Aprili 26, 1964 ni siku ya hasara kwa Wazanzibari

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
776
1,121
" DAY OF LOSS"
---SIKU YA HASARA---

1) Tarehe 26/4/1964 ndio siku ambayo Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ikiuwawawa ( state death).

2. Tarehe 26/4/1964 ndio siku ambayo wazanzibar walipoteza mamlaka ( sovereignty) ya nchi yao.

3).Tarehe 26/4/1964 ndio siku ambayo Wazanzibar walipoteza uraia ( citizenship) wao wa Zanzibar.

4). Tarehe 26/4/1964 ndio siku ambayo Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar alikoma ( cease) kuwa Amiri Jeshi Mkuu.

5) Tarehe 26/4/1964 ndio siku ambayo Wanzanzibar walipoteza kiti chao Umoja wa MATAIFA.

--ZANZIBAR IMETOKA KUWA DOLA HADI KUWA MKOA--

-- UZANZIBAR UMETOKA KATIKA HADHI YA URAIA HADI KUWA UKAAZI ( Raia wa Zanzibar hadi Mzanzibari mkaazi)

--Kutoka Amiri Jeshi Mkuu hadi Kamanda Mkuu wa Idara maalumu--

-- Kutoka Rais wa Dola ya Zanzibar hadi Waziri asiye na Wizara maalumu--

--ZANZIBAR kutoka mwanachama wa Umoja wa Mataifa kukataliwa kujiunga na FIFA

TAREHE 24/4/1964 ni SIKU YA HASARA (DAY OF LOSS) KWA WAZANZIBAR

HAKUNA KITU CHOCHOTE DUNIANI KINACHOWEZA KUFIDIA WAZANZIBAR KUPOTEZA UTAIFA WAO WA ZANZIBAR

HAKUNA KITU CHOCHOTE DUNIANI KINACHOCHEZA KUFIDIA WAZANZIBAR KUPOTEZA DOLA YAO JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR

HAKUNA KITU CHOCHOTE DUNIANI KINACHOWEZA KUFIDIA WAZANZIBAR KUPOTEZA URAIA WAO WA ZANZIBAR

HAKUNA KITU CHOCHOTE DUNIANI KINACHOWEZA KUFIDIA WAZANZIBAR KUPOTEZA UTAMBULISHO WA DOLA YAO

HAKUNA KITU CHOCHOTE DUNIANI KILICHOWEZA--KINACHOWEZA AU KITAKACHOWEZA KUFIDIA HASARA WALIYOIPATA WAZANZIBAR TAREHE 26/4/1964

SIKU YA MAOMBOLEZI
 
Poleni sana waZanzibar. Naomba kama unaweza utuwekee hapa ramani ya mipaka halisi ya Jamhuri ya Zanzibar ilivyokuwa kabla ya mamlaka yake kutwaliwa na Tanganyika kwa kivuli cha Tanzania? Maana nimesoma shule zote sijawahi kuona mipaka ilivyokuwa baina ya Zanzibar na Tanganyika (pamoja na Kenya labda?)
 
Wazanzibar kwa kunung'unika! Sasa mbona sisi Watanganyika tunafaidika kiduchu sana na huo Muungano kuliko mnavyofaidika ninyi! Hivi ikatokea huo Muungano ukavunjika leo, hivi ni nani hasa atayepoteza zaidi!

Tuwape nini ili mridhike ndugu zetu? maana tunawapenda sana na kutengana kabisa haiwezekani mpaka hapa tulipofikia.
 
Mtulie hivyo hivyo..tangu lini sikio likazidi kichwa ukubwa..bora muungano kuliko utengano sema muundo wa muungano ndio umekaa hovyo.

#HappyMuunganoDay
 
Wazanzibar kwa kunung'unika! Sasa mbona sisi Watanganyika tunafaidika kiduchu sana na huo Muungano kuliko mnavyofaidika ninyi! Hivi ikatokea huo Muungano ukavunjika leo, hivi ni nani hasa atayepoteza zaidi!

Tuwape nini ili mridhike ndugu zetu? maana tunawapenda sana na kutengana kabisa haiwezekani mpaka hapa tulipofikia.
Sasa kama hamufaidiki kwanini mnawang'ang'ania ?
 
Wazanzibar kwa kunung'unika! Sasa mbona sisi Watanganyika tunafaidika kiduchu sana na huo Muungano kuliko mnavyofaidika ninyi! Hivi ikatokea huo Muungano ukavunjika leo, hivi ni nani hasa atayepoteza zaidi!

Tuwape nini ili mridhike ndugu zetu? maana tunawapenda sana na kutengana kabisa haiwezekani mpaka hapa tulipofikia.
Kwani Zanzibar inapata nini hasa? Budget yote ya Tanzania inaishia Tanganyika, Zanzibar kinachokuja ni mishahara tu wafanyakazi wa chini ya Muungano ambao ni majeshi na askari na wapo huku Zanzibar kwa lengo la kulinda koloni Lao.
 
Kama mmeshazika kila kitu si mjisalimishe tu muachane na malalamiko. Ivi kuwa Mzanzibar kuna faida gani zaid ya kua Mtanzania?
 
Wazanzibar kwa kunung'unika! Sasa mbona sisi Watanganyika tunafaidika kiduchu sana na huo Muungano kuliko mnavyofaidika ninyi! Hivi ikatokea huo Muungano ukavunjika leo, hivi ni nani hasa atayepoteza zaidi!

Tuwape nini ili mridhike ndugu zetu? maana tunawapenda sana na kutengana kabisa haiwezekani mpaka hapa tulipofikia.
Tupeni Nchi yetu ni hilo tuu
 
Ingieni msituni mfanye Mapinduzi tena...muikomboe Zanzibar yenu. Si mnapenda kujitenga.
 
No hii sio siku ya hasara ni siku ya faida kubwa sana kwa Wazanzibari na Tanzania kwa ujumla.

Hii ndio siku ya kuzaliwa kwa taifa jipya la Tanzania baada ya kifo cha Jamuhuri Tanganyika na Jamuhuri ya Watu wa Zanzibar na kuunda taifa jipya la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
P
 
" DAY OF LOSS"
---SIKU YA HASARA---

1) Tarehe 26/4/1964 ndio siku ambayo Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ikiuwawawa ( state death).
SIKU YA MAOMBOLEZI
Yes ni siku ambayo Jamuhuri ya Watu wa Zanzibar ilikufa rasmi kifo cha kujitakia, a voluntary death ili kukiua kijijamhuri kidogo, kiduchu na kujiunga na Lijamuhuri likubwa la JMT. Hivyo Zanzibar kupoteza kijijamhuri chake kidogo kiduchu na kujiunga na Lijamuhuri likubwa la JMT, hivyo Zanzibar ndio imegain.
P
 
" DAY OF LOSS"
---SIKU YA HASARA---
2. Tarehe 26/4/1964 ndio siku ambayo wazanzibar walipoteza mamlaka ( sovereignty) ya nchi yao.
SIKU YA MAOMBOLEZI
Ni kweli Zanzibar ilipoteza kiji sovereignty chake kidogo kiduchu na kugain lisovereignity likubwa la JMT. Ukiwa na ki sovereignty kidogo kiduchu inakuwa na mamlaka madago maduchu na kisauti kidogo kiduchu, lakini ndani ya ji sovereignty jikubwa Zanzibar imepata sauti kubwa, mamlaka makubwa, hiyo Zanzibar ime gain.

P.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom