Apson Mwang'onda, nzi aliyejaribu kubaka demokrasia ya CCM na Tanzania bila ya mafanikio

Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,870
Points
2,000
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,870 2,000
Wadau, amani iwe kwenu.

Jina Apson Mwang'onda si geni kwenye mitandao ya kijamii. Umaarufu wake haukutokana na utendaji kazi wake akiwa kwenye idara nyeti hapa nchini, la hasha. Umaarufu wake haukuonekana akiwa Mkuu wa Idara nyeti bali umeanza kujitokeza miaka miwili kabla ya Tanzania kuingia kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.

Awali ilikuwa kama fununu tu lakini baadaye ikadhihirika kuwa nzi huyo alikuwa akiruka huku na kule kuhakikisha kuwa anaweka watu ambao wataendeleza mfumo mbovu wa kifisadi ndani ya CCM na Tanzania kwa ujumla. Hapana shaka kwamba Watanzania bado wana imani na CCM isipokuwa walichoshwa na aina ya mfumo uliotengenezwa na baadhi ya watu ambao walikuwa wanatumia fedha nyingi kupata viongozi. Matokeo yake CCM ikaanza kupoteza mwelekeo kwa vile wale wafadhili wa mfumo huo ndio waliokuwa wanaendesha chama na serikali.

Mapinduzi yaliyofanywa ndani ya chama mwaka 2007 na kusababisha baadhi ya watu kujivua magamba huku wengine wakikaidi kufanya hivyo ndiyo yaliyomshtua Apson. Apson alishtuka hasa baada ya marafiki wake wakuu ambao ni Rostam Aziz, Edward Lowasa, Nazir Karamagi, Andrew Chenge na wengineo ndio waliotakiwa kujivua hayo magamba. Naam, Rostam alijivua gamba ila Lowasa akashindwa kufanya hivyo kwa ushauri wa Apson. Apson aliona kuwa ikiwa Lowasa atajivua gamba, ndoto yake ya kwenda Ikulu itakuwa imeyeyuka. Hivyo akamshauri kuwa akomae na hivyo kujikuta akisakamwa mara kwa mara na watetezi wa chama na waliochoshwa na siasa chafu ndani ya chama hicho kama vijana machachari Nape Nnauye, Paul Makonda pamoja na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti Philip Mangula.

Ili kuonesha kuwa Apson alikusudia kumuweka mtu wake ambaye atalinda maslahi yake kutokana na ukwapuzi aliofanya akiwa Mkurugenzi ndani ya Idara hiyo, nyumba yake ndiyo iliyokuwa inatumika kufanya vikao vya kuratibu mkakati wa Lowasa kwenda Ikulu. Kama hiyo haitoshi, yeye mwenyewe akajipachika cheo cha Mwenyekiti wa Kamati ya Wezesha Lowasa aende Ikulu.

Nyumba ya Apson pamoja na Hotel ya Sea Cliff ya Dar es Salaam ndio mahala palipokuwa panatumika kupanga mikakati yote ovu pamoja na kupeana mabulungutu ya fedha ambazo zilikuwa zinatumika kuwarubuni wajumbe wa vyombo vya maamuzi ndani ya CCM kama vile wajumbe wa Halmashauri Kuu, Kamati Kuu, Sekretarieti na Mkutano Mkuu. Pia maburungutu hayo yalitumika kuhonga baadhi ya viongozi wa dini ili watumie nyumba za ibada kumnadi mwanasiasa huyo. Habari zote hizi zilikuwa zinaripotiwa humu na vijana waliojitolea kupambana na mafisadi ijapokuwa wapo waliokuwa wanabeza ukweli wa taarifa hizo.

Baada ya mkakati wa Apson ndani ya CCM kukwama na Lowasa kuchinjiwa baharini wakati wa mchujo wa kumpata mgombea Urais ndani ya chama hicho, alimshauri ahamie upinzani. Lowasa bila ya kutafakari madhara yake aliamua kujitosa mzima mzima. Mikakati ya Apson baada ya Lowasa kuhamia upinzani ilikuwa kuhakikisha wanafanikiwa kurubuni Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili waweze kuchakachua matokeo. Wapo baadhi ya Wakurugenzi wa Tume hiyo ambao waliingia kwenye majaribu ya Apson. Mfano halisi ni Mkurugenzi wa IT ambaye alitengewa burungutu kubwa.

Hata hivyo, mkakati huo ulikwama baada ya Mkurugenzi huyo kusimamishwa kutokana na ubadhilifu mkubwa aliofanya wakati wa ununuzi wa mashine za BVR. Apson likamshuka. Maji yakamfika shingoni. Hata hivyo hakukata tamaa. Akaingia mkenge kwa kusaka vijana wenye weledi na masuala ya IT kutoka ndani na nje ya nchi. Wakafanikiwa kuwapata vijana hao wengi kutoka Tanzania na wengine wakitoka Kenya, Ufaransa, Marekani, Canada na Korea.

Wataalam hao wa IT kwa maelekezo ya Apson wakafanikiwa kuhack mfumo wa Tume na wakafanikiwa kuingiza data zao ili kumbeba Lowasa. Pia data hizo ziliwabeba baadhi ya wabunge wa Dar es Salaam kama Halima Mdee, Saed Kubenea na John Mnyika.

Mungu si Athuman. Wasamaria wema wakatoa taarifa polisi kuwa kuna vijana ambao hawaeleweki wapo kwenye hoteli kadhaa Dar es Salaam hasa maeneo ya Sinza, Kijitonyama na Masaki. Taarifa hizo ndizo zilizofanikisha kukamatwa kwa vijana wale 191 wakiwa na laptop na simu zinazofanana. Wakatiwa nguvuni na vitendea kazi vyao kutaifishwa.

Baada ya hapo mchezo ukamalizika. Hakika Lowasa, Apson na genge lake wameumia sana kukamatwa kwa wale vijana maana ndio lilikuwa tegemeo lao la mwisho. Kutokana na kukamatwa kwa vijana wale, matakwa halisi ya wananchi yakaanza kujionesha baada ya Magufuli kushinda katika maeneo mengi hata yale ngome ya UKAWA.

Kwa sasa Apson na genge lake wanajuuta kwa upuuzi waliofanya. Hawajui wafanye nini. Lowasa amenuna. Rostam kawakasirikia kwa vile wamekula fedha zake nyingi bila ya mafanikio. Na nasikia kuwa ameapa kula nao sahani moja kwa hasara waliyomsababishia.

Hakika Mungu alikuwa na mpango wake kwa Watanzania. Tumempata Rais ambaye alikuwa anapambana na watu ambao walijiequip kwa kila hali.
 
MSUMARI WA MOTO

MSUMARI WA MOTO

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2015
Messages
461
Points
250
MSUMARI WA MOTO

MSUMARI WA MOTO

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2015
461 250
Tunataka JECHA ajiuzulu kwanza. Porojo baadaye!
 
Zagazaga

Zagazaga

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2011
Messages
563
Points
250
Zagazaga

Zagazaga

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2011
563 250
Huna lolote ccmmm imeshinda kwa wizi kila mtu anslijua hilo... lowasa kawatoa kamasi vibaya sana...hapa unaleta maneno ili kujustify wizi wenu... kama taarifa zote milikua nazo vyombo vya ulinzi vilifanya nn!?? Ww unafurahi lowasa kukosa urais sababu uliempenda.. meembe alikosa.. hamna zaidi ya hilo... wizi umejionyesha wazi wazi..hata yaliyotokea zanziba yanathibisha wizi wenu ulio kubuhu
 
M

mikeimani

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2015
Messages
2,687
Points
2,000
M

mikeimani

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2015
2,687 2,000
Aibu. Kama kweli bosi wa usalama wa taifa anaweza kuwa na akili za aina hiyo.

Vipi, hakuchukunguzwa kabla hajawa bosi wa idara hiyo?
 
Lambert Mende

Lambert Mende

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Messages
210
Points
195
Lambert Mende

Lambert Mende

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2015
210 195
Lizaboni
Mpeni muda magufuli afanye kazi,acheni majungu yenu,uchaguzi umeshaisha,mlipopiga mmepga basi
 
Last edited by a moderator:
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,870
Points
2,000
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,870 2,000
Aibu. Kama kweli bosi wa usalama wa taifa anaweza kuwa na akili za aina hiyo.

Vipi, hakuchukunguzwa kabla hajawa bosi wa idara hiyo?
Inawezekana aliyemteua alikuwa na dhamira njema. Ila watu wanabadirika. Ni kama Mkapa alipomteua Sumaye kuwa Waziri Mkuu lakini sasa anasema kuwa CCM haijafanya lolote kwa miaka 50
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
34,131
Points
2,000
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
34,131 2,000
Shikamoo Lizaboni.
 
O

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Messages
10,945
Points
1,225
O

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined May 24, 2008
10,945 1,225
Lizaboni Uchaguzi umeisha Mkuu... Kuendeleza haya mapambano ya matusi, kejeli, kashfa hayatasaidia Taifa kurudi katika umoja wa awali...

