Apoteza maisha kwa kushambuliwa na tembo, Handeni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Mtu wa pili amepoteza maisha ndani ya wiki moja baada ya kushambuliwa na tembo wanao endelea kuzurura hovyo kwenye makazi ya watu katika mtaa wa malezi wilayani Handeni mkoani Tanga.

Akiongea na ITV akiwa hospitali ya wilaya ya Handeni ulipohifadhiwa mwili wa marehemu ambaye amejulikana kwa jina la Mwanahawa Mohamed, mume wa marehemu amesema mke wake amekutwa na tukio hilo, asubuhi ya leo wakati akiwa na wajukuu zake wakichimba muhogo kwa ajili ya futari.

Aidha, Baadhi ya wananchi wilayani humo wamesema kuwa hofu yao imeongezeka kutokana na tembo hawa kushindwa kudhibitiwa mpaka sasa hali inayo sababisha baadhi yao kushindwa kwenda mashambani kupalilia mazao yao huku waliopo mjini nao wakiwa hawana amani baada ya hivi majuzi tembo hao kupita karibu na makazi ya Mkuu wa Wilaya.
 
Huyo marehemu angefanikiwa kuuwa Tembo kuna uwezekano angedakwa kwa tuhuma za ujangili
Ni kweli. Serikali yetu hazijali maisha ya wananchi wake. Kuna sehemu walichoka na huu ujinga wa kunyanyaswa na wanyama na serikali inajifanya haioni wakaamua kuweka sumu kwa siri kwenye malisho yao. BTW wahanga wa matukio kama haya walistahili kulipwa fidia kubwa sana.
 
Jana niliona kwa taarifa ya habari yani mfiwa anaongea anatabasamu kama vile aliyekufa sio mke wake.
 
Watu wa Tanga nao ni laini laini sana,wanaume wao wanashindwa kuji organise na kumtafuta huyo tembo.hawaoni kule Serengeti Wakurya wanavywafanya hao wanyama.
 
Ninaona kila dalili za serikali kuzidiwa kuhusu uhifadhi wanyama. Kitakachotokea ni wanyama kuangamia. Binadamu hawezi kukubali kutawaliwa na mnyama. Poleni wafiwa
 
Na tembo akiua ataendelea kuua tu anajua binadamu yeyote ni adui yake mkubwa kinachotakiwa ni kumtafuta huyo muuaji wa binadamu na hata akiwa kwenye kundi akiona watu yeye anakua na mchecheto zaidi na kujitenga kwa kuinua masikio yake juu yaani muda wowote ni vita tuu...poleni sana wafiwa kwa tukio hili
 
Back
Top Bottom