Elections 2015 Apson Mwang'onda afanya vikao vya kuchangisha fedha Oysterbay ili Lowasa ahamie CHADEMA

Huu ni wakati wa kusikia mambo mengi sana ila mwisho wa siku hakuna jipya litakalotokea maana kama Lowassa kapigwa chini huko kwenye chama cha aistegemee kutoka kwenye muungano wa vyama hivi vinne labda amtafute ZZK na chama chake ACT.
Hahahahahahahaaaaaaa! Kwenye siasa kila kitu kinawezekana
 
Hapo ndo amechemka kwenye hadithi yake,
Tunajua ukweli ni riz1 + manji+ membe= ubunge wa kigamboni aliohidiwa manji endapo membe angepita.

Hivi mkuu wa wilaya badala ya kufanya majukumu ya ofisi anapata wapi muda wa kufanya huu utunzi na kumuinbox lizaboni asambaze?

Mkuu, anachofanya Lizaboni ni ku provide kile ambacho vitani kinaitwa fire cover. Fire cover hufanyika pale mwenzenu anapojitolea au anapotakiwa kwenda upande waliopo adui zenu au anaporudi. Lengo la Fire cover ni kuaminisha maadui adui zenu kwamba mnamshambulia yule anayekimbia (yaani mwenzenu) au munashambulia maadui ili wakose nafasi ya kumdhuru mwenzenu.
Hivyo, binafsi ninawakubali sana Lizaboni na Chabruma kwa namna ambayo wamekua wakitoa fire cover kwa muda wote kwa lengo la kumlinda Mzee Apson kitu kilichosaidia upande mwingine kujenga trust kwa jamaa na kumuwezesha kujikita ndani zaidi.
Other wise, bila hizo fire cover akina Lowasa wangesham red Apson kitambo sana
 
Last edited by a moderator:
Bilioni 252 CAG Alishazitolea maelezo ndugu,ukipenda siasa ifuatilie na kuisoma siyo kukurupuka tu na story za kwenye shoe shine
 
Jamani Lowasa akiteuliwa na chama chochote hawezi kupitishwa na Tume ya Kuchaguzi kwa kuwa alishaanza kampeni mapema kabla ya muda wake. Safari yake yote ya kutafuta wadhamini alifanya mikutano ya wazi ya kujiombea kura kwa wananchi wakati muda wa kampeni bado
 
Jamani Lowasa akiteuliwa na chama chochote hawezi kupitishwa na Tume ya Kuchaguzi kwa kuwa alishaanza kampeni mapema kabla ya muda wake. Safari yake yote ya kutafuta wadhamini alifanya mikutano ya wazi ya kujiombea kura kwa wananchi wakati muda wa kampeni bado
Lowasa anahangaika tu
 
IMG_0596.jpg
attachment.php
 
Wadau amani iwe kwenu.

Taarifa nilizopata hivi punde kutoka kwa mdau wangu zinasema kuwa Apson Mwang'onda, Mwenyekiti wa Wezesha Lowasa Aende Ikulu ameanza vikao vya kuwashawishi baadhi ya wafanyabiashara wachangishe fedha ambazo zitawezesha kukamilisha deal la Lowasa kuhamia CHADEMA. Inadaiwa kuwa Apson ameamua kufanya hivyo baada ya Lowasa kutoswa ndani ya chama chake, CCM ambapo alishindwa hata kufika Tano Bora.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, wafadhili wakuu wa Lowasa ambao ni Nazir Karamagi, Rostam Aziz, Reginald Mengi na Yusuph Manji wamesitisha kuendelea kutoa fedha baada ya jitihada zao za kuhakikisha Lowasa anapeperusha Bendera ya CCM kukwama. Kwamba, wafadhili hao wametumia zaidi ya shilingi Bilioni 50 ambazo hata hivyo manufaa yake hayajapatikana. Kutokana na hali hiyo, wafadhili hao wametoa masharti kwamba ni lazima jitihada zifanyike ili Lowasa ahamie CHADEMA na ateuliwe kupeperusha bendera ya UKAWA ndipo waendelee kutoa fedha. Kwamba, kwa vile Lowasa ameonesha nia ya kutafuta mabadiliko nje ya CCM baada ya jitihada za ndani kukwama, wao hawana tatizo ikiwa Apson atawahakikishia kuwa kuhamia kwa Lowasa CHADEMA kutaenda sambamba na kupeperusha bendera ya UKAWA kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Kwa mujibu wa chanzo changu tayari Apson amefanya kikao na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wamekubaliana kwamba, ili Lowasa ahamie CHADEMA na hatimaye kupeperusha Bendera ya UKAWA, MBOWE apewe shilingi bilioni kumi ili afanikishe mpango huo. Kwamba, ikiwa fedha hizo zitapatikana, Mbowe atashawishi viongozi wenzake ndani ya CHADEMA na UKAWA ili wampokee Lowasa na kwamba ikiwa deal hilo litafanikiwa kabla ya mwezi wa Nane, Lowasa ndiye atakayepeperusha Bendera ya UKAWA. Aidha, taarifa zinasema kuwa ikiwa viongozi wa UKAWA hawataafiki mpango wa Lowasa kupeperusha bendera ya UKAWA, CHADEMA itajitoa ndani ya umoja huo na kwamba itawafukuza viongozi wake ambao wataonesha kupinga mpango huo.

kutokana na masharti hayo, Apson Mwang'onda ameamua kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kufanikisha mpango huo. Majira ya mchana wa leo, Apson Mwang'onda amekutana na mmiliki wa Supermarket za ( TSN), Farouk Bonghoza kwenye moja ya maduka yake yaliyopo Oysterbay Shopping Center, Kinondoni Dar es Salaam. Aidha, Apson pia amepanga kukutana na wafanyabiashara wengine na kwamba ana matumaini kuwa kiasi hicho cha fedha kitapatikana ndani ya wiki hii kwa vile anayo akiba zaidi ya bilioni tano ambazo zilipangwa kutumika wakati wa kampeni na bado zipo kwenye akaunti maalum iliyofunguliwa kwa madhumuni hayo.

Wadau, huyu ndiye Apson Mwang'onda, shushushu ambaye ameamua kwa kila njia kuhakikisha kuwa fisadi anaingia Ikulu. Kwa sasa anahaha kuhakikisha kuwa fedha hizo bilioni 10 zinapatikana ili kufanikisha deal hilo. Wakati Apson anahaha kutafuta fedha hizo, taarifa zinasema kuwa tangu juzi hawajawasiliana na Lowasa. Kwamba, Lowasa amemnunia Apson kutokana na hapo awali alihakikishiwa kuwa njia ni nyeupe ya kwenda Ikulu na sasa ameshangaa kuona ameshindwa hata kufika tano bora.

APSON MWANG'ONDA AKIWA NA FAROUK BONGHOZA LEO OYSTERBAY SHOPPING CENTER
View attachment 267808

Hivi SSIT Mnashindwa Na Mnachelewa Nini Kum Imran Kombe Na Huyu Mzee? Anawashindeni Nini? Mnamwogopea Nini? Huyu Mzee Baba Jimmy Anaitakia Nini Tanzania? Mzee Amekaa KINAFIKI Na KIFUJOFUJO Tu Halafu Anashindwa Hata Kujishtukia. Magufuli Tafadhali Ukiingia Tu Madarakani Anza Na TAKATAKA Hii Kwani Ni Kirusi Kisichotakiwa KULELEWA Tanzania. Nimemdharau KULIKOTUKUKA Huyu Mzee!
 
Hivi SSIT Mnashindwa Na Mnachelewa Nini Kum Imran Kombe Na Huyu Mzee? Anawashindeni Nini? Mnamwogopea Nini? Huyu Mzee Baba Jimmy Anaitakia Nini Tanzania? Mzee Amekaa KINAFIKI Na KIFUJOFUJO Tu Halafu Anashindwa Hata Kujishtukia. Magufuli Tafadhali Ukiingia Tu Madarakani Anza Na TAKATAKA Hii Kwani Ni Kirusi Kisichotakiwa KULELEWA Tanzania. Nimemdharau KULIKOTUKUKA Huyu Mzee!
Naona umeamua kutoa ya moyoni. Mie simo
 
Back
Top Bottom