Aponda gari lake bandarini kwa kukerwa na urasimu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aponda gari lake bandarini kwa kukerwa na urasimu!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Akili Unazo!, Jul 31, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,790
  Likes Received: 2,452
  Trophy Points: 280
  Jamaa mmoja alipandwa na jazba na kuamua kuliharibu gari lake jipya kutokana na urasimu katika bandari ya nchi yao.

  Mtu huyo aliagiza gari hilo kutoka china lilikuwa maalumu kwenye birth day ya mpenzi wake.

  Baada ya gari hilo kuwasili jamaa alikuwa anazungushwa na maofisa wa badnari kwa siku kadhaa.

  Jamaa huyo alifika tena bandarini hapo siku hiyo ambayo ilikuwa siku ya kuzaliwa mpenzi wake akiwa na matumaini ya kutoa gari hilo lakini ikashindikana na ndipo akaamua kulipondaponda.

  Chanzo cha vuta nikuvute kulitokana na kuwa gari hilo aina ya Aixam 500 lilikuwa halijulikani kama dereva wake atatakiwa kutumia leseni ya aina gani kati ya ile ya gari au pikipiki.

  Wakuu kumbe ukiritimba upo bandari zote duniani?

  Je kazi ya watu wa bandarini wanahusika kujua aina ya leseni itakayotumiwa na dereva kuendeshea gari huiska?

  Au hii sheria ipo huko Serbia kwa Kondic?

  Huyu jamaa nahisi kwa Tanzania nahisi angechomaa bandari nzima kwa ukiritimba tulionao tunaongoza.
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hasira hasara
   
Loading...