Arab Contractorss wakabidhiwa rasmi eneo la ujenzi wa mradi wla kufua umeme wa Stiegler.

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
11,590
2,000
1550229601450.png

Eneo la mto Rufiji kama ionekanavyo kutoka angani.

Pamoja na kelele nyingi zinazoendelea za kutaka kuishinikiza serikali ya Tanzania kuachana na mradi huo, mkandarasi Arab Contractors na El Sewedy Electric wamekabidhiwa rasmi eneo la ujenzi.

Jana maofisa wa serikali ya Tanzania na wawakilishi wa mkandarasi huyo walikabidhishana makabrasha ya kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa mradi huo katika eneo la mto Rufiji ambapo umeme wa kiasi cha megawati 2115 utazalishwa.

Akikabidhi rasmi eneo hilo la ujenzi waziri wa nishati Dr Menard Kalemani alisema mradi huo umekuwa unasubiriwa kwa hamu na serikali ili utapokamilika tatizo la umeme kwa nchi ya Tanzania itakuwa ni historia.

Dr Kalemani alimkumbusha mkandarasi huyo kuhakikisha anafuata makubaliano ya mkataba kwa kumaliza ujenzi wa mradi huo kwa wakati ulopangwa bila kuchelewa.

Mradi huo utapokamilika Tanzania itakuwa ni nchi inayoongoza barani Afrika kwa uzalishaji umeme na katika eneo lote la Afrika mashariki na hilo litakuwa ni bwawa la nne kwa ukubwa barani humo.

Bwawa kubwa kabisa barani Afrika ni la Renaissance lililopo nchini Ethiopia ambalo halijakamilka kujengwa, likifuatiwa na mabwawa ya Mambira lililopo nchini Nigeria, Shaka la nchini Ethiopia na bwawa la Aswan lililopo nchini Misri.

1550229659071.png

Nae mwakilishi wa mkandarasi huyo bwana Waheed Hamde alimhakikishia waziri kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kwa wakati ulopangwa na kwa viwango vya kimataifa bila kujali changamoto zitakazokuwepo.

Kwanini eneo hili laitwa Stiegler Gorge?

Jina la Stiegelr Gorge ni jina la mtafiti wa kutoka nchini Switzerland ambae alifariki kwenye eneo hilo mwaka 1907 eneo lenye kina cha mita 100 alipouawa na tembo au kuanguka.

Eneo hili ni kama shimo au kwa kiingereza "canyon" ambalo limechongwa na maji ambalo lipo kati ya miamba.

Eneo hili ni sehemu ya mto Rufiji ndani ya hifadhi ya Selous lenye urefu wa kilimita 8 na upana wa mita 50.

Inasimuliwa kuwa bwana Stiegler Gorge alikumbana na tembo na akauawa kwa kupondwa kisha kuangukia ndani ya bonde hilo na pia taarifa zingine zinasema alianguka mwenyewe akiwa anajaribu kuvuka eneo hilo akifanya utafiti wake.

Haya twende kazi!!!
 
Aug 5, 2018
74
125
Mwanzo mzuri unapokuwa na vyanzo vya umeme na uwezo mkubwa.uhakika WS power inaboreshwa zaidi. Tupo tutaona mengi na kufaidi. Haya ulaya walienda kwa hatua hizi hizi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom