App yenu ina bugs za kutosha tu. Mlifikiria nini kutengeneza app kama hii kwa kutumia php? Hiyo sio language Inayo weza kumaintain functionality zote hizi. Nawashauri mfanye redesigning tumieni Flutter au react native.

App mpaka saivi haioneshi pics
App haitoi notifications
Baadhi ya threads hazifinguki.
Nakazia halafu Wala hawajali ila yana mwisho haya ipo siku itatokea app bora na tutaipiga chini.
 
Jf ilikua zamani siku hizi hakuna kitu.utaalamu umezidi hadi wameharibu.Itakua wameamua ijifie kifo cha asili taratibu kwasababu ata ule ugreat thinker ulishakufa kifo cha mende sasa hivi ni mataputapu tu.mtu akikirupuka uko na utindio wake wa ubongo anakuja kupost vingine ata havieleweki.
Hakika, kwa sasa maudhui ya jf haina tofauti na Facebook
 
Jf ilikua zamani siku hizi hakuna kitu.utaalamu umezidi hadi wameharibu.Itakua wameamua ijifie kifo cha asili taratibu kwasababu ata ule ugreat thinker ulishakufa kifo cha mende sasa hivi ni mataputapu tu.mtu akikirupuka uko na utindio wake wa ubongo anakuja kupost vingine ata havieleweki.
Sasa hilo ni tatizo la JF au la jamii. Unawataka JF wafanyeje ili watu waache kuposti mataputapu.

Mataputapu hayo ni zao la jamii yetu na mfumo wetu wa hovyo wa elimu japo vijana wetu wanapata A za kutosha tena za points 7 tu. Lakini ukikaa nao ni weupe kichwani balaa. Hata wanaotoka vyuo vikuu ni hivyo hivyo.

Hili si tatizo la JF peke yake. Graduate hana uwezo wa kujenga hoja hata kwa jambo dogo tu na anachojua ni kuporomosha matusi basi...

Kazi tunayo wallahi!
 
Back
Top Bottom