April 7 na mauaji ya kimbari na mchangowa viongozi wa dini

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,561

APRIL 7 YA MAUAJI YA KIMBARI, NA MCHANGO WA VIONGOZI WA DINI KATIKA MAUAJI HAYO
.​

Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255784482959.

Ifikapo tarehe 1/April ya pasaka zitakuwa zimebaki siku 6 ili dunia ikumbuke na kuadhimisha mauaji mabaya kabisa ya kimbari ya Rwanda ya 1994.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha San Diego Timothy Longman katika kitabu chake 'CHURCH POLITICS AND THE GENOCIDE IN RWANDA' anaandika kuwa, mzizi wa mauaji ya Rwanda haukuwa ukabila bali uchochezi wa ukabila.

Anasema, utofauti wa ukabila ulikuwepo mda mrefu na watu waliishi vizuri, na sasa miaka hii ambapo Rwanda kuna amani bado watu hawajajivua kabila zao na bado tunaona amani kubwa.

Anasema, tatizo lilikuwa kuhubiri ukabila kulikoanzishwa na baadhi ya makanisa kwa sura ya kuwa WANAKEMEA UOVU katika jamii huku wakipanda mbegu mbaya ya utengano, taharuki na kutoaminiana baina ya Watutsi na Wahutu.

Anasema katika uk. wa 101 kuwa , kanisa liliacha kazi yake ya msingi(basic duty) kuhubiri utangamano na maridhiano( stability & reconciliation) na likajielekeza katika SIASA za kidola na kikabila.

Anasema, kwakuwa asilimia 99 ya Warwanda ni waumini wa makanisani basi mahubiri hayo yaliyokuwa yamepakwa mafuta ya NIA NJEMA yalipenya kwenye nyoyo zao na baadae wakayafanyia kazi na hatimaye matunda yake yakavunwa kwa roho zaidi ya Milioni 1 ndani ya siku 100 tu kuanzia April 7.

Anawataja, Askofu mkuu wa Anglican Kigali Archbishop Justin Nshamihigo, na askofu wa Katoliki Archbishop Vincent Nsengiyumva kuwa maaskofu wenye ushawishi mkubwa nchini Rwanda kipindi hicho.

Anasema hawa walihubiri siasa za ukabila madhabahuni, waliandika nyaraka/waraka, walifanya press conference zisizo na idadi na walipozuiwa na mamlaka kufanya hivyo walikwenda nchini Kenya ambapo walitumia nafasi hiyo kufanya press conference na vyombo vya kimataifa kwa SURA YA KUKEMEA lakini wakipanda mbegu ya utengano ambayo wao leo pia ni wahanga wa mbegu hiyo.

Anasema hawakujua kama na wao pia watakuwa wahanga kwani, Vincent Nsengiyumva aliuawa kwa kuchinjwa yeye, maaskofu 2 na mapadre 13. Naye Justin Nshamihigo anatafutwa mpaka leo na inasemekana kanisa lake Anglican linamficha maeneo ya ulaya anakoishi kwa kuhamahama.

Mwandishi mwingine Anthony Court, katika kitabu 'THE CHRISTIAN CHURCHES, THE STATE AND GENOCIDE IN RWANDA' anasema kukosekana kwa mipaka ya bayana kati ya kazi za dola(state) na zile za kanisa kuliteketeza watu zaidi ya laki 8.

Anamtaja padri Athanase Seromba kuwa amefungwa miaka 15 jela lakini alistahili zaidi. Anasema huyu na wenzake walionywa sana na Makao Makuu Vatican kuhusu hatari ya KANISA KUFANYA SIASA lakini badala ya kuacha walishiriki kuunda kundi la INTERAHAMWE .

Anasema umbali wa DINI na DOLA/SIASA unatakiwa kuwa wa maelfu ya maili kuliko ule wa Mwanafalsafa Aristotle wa nguzo tatu za dola(mahakama,bunge na serikali). Anasema Rwanda dini na siasa zilikaribiana tu, na kama zingesogeleana hadi kugusana pasingebaki kiumbe kinachopumua.

Anasisitiza sana mataifa ya kidemokrasia kuepuka sumu hii kwani vita nyingi duniani tokea karne ya 6 imetokana na kutokuwa na mipaka kati ya DINI na SIASA kuliko sababu nyingine yoyote.

Anasema walioanzisha chokochoko za SIASA na DINI ndio waliokuwa wa kwanza kuuawa. Analitaja kanisa la Gikondo Pallottine Mission ambapo tarehe 9 April siku 2 tu baada ya mauaji kuanza kanisa lilivamiwa na watu 101 walikatwakatwa mapanga.

Anasema ndani mwake walikuwamo wachungaji na mapadre waliokuwa wakosoaji wakubwa wa rais Juvenal Habyarimana ambao walikuwa wakijiandaa kutoa tamko kwenye vyombo vya habari.

MY TAKE# Shime viongozi wetu wapendwa sana wa DINI msitufikishe huko tafadhali. Lakini kama mtaendelea kupuuza miito ya aina hii na mkaona tunafaa kufika huko sawa, wacha tufike, madhali na nyie mko humuhumu tutabanana tu, kwani shida iko wapi.
 
Huku kwetu hakuna hii, ila huwa wanaandika waraka maalumu kila ikifika siku ya kuazimisha! Mfano ni hii ya juzi ya matawi kuelekea pasaka waliandika waraka maalumu kwa mtawala wakieleza mambo mbalimbali wanaokutana nayo mtaani! Ila sio kila siku wanafanya siasa, kingine ni kua huku wanatumia lugha ya taifa na sio kikabila! Sisi hatujafikia huko, ila kwa hali iliopo kwa sasa tunakoelekea ni giza!
 
Viongozi wa makanisa au miskiti ni sauti ya mwisho ya haki Na usawa katika nchi si vinginevyo. Ndiyo mana hata raisi wetu anaombewa au anasisitiza aombewe,, Na sisi tumeomba viongozi wa kidini wasifumbie macho maovu kama mauwaji,haki itendeke.pasiwe Na dhulma, watu wasiojulikana wajulikane nchi inahitaji maombi ya style nyingi sana hata ujenzi wa viwanda ukamilike %100 Na vinginevyo vingi
 
Back
Top Bottom