#COVID19 Approach sahihi kwa Askofu Gwajima ilikuwa kumuandalia mdahalo na wataalamu wa tiba wamjibu hoja zake

Ralph Tyler

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
2,827
3,568
Wamekosea sana kumpeleka kuhojiwa kwenye kamati za vitisho na polisi kwa sababu huko ataibuka mshindi tu kwani hawataweza kujibu hoja zake. Na kwa kuwa wameshamtisha na akaonyesha ushupavu wa kutotishika atazidi kuwa maarufu.

Na wakikosea zaidi wakamuumiza popote, au hata wakimfukuza ubunge, basi hata wale ambao walikuwa hawamwamini watamwamini kwa kigezo cha kwamba serikali inatumia nguvu kulazimisha jambo ovu ndio maana hata anayelipinga wanamsulubu. Atajipatia "ushujaa" kutoka kwa kundi kubwa kuliko awali.

Kwa maoni yangu, approach sahihi kwa issue ya Gwajima kupinga chanjo ya COVID, wangempa nafasi ya kujadiliana na wataalamu wa tiba, siyo na wanasiasa. Wamruhusu kuja na wataalamu wake wanaompa hayo maelezo anayoona kuwa ni ya kitaalamu.

Wampe nafasi ya kumsikia hoja zake zote na aweke mezani evidence zote anazoona zinasupport msimamo wake, kisha watoe nafasi kwa wataalamu kuzijibu huku nao wakiweka evidence zao mezani.

Watoe fursa ya mdahalo kati ya Gwajima na wataalam wake dhidi ya serikali na wataalamu wake, mjadala uwe wa kisayansi, evidence based.

Naamini watafikia muafaka. Akishaelewa anapokosea au alipopotoshwa na 'wataalam' wake, yeye mwenyewe atarudi kwa waumini wake aseme maswali yetu yote yameshajibiwa, nimejiridhisha kuwa chanjo ni salama, nendeni mkachanjwe.
 
Tatizo ni kuwa viongozi wetu wa juu wamedanganywa mno, Dkt Magufuli hakuwa mtu wa kumpelekea kitu bila kuwa na evidence na ndiyo maana ukiumwa kovid kwa sasa ukaenda hospitali lazima madakitari wafanye mbinu ufe ili wapate idadi kubwa ya waliofariki na kovidi. Ukiona dalili za kovid kaa nyumbani tumia mbinu zile zile tulizotumia wimbi la kwanza na la pili. Chanjo hii ni hatari mno.
 
Yaani na wewe ni wale wanaofikiria Gwajima hajui ukweli! huyu anapenda drama na awe kwenye TV
 
Tatizo la nchi yetu ni siasa. Wataalam wengi wameshaenda kwenye siasa. Hawana tena namna ya kuhangaika na taaluma zao isipokuwa siasa.
 
Back
Top Bottom