na usawa.

  Watanzania tumekuwa mazuzu mno, waoga.

  Bora hawa watawala wazidi kufanya madudu ili tupate machungu ili tuamke.

  Lets wait and see.

  Angalizo, katika hali hii, sio hao wageni au watawala watakaokuwa salama when time bomb will erupt!!!
   
 7. sodeely

  sodeely Senior Member

  #7
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Umefafanua vizuri sana..
   
 8. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mama salma Kikwete amekumbwa na kashifa ya Kupora Ardhi ya Wapiga kura Mkoani Lindi, kwa kutumia madaraka ya Ikulu!!!!!!!!!!

  Salma Kikwete
  aichafua Ikulu

  *Atumia nafasi yake kujimilikisha ardhi mkoani Lindi
  *Afanya yale yale ya Anna Mkapa, enzi za Ben Mkapa
  *Wenye ardhi walalamika, Mahakama yatoa hukumu


  MKE wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
  wa Tanzania, Mama Salma Kikwete,
  ameiingiza Ofisi ya Ikulu katika
  kashfa, baada ya kutwaa ardhi yenye ukubwa
  wa ekari takriban 250 ndani ya halmashari ya
  Mji wa Lindi kwa kutumia kivuli cha Taasisi
  yake ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),
  ANIKA Ukweli linaweza kuthibitisha.
  Uchunguzi wa kina uliofanywa na timu ya
  waandishi wa gazeti hili mkoani Lindi na Dar


