Apple kuwapa watumiaji wake uhuru wa kutengeneza simu zao wenyewe

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
9,786
2,000

a18828a4adf2c38a41326c1d3e305e9d.png
Kwa muda mrefu Apple imekuwa ikizuia wateja wake wasijitengenezee simu, Macs au vifaa vya Apple; au kutumia mafundi ambao hawajasajiliwa na Apple. Hali hiyo ilipelekea Apple kufunga na kuzuia watu wasirekebishe simu kwa mafundi wa mitaani ambao sio authorized na Apple.

Kutokana na baadhi ya maeneo kulazimisha sheria ya “Rights to Repair” Apple imelazimika kuachia uhuru kwa watumiaji wake kurekebisha simu wenyewe au kwa mafundi ambao hawajasajiliwa. Itasaidia wateja wa Apple ambao wana uwezo wa kutengeneza simu zao wenyewe, kuwa na uhuru wa kuagiza vifaa na spare za kurekebisha simu; na Mafundi wa Mitaani kuwa na uhuru wa kusaidia watu katika kuwatengenezea vifaa vyao bila kuharibu Warranty, FaceID kugoma baada ya kubadilisha kioo Au Error Message ya kusema battery sio Genuine.

Wateja ambao watahitaji kurekebisha simu zao wenyewe, mfano kubadili Battery, Kamera au Kioo; wanaweza kucheck Apple Repair and Repair Status Check - Official Apple Support na kuagiza spare au kutazama namna ya kurekebisha simu mwenyewe.

Hii ni good news hata kwa mafundi wa mitaani ambao wanaweza kurekebisha simu vizuri.

Mabadiliko haya yataanza Mwaka 2022, naitaanza kwa watumiaji wa iPhone 12 na iPhone 13 tu. Sehemu zilizoruhusiwa kubadilishwa ni Kioo, Kamera na Battery; pia ni muhimu kuhakikisha unabadili kwa kutumia vifaa Original
 
Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
9,786
2,000
Kama wametoa vitambaa vya kupangusia simu wanaviuza $25 hiyo kit ya kufanya repair nadhani wataiuza $600.
Ikija apple car nadhani tesla atapata tabu sana
Ngoja tusubiri tuone maana wanataka kuteka soko duniani
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
25,559
2,000
Watu wana mahaba na apple mkuu we acha. Mimi nilishangaa kitambaa kimefungwa hafi kwenye box tena kimekunjwa kwa style moja matata na kinauzwa $25 na wameuza kama njugu.

Huenda hata gari akauza sana maana anaiba ma engineer wa tesla

gari sio simu,jiulize kuna PC ngapi za mac ofisini mkuu mbali na kuwa bora??

kwenye magari kule ubora na uzuri sio kigezo cha kuuza,bali ni bei ndio inaamua.kuna gari kali na bora ila sababu tu zinauzwa millions of money watu zinawashinda,zinabaki kuwa za watu wachache tu.
sasa kwa tabia ya apple,tutegemee atakaa level za akina maybach,wagon,lambo,RR,buggat,teslank ambako huko mahaba hayafanyi kazi ni hela tu ndio zinaongea.
ili asumbue wote hapo gari zake ziwe za bei chee,kitu ambacho sio utaratibu wake.
 
Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,806

Obviously ataenda kupambana na tesla sidhani kama kalenga kutengeneza gari za level kama ya buggat.
Kwenye magari ubora wa gari una matter sana. Hivi unajua kwamba toyota anaongoza katika kuuza magari marekani akifuatiwa na ford? Ukisoma sababu wanazotoa, wanasema gari za toyota ni reliable sana tofauti na za makampuni ya ndani.
Yes, gari siyo simu ila sidhani kama wamelenga soko hilo la akina buggat, nadhani watakuwa wanalenga soko la watumiaji wa kawaida hao hao tesla like.
Ngoja tuone
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
10,537

Ford ndie anaongoza Toyota ni duniani kwa ujumla ila ukija soko la marekani sio kihivyo. Brand kama Ford, Chevrolet kwa marekani ndizo zinauza sana na wana magari mengi sana ya kisasa ambayo Toyota hafui dafu inapokuja swala la performance.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom