App ya kupokea Wageni toka Nje (Couchsurfing) : Hivi ndivyo ninavyopokea wageni na kutengeneza pesa

Mbona kimnya hakuna mirejesho au ndo hamtaki na wengine tutoboe
Apps zipo nyingi mno ila zote ni za kulipia ili uwe verified, cha msingi uwe na sehemu za kupokea wageni yaani uwe na chumba au nyumba na iwe na fanicha ili wageni wawe na pakukaa, utapokea wageni wa kizungu kila uchao utachoka wewe tena wanawake ndio wengi
 
Una nyumba ambayo haina mtu. Unajisajili kwenye site yao. Kama uko mji A na kuna mgeni anataka kuja huo mji, anaingia kwenye site yao ana-search. Akichagua nyumba yako ulioisajili basi akija anakaa pale kwa muda alio-book. Fedha zinalipwa moja kwa moja AirBNB na wao wanaingiza kwenye account yako baada ya kuchukua commission yao. Ni kama Uber tu inavyofanya kazi lakini hapa ni nyumba badala ya gari.
Vipi kama nipo kwenye nyumba ya kupanga?
 
IMG-20230313-WA0004.jpg
nilifungua account sikuingia kwa muda kumbe kuna mtu kanitafuta hakunipata aka cancel duh 😂wabongo sisi
 
Shukrani mkuu.

Fanyia kazi hizi opportunity.

Nimeweza fungua tours company kwa njia hizi za kukutana na wageni na kuwauzia safari packages
Global Citizen hii kitu nimejifunza iko vizuri je hii unaweza pokea wageni na kuwadirect kwa hoteli za kitalii au ni lazima wafikie ninapoishi??
 
Hv hii unaweza poker wageni na kuwapeleka may be hotel za kitalii au ni lazima wewe ndo uwahost
 
Hv hii unaweza poker wageni na kuwapeleka may be hotel za kitalii au ni lazima wewe ndo uwahost
Nyingi zinataka wewe ndio uwe host ndio maana nyingi zinataka uwe na nyumba au chumba, mgeni au wageni wakija unawapokea wanakaa, kwa muda na wageni wanakulipa wakikuelewa kukukatia tiketi za kwenda Ulaya,Asia au Amerika ni kawaida sana pia inakuwa rahisi kukuletea au kuwaelekeza wenzao kuhusu wewe kikubwa kuwa muaminifu.
Ndugu yangu anakaa nyumba ya urithi ana vyumba vitatu kaboresha anafanya hii shughuli sometimes upokea wageni hata 10 wanakuja fanya utafiti labda wa mimea, magonjwa au hali ya maisha, kwa siku wanamlipa $10 mpaka 20$ kila mmoja hukaa hata mwezi anafaidika sana kwasababu hawapendi kukaa hotelini ni gharama.


Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hii kitu nzuri sana kwa wananchi wa Tanganyika maana serikali haijawabana sana local tour guide ila kule nchini Zanzibar sheria zao ni kali sana na zinawalinda guide wao.
 
Dah sitasahau nilikutana na mzungu Kigoma kupitia couchsurfing...ile nakutana naye stend tunaagana ananishika mkono kama dakk 3 nzima haniachii, nikapata alarm ya ugasho tokea hapo nikamkimbia.
Akawa anapiga masimu kama mvua.
 
Kwa wale mloopokea wageni jamani je ni lazima kuwa verified ndo upate info zakuja kwa mgeni au utafutwe?Faida za kuwa verified na kutokuwa verified ni zipi katika kupata wageni?nisipokuwa verified sitapata mgeni?
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom