Ardhi bado haijapata suluhisho, siasa ni nyingi kuliko utendaji.

mng'oa kucha

Senior Member
Jul 31, 2013
150
179
Nimekuwa nikijaribu kufuatilia kwa karibu sana matatizo yaliyopo ardhi (wizarani na idarani) nikagundua mengi sana nakaona nisiwe mchoyo, hivyo nimeamua ku shirikisha wadau bure kabisa.

Wizara yenye dhamana na ardhi kwa nchi yetu ni wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi chini ya waziri Mh Lukuvi, huyu mheshimiwa ana matamko mengi ya kisiasa ambayo kiuhalisia hayatekelezeki, kwani jukumu kubwa la ardhi wanalo manispaa na halmashauri husika ambayo iko chini ya wizara tofauti (nimefurahi sana kuona leo waziri mkuu akiwakumbusha wanasiasa kutotoa matamshi ambayo hayatekelezeki)

naomba niongelee utaratibu wa kumiliki ardhi kwa nchi yetu ntatoa mfano hatua kwa hatua, utaratibu wa awali ni kumtafuta surveyor ambaye atakupa jibu kwamba eneo lako limetengwa kwa matumizi gani, huwa wanatoza wastani wa shilingi laki moja za kitanzania, kama eneo lako lilikuwa halijapangiwa matumizi yaani kwa lugha nyingine halina mchoro, itakulazimu uchore huwa ni minimum ya kilometa moja ya mraba kwa hiyo hapo utakuwa na kazi ya kuwashawishi majirani na kama majirani wengine wasipoonyesha ushirikiano itabidi itabidi ukomae mwenyewe au wale wachache walio tayari hapa tunazungumzia mamilioni ya hela ili kupata tu mchoro au kupanga eneo husika,

Mchoro utakaokuwa umependekezwa utakwenda kupitiwa na naraza la madiwani (wanasiasa) ambao hawana uelewa wowote wa ardhi ama mipango miji ila wenyewe ndio wenye dhamana ya kupitisha mchoro ama la na wako wengi wenye itikadi tofauti kwa hiyo hapo ndipo utakapoanza kuona ni rahisi ngamia kupita kwenye tundu la sindano a ikumbukwe hili baraza huwa linakaa kwa mwaka mara tatu (unaweza kunirekebisha) ila kifupi hapo ni kwamba mwaka umeshashakatika na mamilioni yasiyo na idadi pia yamekwenda.

Mchoro pendekezwa ukifanikiwa kupita katika baraza la hawa (wanasiasa) utaomba kibali cha kupimiwa eneo hii peke yake inaweza kuchukua mwezi mpaka miezi mitatu na hela itakutoka ikumbukwe haya yoye yanafanyika halmashauri ama manispaa husika, baada ya kupata kibali cha upimaji unaruhusiwa kutafuta kampuni binafsi ambapo gharama zao huanzia laki 8 na kuendelea kutegemea ukubwa wa ardhi na sehemu ardhi yako ilipo hapa inaweza kutumia miezi miwili ama mitatu ambapo utawekewa mawe ya namba (beacon).

baada ya eneo kupimwa utaandika barua kwenda kwa mkurugenzi wa eneo husika kuomba kumilikishwa utaambatanisha na fomu ambazo zitakuwa zimejazwa na mwenyekiti na mtendaji wa serikali ya mtaa, majirani na afisa kutoka kata hapo ndipo itabidi wachukue ramani ya mipango miji wizarani kubuka hauko peke yako ziko nyingi kwa hiyo "ushapu wako" ndio utakuwahishia kazi yako.

Baada ya hapo watakuletea makadirio ya kodi ambayo unastahili kulipa, ukishalipia karatasi zako zitarudi tena halmashauri au manispaa husika ili kutengenezewa risiti, via,natanishi vyoye pamoja na stakabadhi za malipo zitapelekwa wizarani kwa ajili ya kuandaliwa hati, ambapo pia utakuta kuna msururu wa watu itabidi pia uwe "mshapu" ili kupata hati yako.

Katika mtiririko huu mrefu nadhani mmeona ushiriki wa wizara ya ardhi ni sehemu ndogo sana sasa inashangaza kusikia waziri kusema hawa watu wapewe hati zao haraka sana wakati hilo zoezi hapo si chini ya miaka mitatu tena ukichanganya na "ushapu"

Tanzania bado tunasafari ndefu.
 
Huyo Lukuvi sioni achofanya hapo Wizarani zaidi ya kujitafitia Utajiri kwa maslai yake binafsi. Kule Mkuranga kuna migogoro kibao ya ardhi kuanzia Vijiji vya Lugwadu,Magodani mpaka Kigamboni na kote huko mtu anaeleta tatizo kwa kupora ardhi za Vijiji husika ni Muhindi mmoja almaarufu Bush. Anagawa sana pesa kuanzia Wilayani,Mkoani,Mahakamani mpaka Wizarani.
 
Hahaha kuna mama mmoja alipata shida nyingi sana za kupata umiliki wa kiwanja na nyumba aliyoachiwa na mumewe aliyefariki.
Katika maongezi alisema "mwanangu kama shetani yupo, basi sina shaka makazi yake yako Tanzania". Aliendelea kusema "ukitaka kufahamu shetani anaishi, subiri upate shida inayo husu ardhi, utamuona shetani kwa sura yake halisi".
Aisifiaye mvua imemnyea. Sina shaka na matatizo watu wayapitiayo huko ardhi, ni kuomba ukutane na watendaji wazuri.
 