  es Salaam, umebaini kwamba
  utwaaji huo wa ardhi aliufanya
  kati ya mwaka 2009 na 2010.
  Kuibuka kwa kashfa hii kumekuja
  baada ya baadhi ya waliokuwa
  wamiliki halali wa ardhi hiyo
  kufungua shauri katika
  Mahakama ya Usuluhishi ya
  Migogoro ya Ardhi ya Mjini Lindi,
  wakilalamikia kulipwa fidia
  kidogo kulingana na ukubwa wa
  ardhi na mali zilizomo ndani ya
  ardhi yao.
  Shauri hilo ambalo lilikuwa
  chini ya Hakimu Njiwa J, kama
  Mwenyekiti wa Jopo la Baraza la
  Ardhi, lilifikia tamati Septemba
  7, mwaka jana, kwa baraza hilo
  kukubaliana na walalamikaji
  ambao katika shauri hilo
  waliwakilishwa na Lali Mchokozi,
  hamed S. Mahafoudhi na Fatuma
  S. Mahafoudhi.
  Ardhi ambayo Mama Salma
  anadaiwa kujimilikisha,na
  ambayo inakadiriwa kuwa na
  ukubwa wa ekari 250, ipo katika
  eneo la Mabano-Mitwero ndani
  ya Halmashauri ya Mji wa Lindi.
  Inaelezwa kwamba mke huyo wa
  Rais aliitumia Halmashauri hiyo,
  chini ya usimamizi wa
  Mkurugenzi kutwaa ardhi hiyo
  ikiwa ni pamoja na kuwalipa fidia
  wamiliki wa mwanzo wa ardhi
  hiyo, ingawa karibu wote
  walilalamikia fidia hiyo kwamba
  ni ndogo.
  Kwa mujibu wa hukumu ya
  shauri hilo dhidi ya Mama Salma,
  walalamikaji hao walifungua
  shauri lao katika Mahakama ya
  Mkoa wa Lindi, Kitengo cha
  Ardhi Desemba 13, 2010, kabla
  hukumu hiyo kutolewa
  Septemba 7, 2011, kwa
  kuwaamuru wahusika wa utwaaji
  wa ardhi hiyo kufanya tathimini
  upya ya ardhi na mali zilizomo
  na kuwalipa fidia stahiki kwa
  mujibu wa Sheria ya Ardhi ya
  mwaka 1999, kifungu cha 3 (1) (g).
  "Napenda kuchukua fursa hii
  kukutaarifu kuwa baada ya
  kulipwa fidia na taasisi ya WAMA,
  unapewa notisi ya siku 90
  kuanzia tarehe 15/10/2009 mpaka
  tarehe 15/01/2010 uwe umehama
  katika eneo husika. Sheria ya
  Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999,
  Sheria ya Utwaaji Ardhi Na 47 ya
  mwaka 1967 na Sheria Na 8 ya
  Mipangomiji ya mwaka 2007
  zimezingatiwa katika kutekeleza
  adhma hii," inasema sehemu ya
  barua ya notisi iliyotumwa kwa
  mmoja wa wananchi ambao ardhi
  yao imetwaliwa na Mama Salma
  Kikwete ya Oktoba 13, 2009 na
  kusainiwa na I.H. Chepa kwa
  niaba ya Mkurugenzi wa
  Halmashauri ya Mji wa Lindi.
  Mbali na Mchokozi, Hamed
  na Fatuma Mahafoudhi, wengine
  ambao ardhi yao ilitwaliwa, na
  ambao wamelalamikia fidia
  ndogo, ingawa hawapingi
  kutwaliwa kwa ardhi yao, ni
  pamoja na Salima Mohamed
  Luka, Lucy Anthony Magulya,
  Adamu Matwanje, Morris Musika,
  Jane John Alfred, Kaisi Bakari
  Kaisi, Abdallah Ismail Sokwe,
  Halima Lali Ismail, Hashimu Lali
  Ismail, Juma Seleman Madembe,
  Mohamed Said Dadi, Habiba
  Ally, Halima Mwishante, Alimbe
  Ally Abdallah, Mugabo Wekwe,
  Yohana Izaka Mnimaika, Jacob
  Issa Mpili, Evarist Munyeti
  Shileki na Issa Salum Mnala.
  Katika madai yake mbele ya
  wajumbe wa Baraza la Ardhi,
  Mchokozi, pamoja na mambo
  mengine, anasema alifunga
  safari hadi kwa Mama Salma
  Kikwete kulalamikia zoezi zima
  uthamini wa ardhi yake, lakini
  mke huyo wa Rais akamtuliza
  kwa kumwambia asiwe na
  wasiwasi atalipwa fidia stahiki,
  kabla ya kumpoza na Sh 50,000.
  Aidha, anasema eneo lake la
  ardhi lilikuwa na ukubwa wa
  ekari 10, likiwa na nyumba mbili
  za kuishi familia yake pamoja na
  mazao kadhaa ikiwamo minazi
  20, lakini yalipokuja malipo ya
  fidia ya ardhi yake hiyo, alikuta
  ametengewa Sh 2,400,000. Hata
  hivyo, anasema eneo lake hilo,
  kama lingethaminiwa sawa sawa
  na mali zake zilizomo angeweza
  kupata walau Sh 20,000,000.
  Kwa upande wake,
  mlalamikaji wa pili katika shauri
  hilo, Hemed Salum Mahfoudhi,
  aliliambia jopo hilo la wajumbe
  wa Baraza la Ardhi kwamba yeye
  hakuwa akijua hasa ukubwa wa
  shamba lake. Hata hivyo,
  anasema hakushirikishwa katika
  zoezi zima la kutwaliwa kwa
  ardhi yake na wala hakuwa akijua
  kama ardhi yake ilishatwaliwa
  hadi pale alipitwa kuchukua
  fedha za fidia ya eneo lake katika
  ofisi ya Mkurugenzi wa
  Halmashauri ya Mji wa Lindi na
  kukuta fidia yenyewe ikiwani Sh
  170,000 tu. Kutokana na hali
  hiyo, yeye anataka ama alipwe
  fidia ya Sh 15,000,000 au ifanyike
  tahimini upya ya ardhi na mali
  zilizomo kwa mujibu wa sheria ya
  ardhi.
  Mlalamikaji wa tatu, Fatuma
  Salum Mahfoudhi, anasema
  wakati fulani mwaka 2009 akiwa
  nyumbani kwake alifikiwa na
  mgeni aliyejitambulisha kwake
  kwa jina la Mussa, na
  kumwambia kwamba yeye
  alikuwa ni Saveya (Surveyor)
  kutoka Halmashauri ya Lindi.
  Aliendelea kusema kuwa Mussa
  alimwambia alikuwa amefika
  hapo kwa lengo la kufanya
  tathimini ya eneo lake hilo na
  kwamba kazi hiyo alikuwa
  ametumwa na mke wa Rais,
  Mama Salma Kikwete.
  Aidha, Fatuma alilieleza
  baraza hilo kwamba ardhi yake
  ilikuwa na ukubwa wa ekari tatu
  na nusu, lakini pia ikiwa na
  nyumba moja yake ya kuishi na
  familia yake. Alisema pia
  kwamba mbali na nyumba hiyo
  kulikuwamo mazao ya miti ya
  mikorosho 58, migomba 18 ya
  ndizi na kadhalika, lakini fidia
  aliyolipwa ni Sh 1,962,000.
  Anasema baada ya kulipwa
  fidia hiyo, alijikuta akipewa
  notisi ya siku 90 kuondoka katika
  ardhi yake hiyo, kabla ya
  kufunga safari hadi Dar es
  Salaam yalipo makao makuu ya
  WAMA. Akiwa katika ofisi za
  WAMA, anasema alibahatika
  kukutana na Mama Salma
  Kikwete, ambaye baada ya
  kumsikiliza malalamiko yake,
  alimjibu kuwa ardhi yao hiyo
  yeye haichukui kwa nguvu bali ni
  kwa makubaliano yao na
  halmashauri yao ambayo hiyo
  ndiyo inayoshughulikia malipo
  yao ya fidia. Mbali na
  Mwenyekiti Njiwa J, wengine
  waliounda jopo hilo wametajwa
  kwa majina ya Jumaa na Kitenge.
  Katika hukumu ya Mahakama
  hiyo, Mwenyekiti huyo alisema
  haoni mantiki ya walalamikaji
  hao kutaka walipwe fidia ya Sh
  15,000,000 kila mmoja, lakini pia
  Mwenyekiti huyo akasema
  anakubaliana na madai ya
  walalamikaji hao ya kwamba
  fidia hiyo waliyopewa siyo ya
  sawa na ya haki, na hivyo
  akamwamuru mlalamikiwa,
  ambaye ni Halmashauri ya
  Manispaa ya Lindi kufanya
  tathimini upya ardhi na mali za
  walalamikaji hao ili waweze
  kulipwa fidia yao stahiki kwa
  mujibu wa Sheria ya 1999,
  kifungu cha 3 (1) (g).
  Sheria na kifungu hicho kwa
  mujibu wa hukumu hiyo ambayo
  gazeti hili limefanikiwa kupata
  nakala yake, inasema pamoja na
  mambo mengine, kwamba moja
  ya mambo ya msingi kabisa
  yanayozingatiwa na sheria ya
  asili ya ardhi ni kwa mmiliki wa
  ardhi kulipwa malipo ya haki na
  kwa wakati.
  Juhudi za kumpata Mama
  Salma Kikwete au ofisa yeyote
  wa WAMA ili kuzungumzia kashfa
  hii mpya ambayo wachambuzi
  wa mambo wamelielezea kama
  mwendelezo matendo wa wake
  wa marais kutumia nafasi zao
  kujitwalia raslimali za nchi kwa
  kutumia vivuli vya taasisi zao,
  hazikuzaa matunda hadi
  tunakwenda mitamboni juzi
  Jumatano.
  WAMA, kama ilivyokuwa
  EOTF enzi za utawala wa Mzee
  Benjamin Mkapa, ni taasisi
  binafsi iliyoanzishwa na Mama
  Salma Kikwete ikiwa na malengo
  ya kuwainua wanawake na
  watoto wa kike kimaendeleo.
  EOTF nayo ilianzishwa na Anna
  Mkapa, wakati Mkapa akiwa
  Ikulu, ikiwa na malengo hayo
  hayo ya kuwapa fursa za
  kiuchumi wanawake nchini.
  Hata hivyo, tofauti na
  malengo mazuri hayo, Mama
  Anna Mkapa, aliitumia taasisi
  yake hiyo kununua ardhi katika
  maeneo mbalimbali nchini, ikiwa
  ni pamoja na kununua majengo
  ya yaliyokuwa yakimilikiwa na
  Serikali, kwa kutumia kivuli cha
  ubinafsishaji uliokuwa
  unaratibiwa na Tume ya
  Kurekebisha Mashirika ya Umma
  (PSPRC) iliyoundwa na utawala
  wa Rais Mkapa kwa lengo la
  kuharakisha na kusimamia
  uuzwaji wa zilizokuwa mali za
  umma.
  Source :ANIKA UKWELI, IJUMAA, MACHI 30 -APRILI 5, 2012 HABARI 3
   
 9. C

  Comreed Member

  #9
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  sio mama salma pekee wako wengi waliotwaa ardhi kinyemela
   
 10. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mwana wa Vasco anamiliki majumba na ardhi kubwa Arusha, je wananchi wengine hawataki ardhi.

  kwa nini wizara ya ardhi au hizi manispaa zisiweke utaratibu ulio wazi wa wazawa au wananchi kumiliki ardhi?
   
Loading...