Apona ghafla tu baada ya Gari ya Wagonjwa iliyokuwa ikimkimbiza Hospitali kupata Ajali na Kuua Muuguzi na Dereva

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
MGONJWA aliyekuwa akiwahishwa katika Hospitali ya Wilaya Same, Ester Paresetwi (35) na gari likapinduka na kuua muuguzi na dereva amepona mara tu baada ya ajali.

Katika ajali hiyo ya gari la wagonjwa, muuguzi wa zahanati ya Kisiwani wilayani humo, Joshua Jacob (29) na dereva, Jumanne Makumbe (48) walikufa na wengine watatu walijeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema jana majeruhi akiwemo mgonjwa aliyekuwa akipelekwa hospitali wanaendelea vizuri katika Hospitali ya Wilaya ya Same.

Alisema ajali hiyo ilitokea eneo la Majevu Kata ya Kisiwani wilayani Same Agosti 7 mwaka huu saa 10 jioni wakati tairi la nyuma la gari lilipopasuka, likapoteza mwelekeo na kupinduka.

Chanzo: HabariLeo
 
Huwa sielewi kwanini ambulance zinaendeshwa kwa kasi hizo hasa huku Tanzania ambapo miundombinu ya barabara sio rafiki.

Haraka ya kuokoa maisha ya mtu mmoja inaweza kusababisha vifo vya makumi ya watu. Kuna haja ya kutafuta suluhisho la jambo hili.
Je, unadhani kama Mgonjwa kapona ghafla tu baada ya Ajali hiyo na kuwaua hao waliokuwa wakimuwahisha Hospitali Dereva na Muuguzi alikuwa anaugua Ugonjwa gani?
 
Mungu anamaajabu yake acha aitwe Mungu
Hiyo ni sayansi mkuu, kwa vile huna majibu unasingizia mungu,

Linapotokea tukio la hatari ghafla mwili wa binadamu huzalisha hormone iitwayo endorphin hii huzalishwa kwenye pituitary gland au kwenye neurone za ubongo, kemikali hii hufanya kazi ya kuyazima maumivu na kukufanya uwe na nguvu au afya njema kwa muda ili ukabiliane na hatari kwa muda flani,

Hujawahi kusikia story za mgonjwa wa miguu au mlemavu kusimama na kutimua mbio baada ya kuona simba au nyoka mkubwa?

Hujawahi kuchinja kuku kabla hajafa ukamuachia akatimua mbio?

Basi hiyo ni endophin hormone ndiyo inayofanya yote hayo kikemikali inafanana na cocaine
 
Je, unadhani kama Mgonjwa kapona ghafla tu baada ya Ajali hiyo na kuwaua hao waliokuwa wakimuwahisha Hospitali Dereva na Muuguzi alikuwa anaugua Ugonjwa gani?
Mimi hoja yangu sio hiyo mkuu. Mimi ningependa tuwe na njia mbadala za kuweza kuokoa maisha ya watu kuliko hii ya kukimbiza magari kwa kasi ambayo inaweza kusababisha vifo vya watu wengi zaidi katika harakati za kuokoa mtu mmoja.
 
Hiyo ni sayansi mkuu, kwa vile huna majibu unasingizia mungu,

Linapotokea tukio la hatari ghafla mwili wa binadamu huzalisha hormone iitwayo endorphin hii huzalishwa kwenye pituitary gland au kwenye neurone za ubongo, kemikali hii hufanya kazi ya kuyazima maumivu na kukufanya uwe na nguvu au afya njema kwa muda ili ukabiliane na hatari kwa muda flani,

Hujawahi kusikia story za mgonjwa wa miguu au mlemavu kusimama na kutimua mbio baada ya kuona simba au nyoka mkubwa?

Hujawahi kuchinja kuku kabla hajafa ukamuachia akatimua mbio?

Basi hiyo ni endophin hormone ndiyo inayofanya yote hayo kikemikali inafanana na cocaine
Sayansi yako hii ni ya kweli kabisa

lakin kwasababu na wewe hujui lolote kuhusu Mungu. Basi huna budi kubaki na sayansi yako tu
 
Hiyo ni sayansi mkuu, kwa vile huna majibu unasingizia mungu,

Linapotokea tukio la hatari ghafla mwili wa binadamu huzalisha hormone iitwayo endorphin hii huzalishwa kwenye pituitary gland au kwenye neurone za ubongo, kemikali hii inafanana na cocaine
Sayansi imejaa uongo na nadharia nyingi Sana.Sasa hiyo hormone aliyeiweka ni nani km si MUNGU?.
 
Amepona ? Alikuwa anaumwa nini Kabla ?

(Adrenaline) Hormone ya Flight or Fight ilifanya kazi yake.... Hata wewe usishangae ukikutana na majambazi ukapata ujasiri wa ajabu wa kupambana nao, au ukipata ajali usisikie maumivu mpaka baadae kidogo (hio ni njia ya mwili kuji-protect)
 
Alikua anatoka damu masikioni na mdomoni

Ila baada ya ajali damu zikakata

Akapona yeye na ndugu zake (wasindikizaji) dereva na nesi wakang'ata vumbi

Tena ilikua mita chache kufika hospitali ya wilaya (Destination )
 
Back
Top Bottom