Nimekuwa nikijaribu kufuatilia kwa karibu sana matatizo yaliyopo ardhi (wizarani na idarani) nikagundua mengi sana nakaona nisiwe mchoyo, hivyo nimeamua ku shirikisha wadau bure kabisa.

Wizara yenye dhamana na ardhi kwa nchi yetu ni wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi chini ya waziri Mh Lukuvi, huyu mheshimiwa ana matamko mengi ya kisiasa ambayo kiuhalisia hayatekelezeki, kwani jukumu kubwa la ardhi wanalo manispaa na halmashauri husika ambayo iko chini ya wizara tofauti (nimefurahi sana kuona leo waziri mkuu akiwakumbusha wanasiasa kutotoa matamshi ambayo hayatekelezeki)

naomba niongelee utaratibu wa kumiliki ardhi kwa nchi yetu ntatoa mfano hatua kwa hatua, utaratibu wa awali ni kumtafuta surveyor ambaye atakupa jibu kwamba eneo lako limetengwa kwa matumizi gani, huwa wanatoza wastani wa shilingi laki moja za kitanzania, kama eneo lako lilikuwa halijapangiwa matumizi yaani kwa lugha nyingine halina mchoro, itakulazimu uchore huwa ni minimum ya kilometa moja ya mraba kwa hiyo hapo utakuwa na kazi ya kuwashawishi majirani na kama majirani wengine wasipoonyesha ushirikiano itabidi itabidi ukomae mwenyewe au wale wachache walio tayari hapa tunazungumzia mamilioni ya hela ili kupata tu mchoro au kupanga eneo husika,

Mchoro utakaokuwa umependekezwa utakwenda kupitiwa na naraza la madiwani (wanasiasa) ambao hawana uelewa wowote wa ardhi ama mipango miji ila wenyewe ndio wenye dhamana ya kupitisha mchoro ama la na wako wengi wenye itikadi tofauti kwa hiyo hapo ndipo utakapoanza kuona ni rahisi ngamia kupita kwenye tundu la sindano a ikumbukwe hili baraza huwa linakaa kwa mwaka mara tatu (unaweza kunirekebisha) ila kifupi hapo ni kwamba mwaka umeshashakatika na mamilioni yasiyo na idadi pia yamekwenda.

Mchoro pendekezwa ukifanikiwa kupita katika baraza la hawa (wanasiasa) utaomba kibali cha kupimiwa eneo hii peke yake inaweza kuchukua mwezi mpaka miezi mitatu na hela itakutoka ikumbukwe haya yoye yanafanyika halmashauri ama manispaa husika, baada ya kupata kibali cha upimaji unaruhusiwa kutafuta kampuni binafsi ambapo gharama zao huanzia laki 8 na kuendelea kutegemea ukubwa wa ardhi na sehemu ardhi yako ilipo hapa inaweza kutumia miezi miwili ama mitatu ambapo utawekewa mawe ya namba (beacon).

baada ya eneo kupimwa utaandika barua kwenda kwa mkurugenzi wa eneo husika kuomba kumilikishwa utaambatanisha na fomu ambazo zitakuwa zimejazwa na mwenyekiti na mtendaji wa serikali ya mtaa, majirani na afisa kutoka kata hapo ndipo itabidi wachukue ramani ya mipango miji wizarani kubuka hauko peke yako ziko nyingi kwa hiyo "ushapu wako" ndio utakuwahishia kazi yako.

Baada ya hapo watakuletea makadirio ya kodi ambayo unastahili kulipa, ukishalipia karatasi zako zitarudi tena halmashauri au manispaa husika ili kutengenezewa risiti, via,natanishi vyoye pamoja na stakabadhi za malipo zitapelekwa wizarani kwa ajili ya kuandaliwa hati, ambapo pia utakuta kuna msururu wa watu itabidi pia uwe "mshapu" ili kupata hati yako.

Katika mtiririko huu mrefu nadhani mmeona ushiriki wa wizara ya ardhi ni sehemu ndogo sana sasa inashangaza kusikia waziri kusema hawa watu wapewe hati zao haraka sana wakati hilo zoezi hapo si chini ya miaka mitatu tena ukichanganya na "ushapu"

Tanzania bado tunasafari ndefu.
DAAH hatari sana!!
 
Ndiyo maana mimi binafsi sidhani kama kuna upinzani wa kweli Tanzania. Ni kiini macho tu! Wapinzani wapo (baadhi) ila upinzani wa kweli HAKUNA. Ngoja nirekebishe kauli yangu. Hakuna chama (ikiwemo CCM) ambacho kiko serious katika utatuzi wa kero za watanzania, ni porojo tu.

Kuna matatizo kama haya ya msingi kabisa yanayoumiza watu wengi lakini hamna chama hata kimoja ambacho unaweza kusema platform yake ni kodi ndogo kwa wafanyabiashara wa kitanzania, kuondoa urasimu kwenye ardhi, umeme wa uhakika, kutatua changamoto za kilimo, nk. Sanasana wanaandika hayo mambo kwenye ilani zao za uchaguzi ila wakisimama majukwaani ni mipasho tu matokeo yake hamna jinsi ya kumbana mtu akipewa uongozi atekeleze alichoahidi.
 
By the way, natambua CCM wamekuwa na kamchezo ka kuteka sera za upinzani na kuzifanya zao, hiyo ni challenge kubwa inayowakabili wapinzani. Je matokeo chanya tunayaona katika utekelezaji wa hizo sera au CCM wanaharibu kwa makusudi ili sera za upinzani zionekane mbovu?
 
Back
Top Bottom