Haya mambo kwa sasa hayana nafasi. Lets focus kwenye kujenga nchi na kuziba ufa uliojitokeza
 
Last edited by a moderator:
Lambert Mende

Lambert Mende

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Messages
210
Points
195
Lambert Mende

Lambert Mende

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2015
210 195
Inawezekana aliyemteua alikuwa na dhamira njema. Ila watu wanabadirika. Ni kama Mkapa alipomteua Sumaye kuwa Waziri Mkuu lakini sasa anasema kuwa CCM haijafanya lolote kwa miaka 50
Mkuu Lizaboni
Hivi Mzee kitine nae kugombea urais kapitia Ccm ilikuwa ni halali?
Kabla ya kutoa shutuma tujiongeze kidogo,mm bado nasema kuwa,uchaguzi umeisha tubaki wamoja,tumpe muda mh magufuli afanye kazi,watu waaache kuchokoana kila wakati
 
Last edited by a moderator:
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,870
Points
2,000
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,870 2,000
Uchaguzi umeisha Mkuu... Kuendeleza haya mapambano ya matusi, kejeli, kashfa hayatasaidia Taifa kurudi katika umoja wa awali...

Haya mambo kwa sasa hayana nafasi. Lets focus kwenye kujenga nchi na kuziba ufa uliojitokeza
Mkuu, kushinda uchaguzi ni hatua moja tu ya mapambano. Hujui hawa mafisadi wanawaza nini.
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,870
Points
2,000
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,870 2,000
Mkuu Lizaboni
Hivi Mzee kitine nae kugombea urais kapitia Ccm ilikuwa ni halali?
Kabla ya kutoa shutuma tujiongeze kidogo,mm bado nasema kuwa,uchaguzi umeisha tubaki wamoja,tumpe muda mh magufuli afanye kazi,watu waaache kuchokoana kila wakati
Kitine alitumia demokrasia yake kihalali. Hawa akina Apson walikuwa wanabaka demokrasia. Ndo maana wakawa na mikakati ovu kila uchwao.
 
Lambert Mende

Lambert Mende

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Messages
210
Points
195
Lambert Mende

Lambert Mende

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2015
210 195
Kitine alitumia demokrasia yake kihalali. Hawa akina Apson walikuwa wanabaka demokrasia. Ndo maana wakawa na mikakati ovu kila uchwao.
Hahahaha,demokrasia ipi iliyobakwa?
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,870
Points
2,000
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,870 2,000
Hahahaha,demokrasia ipi iliyobakwa?
Mkuu, kwa upande wako unaona Apson alikuwa sahihi kuhonga wajumbe wa NEC, CC na MM ili tu Lowasa awe Rais? Pia unaona kuwa Apson alikuwa sahihi kuajiri vijana wa IT ili wahack mfumo wa Tume?
 
Hot Lady

Hot Lady

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Messages
1,035
Points
1,250
Hot Lady

Hot Lady

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2014
1,035 1,250
Magufuli anza na Apson Mwang'onda kwenye mapambano yako dhidi ya ufisadi. Hakika tutakupa ushirikiano stahiki
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
34,131
Points
2,000
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
34,131 2,000
Marhana mkuu GENTAMYCINE. ​ Tulikuwa pamoja kwenye haya mapambano
Na Ndiyo WAKAJIFUNZE Ni Kwanini TANZANIA Ni Ya 2 Ktk UJASUSI Barani AFRICA Na Ni Ya 10 Ktk UJASUSI ULIOTUKUKA Duniani. Mkuu LIZABONI Nitoe Breaking News Ya UKAWA Iliyotokea Sasa au Na Wewe UMESHAIPATA Nikuache Uitoe? Wanajifanya KUWAFICHA Watu Waliowadanganya ILA Kuna Kitu Huko Kimetokea Jana Usiku Na Kingine Kimemalizika Kutokea Muda Si Punde Na Najua Kwa UTUNDU Na UELEDI Wako Na Wewe UMESHAKINYAKA Mkuu au Bado? Siku 7 au 21 Zijazo Hutokuja Tena KUUSIKIA Huo Muungano Wao Kwa Hiki Kilichotokea Jana Na Hivi Punde Na Kuna Bonge La FUKUTO Huko Sasa. Hakika CCM Ni Habari Nyingine!
 

Forum statistics

Threads 1,343,136
Members 514,956
Posts 32,774,818
Top