Ardhi na Maendeleo ya mgeni njoo mwenyeji akonde! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ardhi na Maendeleo ya mgeni njoo mwenyeji akonde!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Apr 5, 2009.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Apr 5, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mwezi Machi, nilipata wasaa wa kushiriki mkutano wa wananchi katika mtaa wa Kwembe, mkutano mambo kadhaa niliyatakari siku hiyo yaliyonifanya niandike makala ifuatayo ambayo naamini maudhui yake yanapaswa kujadiliwa:

  "Wahenga walisema, mgeni njoo mwenyeji apone. Msemo huu, ni ishara ya baraka njema inayoletwa na wageni chini ya ukarimu wa kiafrika. Hata hivyo, yapo maeneo ambayo ujio wa wageni ama wa mambo mageni umezua hasara kwa upande wa wenyeji. Tunayaona hayo katika maeneo ya uwekezaji ambayo wenyeji wameondolewa kwa shuruti kupisha wageni bila kupata manufaa ya kutosha kutokana na ujio wa wageni hao. Hayo yamejitokeza katika sekta za uchimbaji madini, uwindaji na maeneo mengine yanayohusiana na rasilimali za taifa. Hapo ndio unapoweza kuzuka msemo mpya wa mgeni njoo mwenyeji akonde. Si dhamira ya makala yangu ya leo kuzungumzia hayo ya wageni katika maeneo ya rasilimali wengi wao wakiwa kutoka nje, leo nataka nizungumze kuhusu wageni wa ndani katika sekta ya ardhi. Inaendelea

  Makala kamili inapatikana hapa: JJ: March 2009

  JJ
   
 2. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna bilioni tatu zilipotea kifisadi kama ambavyo makala imeeleza. Fedha hizo wamelipwa fidia wananchi, na kuwakwamua kiuchumi chini ya falsafa ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Waziri Chiligati naye anapowapa waandishi wa habari viwanja hivyo ni sehemu ya jitihada za serikali kuwajali wanahabari. Halafu saula hili sasa limepelekwa mahakamani hivyo kuendelea kulijadili ni kuingilia uhuru wa mahakama.

  .........ndiyohiyo
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kwani mahakama imekataza kulijadili? Na wale wasiohusika na kesi nao hawatakiwi kujadili yanayofanyika mahakamani?
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Yohana wa Mnyika,

  Nashukuru umelileta hili nikakumbuka taarifa kuwa Kenya wamingia mkataba na Oman wa kuwapa Oman ardhi wajilimie Chakula kwa miaka 80 kwa malipo ya kujengewa Bandari yenye thamani ya Dola Bilioni 4!

  Sasa najiuliza, je hiyo ardhi ni pori lisilo na watu sasa hivi? je kama kuna watu, watahamishwa na wapelekwe wapi? je kutakuwa na rutuba na maji ya kutosha kwa kujilimia na kulisha mifugo yao kama huko wanakondolewa ili mwekezaji ajilimie kwa kutujengea Bandari?

   
 5. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kweli, halafu inaonyesha hiyo makala ni ya Machi wakati kesi imefungiliwa April. Halafu humo kwenye makala imeelezwa ni kwa namna gani hizo bilioni 3 za walipa kodi zimetafunwa, na jinsi Chiligati anavyotumia kofia ya Uwaziri kugawa hivyo viwanja kwa wanahabari gazeti la CCM uhuru. Kwanini hajagawa kwa wa habari leo wa serekali kama ana lengo la kuwajali waandishi?

  Asha
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Mahakama haina mamlaka ya kuzuia freedom of expression ambayo iko kwenye katiba yetu kufuatia kuridhia lile alizimio la haki za binaadamu.

  Hata hivyo, mahakama inazuia kulijadili shauri lililoko mahakamani katika hali ambayo inaweza kuingilia uhuru wa mahakama katika kutenda haki 'contempt of the court'

  Sisi tunafuata mfumo wa sheria wa Comon
  Law tuliorithishwa na waingereza ambapo mtuhumiwa yoyote anahesabiwa 'not guilt until proven guilt by the court of competent jurisdiction'.

  Kwa sheria hii, ni marufuku kupiga posed pictures/video au kuwakutanisha watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi au mahakamani.

  Ni mara ngapi tunaonyeshwa video na picha za watuhumiwa wakiwa mikononi mwa polisi?.
  Ni mara ngapi wapiga picha na video wanapiga picha watuhumiwa ndani ya mahakama?. Vitendo vyote hivi ni ukiukwaji wa haki za binaadamu na kuingilia uhuru wa mahakama lakini mahakama imekaa kimya, wahusiki hawalalamiki kwa vile hawajui haki zao.

  Tufike mahali, wanaichi waelimishwe haki zao ili kuziba mianya ya watu kutotendewa haki.

  Nimemsoma JJMnyika, issue kubwa ni watu kujua haki zao
  Na kuhakikisha serikali inawatendea haki.

  Maeneo husika kama Kwembe, sio maeneo yanayomilikiwa na 'Customary Land Law' kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji No.5 ya 1999. Hao wananchi ni wavamizi wa maeneo hayo na sheria imeukubali uvamizi wa miaka mingi ndio maana wanatoa fidia na kukubali kuhama.

  Kwenye ardhi halisi inayomilikiwa kimila, hata serikali haiwezi kuthubutu kuyatwaa maeneo hayo, mfano uchagani, umasaini, ama kwa Wahaya, wanaithamini ardhi kuliko thamani ya hela yoyote na kwao bora damu imwagike na sio ardhi iondoke.

  Pointi muhimu sana Mnyika ameraise ni hii ya Watu kutambua haki zao, na hata ukishatambua haki zako, hauletewi kwenye kisahani cha chai, bali ni lazima uzidai haki hizo.
   
Loading...