Apoteza maisha kwa kuudhiwa na mke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Apoteza maisha kwa kuudhiwa na mke

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Saint Ivuga, Mar 21, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  Mwingine huyu hapa! Apoteza maisha kwa kuudhiwa na mke
  [​IMG]
  Thursday, March 17, 2011 10:57 AM
  MKAZI wa Mbezi Juu Mtoni jijini Dar es Salaam, aliyefahamika kwa jina la Shabani Kihundo (30), amekutwa amekufa akiwa chumbani kwa kuhisiwa kunywa sumu kwa kuudhiwa na mkewe katika ujumbe aliouacha chini ya kitanda. Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Bw. Charles Kenyela alisema kuwa, Kihundo alikutwa amekufa juzi chumbani kwake majira ya saa 7 mchana akiwa amelala kifudifudi.

  Kamanda Kenyela alidai kuwa, Kihundo aliacha ujumbe uliooneshwa kuwa kulikuwa na ugomvi kati yake na mkewe ujumbe aliokutwa chini ya kitanda chake.

  Kamanda Kenyela alifafanua kuwa ujumbe huo ulisomeka hivi: “Nimejiua kutokana na kutoelewana na mke wangu, nimeona nimuachie dunia name niondoke duniani nikatulize nafsi yangu japokuwa nilimpenda”

  “Nimekuachia hiyo nyumba,japo kuwa ulininyima haki yangu, mimi ni mwanachama wa NSSF na kadi yangu anayo mke wangu,

  “Yeye apewe milioni moja ili ziweze kumsaidia kwa sababu atakuwa na maisha magumu, nimeahca baiskeli apewe mdogo wake mke wangu pamoja, nguo na viatu”

  “Pia Samweli ananidai shilingi 28,000 asante”ulimaliza ujumbe huo

  Maiti imechukuliwa na kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huyu atakuwa mhehe tu!
   
Loading...