Application inayotoa mkopo direct kwenye simu yako kupitia M-pesa.

Mimi Niko na mkopo wa 40,000= baada ya mwezi natakiwa niwe nimelipa 45,540 na hiyo pesa imegawanywa katika makundi manne ambapo marejesho nafanya kila wiki. Nilianza na 10,000= nikazembea malipo nikawa dormant lakini nilipoanza malipo kwa kasi ya 4G mkopo ukapanda. Madhumuni yangu wanikopeshe kuanzia laki5 kwenda milioni ndio naweza kuona raha ya huo mkopo
jaribu na hii ni ndani ya dkk 5
Screenshot_2018-08-15_100902.jpg
 
masharti ya mkopo (BRANCH)



1. UWE NA LINE YA VODACOM YENYE HUDUMA YA M-PESA

2.UWE MTUMIAJI WA MTANDAO WA FACEBOO NA UWE UNAPAKIA PICHA (UPLOAD), KUCHANGIA NA KUWA MARA KWA MARA ONLINE..

3. FACEBOOK IWE KAMA SEHEMU YA MAISHA YAKO YA KILA SIKU.
umejaribu hii?
Screenshot_2018-08-15_100902.jpg
 
Huu utapeli sijui mtaacha lini, ngoja nifanye mpango na wenzangu kuwajulisha Google hizi apps za kitapeli watu wanazofungua, lengo ni kula pesa za download tu hakuna kingine

You are very right

Kuna moja mimi nilijaribu kui download ikakubali

Hatua ya pili nikaaifungua kisha nikaambiwa ni login au Register

Nikajaribu kujirejesta, nikaweka namba ya simu kisha baadaye kabla hata sijafikia mwisho nikaghairi...

Cha ajabu nikaletewa ujumbe wa eti "...you are successful registered for a loan....!! "

Aisee nilishangaa sana.

Nakubaliana na wewe kabisa, zingine ni za kitapeli haswaaa...

Lakini Hawa BRANCH INTERNATIONAL na TALA ni kweli ziko active na wanatoa mikopo ya kusaidia matatizo madogodogo na hata wenye kuhitaji mitaji ya kuuza nyanya ama vitumbua ama mama lishe....

Kwa hawa nimehakikisha na wako vizuri sana......wanasidia sana watu waaminifu!!
 
Back
Top Bottom