APRM yaipaisha Tanzania kidemokrasia, kiuchumi

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
MPANGO wa Tathmini ya Utawala Bora katika Bara la Afrika (APRM), umebaini kuwepo kwa mafanikio makubwa nchini Tanzania, kwa kuimarisha demokrasia, usimamizi wa uchumi na huduma jamii. Pia mpango huo unatajwa kufanya vyema katika maeneo mengine, yakiwemo ya uendeshaji wa mashirika ya biashara, ambako zaidi Tanzania inasiwa katika eneo la usimamizi wa rasilimali ya ardhi na madini.

Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau kutathimini mpango huo, ulioanzishwa miaka 16 iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi alisema mpango huo umeonesha Tanzania kuwa na mafanikio makubwa katika usimamizi wa utawala bora.

Profesa Kabudi alisema mafanikio hayo yanatokana na umoja na ushirikiano uliopo baina ya wananchi wa Tanzania na viongozi wa serikali, hatua iliyoiwezesha kuwa moja ya nchi zilizofanya vizuri. “Tanzania kwa miaka mingi tumekuwa na utawala bora, ni juhudi zilizofanywa na Rais Magufuli nasi tunaziendeleza, mafanikio haya yanatokana na juhudi zetu wenyewe kama serikali chini ya uongozi madhubuti,” alisema Profesa Kabudi.

Alisema tathmini hiyo ya miaka 16, imeangalia pia maeneo mengi muhimu yakiwepo ya huduma za jamii za elimu bure, maji, afya ikiwepo ujenzi wa zahanati na upatikanaji wa huduma za afya. Mtaalamu wa masuala ya kutathmini utawala bora kutoka APRM, Dk Rehema Twalib alisema Tanzania imekuwa ni nchi ya mfano kwenye maeneo ya demokrasia baada ya kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uchumi, sera na mipango mizuri, na kwenye eneo la biashara ikiwepo kwenye sekta binafsi.

Dk Twalib alisema katika kufanikisha mpango huo, Tanzania imepiga hatua kubwa kiasi cha kuiwezesha kutambulika miongoni kwa nchi 33 zinazotekeleza mpango huo Afrika.

APRM ni Mpango wa tathmini ya utawala bora katika Bara la Afrika, wenye lengo la kuangazia nchi hizo na kufanya tathmini kwenye masuala mbali mbali ya huduma za jamii
 
Back
Top Bottom