Apigwa na kuchomwa moto akidaiwa kumuua mkewe kwa shoka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Picha

MKAZI wa Kijiji cha Chiwata, Kata ya Chiwata wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara, Juma Lugomba (61), ameuawa kwa kupigwa na mwili wake kuchomwa moto.

Wananchi wamemuua Lugomba baada ya mwanaume huyo kumshambilia mkewe kwa shoka na kumuua.

Tukio hilo limetokea katika kijijini Chiwata, na limethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Mzee alisema inadaiwa juzi saa 3 usiku, Lugomba alimshambulia mkewe Yolenda Milanzi (59) na kitu chenye ncha kali na kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo baada ya kumjeruhi vibaya kichwani.

Alidai mkazi huyo baada ya kufanya mauaji hayo kwa mkewe, kundi la wananchi wenye hasira kali waliamua kumsaka na walipomkamata walimjeruhi kisha kumchoma moto hadi kusababisha kifo chake na yeye.

“Ni kweli tukio hilo limetokea mume kumshambulia mke wake na kumuua, lakini baada ya yeye kufanya mauaji hayo asubuhi yake wananchi waliamua kumsaka na walipomkamata walimjeruhi kisha kumchoma moto hadi kufa,” alieleza DC huyo.

Alisema bado chanzo cha mume huyo kufanya mauaji kwa mkewe hakijafahamika, lakini Polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.

Mtendaji wa Kijiji cha Chiwata, Thawabu Mturi alisema mume huyo baada ya kufanya mauaji, alikimbilia kijiji cha jirani cha Pemba kujificha ili kukwepa ushahidi.

Alisema wananchi walipogundua kuwa mume huyo amemuua mke wake, walipandwa na hasira ndipo walipoamua kumtafuta wakiwa na wabeba silaha za kijadi na walipogundua kuwa amejificha katika kijiji jirani walifika huko na walifanikiwa kumkamata hivyo walimjeruhi kisha walimchoma moto hadi kufa.
 
Sheria mkononi watajuaje km amefanya mauaji?
Ila miaka 61 bado unakuwa na wivu wa mapenzi?
 
Afu bado tu kuna mawatu yanapinga kuwa Yesu hatarudi tena? nakati yote haya yalitabiriwa kadri maarifa yatavyoongezeka ndivyo Watu tutavyozidi kuwa manyang'au.

MATHAYO 24.
 
Back
Top Bottom