Apson Mwang'onda afanya vikao vya kuchangisha fedha Oysterbay ili Lowasa ahamie CHADEMA

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,870
Points
2,000

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,870 2,000
Wadau amani iwe kwenu.

Taarifa nilizopata hivi punde kutoka kwa mdau wangu zinasema kuwa Apson Mwang'onda, Mwenyekiti wa Wezesha Lowasa Aende Ikulu ameanza vikao vya kuwashawishi baadhi ya wafanyabiashara wachangishe fedha ambazo zitawezesha kukamilisha deal la Lowasa kuhamia CHADEMA. Inadaiwa kuwa Apson ameamua kufanya hivyo baada ya Lowasa kutoswa ndani ya chama chake, CCM ambapo alishindwa hata kufika Tano Bora.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, wafadhili wakuu wa Lowasa ambao ni Nazir Karamagi, Rostam Aziz, Reginald Mengi na Yusuph Manji wamesitisha kuendelea kutoa fedha baada ya jitihada zao za kuhakikisha Lowasa anapeperusha Bendera ya CCM kukwama. Kwamba, wafadhili hao wametumia zaidi ya shilingi Bilioni 50 ambazo hata hivyo manufaa yake hayajapatikana. Kutokana na hali hiyo, wafadhili hao wametoa masharti kwamba ni lazima jitihada zifanyike ili Lowasa ahamie CHADEMA na ateuliwe kupeperusha bendera ya UKAWA ndipo waendelee kutoa fedha. Kwamba, kwa vile Lowasa ameonesha nia ya kutafuta mabadiliko nje ya CCM baada ya jitihada za ndani kukwama, wao hawana tatizo ikiwa Apson atawahakikishia kuwa kuhamia kwa Lowasa CHADEMA kutaenda sambamba na kupeperusha bendera ya UKAWA kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Kwa mujibu wa chanzo changu tayari Apson amefanya kikao na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wamekubaliana kwamba, ili Lowasa ahamie CHADEMA na hatimaye kupeperusha Bendera ya UKAWA, MBOWE apewe shilingi bilioni kumi ili afanikishe mpango huo. Kwamba, ikiwa fedha hizo zitapatikana, Mbowe atashawishi viongozi wenzake ndani ya CHADEMA na UKAWA ili wampokee Lowasa na kwamba ikiwa deal hilo litafanikiwa kabla ya mwezi wa Nane, Lowasa ndiye atakayepeperusha Bendera ya UKAWA. Aidha, taarifa zinasema kuwa ikiwa viongozi wa UKAWA hawataafiki mpango wa Lowasa kupeperusha bendera ya UKAWA, CHADEMA itajitoa ndani ya umoja huo na kwamba itawafukuza viongozi wake ambao wataonesha kupinga mpango huo.

kutokana na masharti hayo, Apson Mwang'onda ameamua kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kufanikisha mpango huo. Majira ya mchana wa leo, Apson Mwang'onda amekutana na mmiliki wa Supermarket za ( TSN), Farouk Bonghoza kwenye moja ya maduka yake yaliyopo Oysterbay Shopping Center, Kinondoni Dar es Salaam. Aidha, Apson pia amepanga kukutana na wafanyabiashara wengine na kwamba ana matumaini kuwa kiasi hicho cha fedha kitapatikana ndani ya wiki hii kwa vile anayo akiba zaidi ya bilioni tano ambazo zilipangwa kutumika wakati wa kampeni na bado zipo kwenye akaunti maalum iliyofunguliwa kwa madhumuni hayo.

Wadau, huyu ndiye Apson Mwang'onda, shushushu ambaye ameamua kwa kila njia kuhakikisha kuwa fisadi anaingia Ikulu. Kwa sasa anahaha kuhakikisha kuwa fedha hizo bilioni 10 zinapatikana ili kufanikisha deal hilo. Wakati Apson anahaha kutafuta fedha hizo, taarifa zinasema kuwa tangu juzi hawajawasiliana na Lowasa. Kwamba, Lowasa amemnunia Apson kutokana na hapo awali alihakikishiwa kuwa njia ni nyeupe ya kwenda Ikulu na sasa ameshangaa kuona ameshindwa hata kufika tano bora.

APSON MWANG'ONDA AKIWA NA FAROUK BONGHOZA LEO OYSTERBAY SHOPPING CENTER
image.jpg
 

Lyimo

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
3,825
Points
1,225

Lyimo

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
3,825 1,225
Mwaka huu watunzi wengi wa hadithi watapata umaarufu. Ni heri huyu muheshimiwa akapumzika kwanza na kuacha kutapanya pesa pasipo kuwa na mafanikio. Ninahakika kama atahitaji kugombea URAIS tu, basi kuna vyama vingine vingeweza kumkaribisha bila senti tano na labda kumpatia nafasi hiyo aliyoikamia kupita maelezo.
 

Tetty

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
26,396
Points
2,000

Tetty

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2012
26,396 2,000
Lizaboni Mamvi au Mapadlock amekulipa ngapi kwa kupotosha watu?Najua mnatafuta kura lakini siyo kwa kuharibu taswira ya vyama vya upinzani kwa sababu ya vijisenti vidogo unavyopew.Bila CCM/Lowassa Tanzania inawezekana.

Huyo Magufuli hana tofauti na huyo Lowassa .Watoto wa mama mmoja baba mmoja.Na amesema fika atalinda maslahi ya watawala waliopita na CCM hajasema atalinda maslahi ya Taifa lake.Kwa uhakika hata wewe wajua hatufai.

Tunahitaji Rais nje ya CCM huyo Lowassa mtafutieni nafasi ACT alikokafibishwa.
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,870
Points
2,000

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,870 2,000
Lizaboni Mamvi au Mapadlock amekulipa ngapi kwa kupotosha watu?Najua mnatafuta kura lakini siyo kwa kuharibu taswira ya vyama vya upinzani kwa sababu ya vijisenti vidogo unavyopew.Bila CCM/Lowassa Tanzania inawezekana.

Huyo Magufuli hana tofauti na huyo Lowassa .Watoto wa mama mmoja baba mmoja.Na amesema fika atalinda maslahi ya watawala waliopita na CCM hajasema atalinda maslahi ya Taifa lake.Kwa uhakika hata wewe wajua hatufai.

Tunahitaji Rais nje ya CCM huyo Lowassa mtafutieni nafasi ACT alikokafibishwa.
Mkuu Tetty, nimeripoti uhalisia. Na huu ndio mkakati unaoratibiwa na Apson Mwang'onda.
 

Forum statistics

Threads 1,344,385
Members 515,452
Posts 32,818,906
Top